Wawekezaji waanza kujiondoa Tanzania

.............ajira zipatazo zaidi ya 150,000

Yaani jamaa wamechuma sana kwa kuchukua madini yetu yote bila kodi eti kwa kutuletea ajira 150,000 tu, tena zile za chini. Wanaona sasa wameacha mashimo tu na kutuona hatuna maana tena; ama wametufanya sisi ni kondomu au tulijifanya wenyewe kuwa kondomu zao.
 
Mwandishi amekosea kidogo. Uwekezaji katika migodi tu ni zaidi ya Dollar Billion 5. Hiyo 433 Million haitoshi hata kujenga mgodi mmoja mkubwa.

Inasikitisha sana kuwa wawekezaji wakubwa namna hii wanaodoka. Inasikitisha zaidi unaposoma mabandiko ya wana great thinkers yanayosema uwekezaji ni unyonyaji. Kwa mtindo huu tutaendelea kuwa omba omba huku tumekalia utajiri.

Dunia nzima ni hawa hawa akina Barrick, Anglogold etc wanaofanya hizi shughuli. Ni kwa nini ishidikane hapa TZ tu?

Kinachowaondoa Barrick si sera ni gharamaza uendeshaji kutokana na matatizo ya umeme sifa kubwa ya Barrick ni kwenye cost control ni moja kampuni inayotolewa mifano sana kwenye somo la cost management hasa kwenye kipengele cha cost analysis na profit ratios wao target kubwa ni cost control tofauti na makampuni mengine ambayo target yao ni bei ya kuuzia. kama watahakikishiwa upatikanaji wa umeme Barrick wataendelea kuwepo Tanzania.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Back
Top Bottom