Wawekezaji wa migodi wazidi kuitafuna serikali...tazama hii!

Wewe umechelewa sana kugundua utata miongoni mwa irregularities nyingi kwenye mikataba ya wawekezaji wa migodi. Je umewahi kuwajulisha wananchi kuwa zaidi ya GOLD inayochimbwa pia huwa wanachimba PLATINIUM. Kama ukiwafahamisha wananchi labda watafungua macho na kudai mikataba yote ibatilishwe na ifanyike mipya kwa maslahi ya taifa. Wananchi wenzangu hembu tengeni muda mdogo kila siku ili mjiulize: KWA NINI UDONGO WENYE DHAHABU SIKU ZOTE UNAPELEKWA NJE YA NCHI KWA KISINGIZIO UNAPELEKWA KUSAFISHWA NA KWA NINI HAPAJAJENGWA MTAMBO WA KUUSAFISHA UDONGO HUO HAPA NCHINI HATA AKIPATINA MWEKEZAJI WA KUUJENGA.

What does a fish know about the water in which it swims all its life?
Mkuu,
kinachochimbwa huko siyo gold na platinum peke yake.
Kuna madini mengine kama vile copper, nickel, iron ores....n.k. lakini kuna ile ile wanaita "major" na hayo mengine ni "minor". Na wao wameingia mkataba wa kuchimba gold tu. Hivyo vingine ni ziada ama takataka. Wanasema siyo commercially viable. Cha ajabu wao hawaachi hata chembe ya madini ya aina yoyote ile kwenye mchanga.

Tupo tunachekelea tu.

Na utakuta Mtendaji mkuu wa Barrick kwa mfano, ni Mtanzania. Lakini anaweza kuitetea kampuni kuliko hata mmiliki (mzungu).
Hivi tumelogwa!?
 
Mmeliwa kudadadeki
Kinachoshangaza ni kuwa hata hao viongozi wakiongea kwenye vyombo vya habari wanaonekana wanajua makosa yanayofanyika, tena huwa wanaahidi kutoyarudia. Cha ajabu hazipiti siku nyingi hao hao tena wanafanya ******.
 
mi nadhani aliyesema wabunge wanawaza kwa kutumia ****** hakukosea, huyu ngeleja naer ni mbunge. KAtumwa na nani aturundikie mihasira? kwanini wanarudia makosa yale yale kila siku? watuachie nchi yetu sasa hawa maandazi, nimewachoka kabisa, sitakim hata kuwasikia. Wanachochea vita hawa, tuingie road watuangamize na risasi za moto.
 
Fikiria na utaona kua sera ya CCM ni kuvutia wawekezaji kwa hali yeyote ile, hadi JK anatembea na mafaili ya uwekezaji kokote aendako - mikataba inafanyika popote hata njiani.

Mimi naamini baada ya huu mradi wa maji kukamilika Kampuni itachangia mapato kwa 80% na wananchi 20% tu. Lakini serikali ya CCM haiwezi kusema hayo mambo kwa kua wanataka kuchakachua asilimia 50% ya mapato. Miradi mingi ya serikali ya CCM mapato yake wale hayaeleweki - ni siri ya serikali. Serikali ya CCM lazima ijifunze kuelimisha raia kuhusu miradi yake hasa kuhusu mapato.
 
Spidi ya Ujuha tu ndio imezidi kutawala, hata kwenye kona kali watu wanapita na 120km/h.
 
Fikiria na utaona kua sera ya CCM ni kuvutia wawekezaji kwa hali yeyote ile, hadi JK anatembea na mafaili ya uwekezaji kokote aendako - mikataba inafanyika popote hata njiani.

Mimi naamini baada ya huu mradi wa maji kukamilika Kampuni itachangia mapato kwa 80% na wananchi 20% tu. Lakini serikali ya CCM haiwezi kusema hayo mambo kwa kua wanataka kuchakachua asilimia 50% ya mapato. Miradi mingi ya serikali ya CCM mapato yake wale hayaeleweki - ni siri ya serikali. Serikali ya CCM lazima ijifunze kuelimisha raia kuhusu miradi yake hasa kuhusu mapato.
Hatukatai "kuwavutia" wawekezaji!
Unaposema unavutia wawekezaji ni kuwa unawapa unafuu wa vitu ambavyo walitakiwa wavigharamie. Madhumuni makubwa ni kuwa pindi biashara yao "itakaposimama" na kuweza kujiendesha basi Taifa liweze kufaidika.
Sasa hawa tunawagharamikia kila kitu...hata mtaji tunakwenda kukopa kwa dhamana ya nchi yetu then tunawapa wao.
Kodi hawalipi.
Huo mrabaha ndo kama hivyo 3% ambayo hakuna evidence kuwa tunapata, na kama tunapata haijulikani kama tunapata hiyo 3% kwelikweli.
Jamii zinayozunguka migodi zinaachiwa zawadi ya mahandaki na sumu zinazotumika kusafishia madini (vizazi vyetu vinazidi kuathirika kibayolojia).
Wafanyakazi migodini wananyanyaswa (kuna ukaguzi ambao unavuka mipaka ya kibinadamu). Hakuna pia uwiano wa malipo kwa wafanyakazi wa kigeni na wale wazalendo, hata kwa kazi zinazolingana.
Pesa yote inakwenda nje.

Kwa mwendo huo ni nini faida ya "kuwavutia" wawekezaji.
 
Back
Top Bottom