Wawakilishi wahoji uhalali wa kuhojiwa na vyama vyao

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=2][/h] Mwakilishi wa jimbo la Chakechake Omar Ali Shehe

Mwakilishi wa jimbo la Chakechake Omar Ali Sheikh amehoji uhalali wa vyama vya siasa kuwahoji wajumbe wa baraza la wawakilishi kufuatia hoja wanazozitoa katika vikao vya baraza hilo zinazokwenda kinyume na sera za vyama hivyo.
Akizungumza katika semina ya elimu ya katiba amesema chombo hicho cha wananchi sasa kinaelekea kujali zaidi maslahi ya nchi badala ya vyama vya siasa, lakini amedai kuna watu wachache wasiojali uzalendo na kutaka kuwayumbisha wananchi.
Shehe amesema katika mjadala wa bajeti unaondelea baadhi ya wawakilishi wamejaribu kuitwa na vyama vyao ili kuhojiwa juu ya msimamo wao wa mfumo wa muungano walioutoa ndani ya baraza hilo.
Amesema kitendo hicho kinakwenda kinyume na sheria namba nne ya mwaka 2007 kuhusu kinga na fursa za wajumbe wa baraza hilo wanapokuwa ndani vikao vya baraza…
Nae waziri wa sheria na katiba Zanzibar Abubakary Khamis Bakar ameshauri utowaji wa maoni hayo, sera za vyama vya siasa havina budi kuwekwa pembeni wakati wa kujadili maslahi ya Zanzibar
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom