GHIBUU
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 4,432
- 3,006
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka CUF na CCM leo hawakutafuna maneno na waliungana pamoja kueleza waziwazi kuwa Mswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba unapaswa kuwapa fursa wananchi kujadili mambo yote likiwemo Muungano na kwamba iwapo wanaona hauna maslahi nao na wakataka usiwepo, basi maoni hayo yaheshimiwe maana mamlaka ya nchi yanatoka na yanaamuliwa na wananchi wenyewe. Samwel Sitta aliondoka na ujumbe huo.