Wachovu
JF-Expert Member
- Jun 25, 2012
- 1,227
- 565
Acheni porojo.tupeni data kama amendments za mipaka baada ya treaty ya mwaka 1890 kama alivyokuwa anaelezea Waziri Membe mwaka 1947...........bungeni, na maazimio ya umoja wa mataifa kuhusu mipika ya kwenye maji,milima,mito n.k.tuone kama tuna hoja vinginevyo hawa wamalawi watatuzidi kwa hoja yao.tutapoteza ziwa lote,wavuvi wetu watatozwa kodi na mengineyo,ni sawa na kuuza baraza ya nyumba yako wakati bado unaishi ndani ya nyumba.
Waafrika tunapashwa kuwa watu wa hekima , Hapa ni hekima na busara inapashwa kutawala ,tuachane na mambo ya wakoloni ambayo kwa akili ya kawaida unajua jambo hili si sahii.Kama Malawi wanasema ziwa lote upandewa Tanzania nia lao ina maana watu wanaoishi kando ya ziwa upande wa Tanzania itawalazimu wakachukue visa kwenda kuchota maji ziwa Nyasa ? Hapa ni kutumia busara wala sio sheria za kijinga jinga tunazoambiwa.
Nitoe mfano wa mto Kagera tunajua kuwa unatoka mbali na kupitia Tanzania na kwa kuwa unapita kwetu ni mali yetu tunaweza kufanya tunavyotaka hata kubadirisha maji yapite kwingine. Tukifanya hivyotutakuwa tumetangaza vita na nchi za waarabu. Sasa basi na watu waliokando ya maziwa haya yetu tuliyonayo wanayo haki ya kuyatumia na utakuwa unatangaza vita kama ukitaka kuwakataza kutumia hii zawadi waliyopewa na Muumba wao. Mipaka inawekwa kwa kutumia busara sio sheria wakati unaona jambo hili litaleta matatizo