Wavamizi' 100 wa ardhi wakamatwa K'ndoni, nyumba 500 zavunjwa

armanisankara

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
283
49
Zaidi ya wananchi 100 wamekamatwa katika Operesheni iliyoanza juzi ya kuwaondoa watu waliovamia maeneo yasiyo yao, inayoendeshwa katika eneo la Nakasangwe, Kata ya Wazo, wilayani Kinondoni chini ya Kamanda Charles Kenyela ambaye pia ni Kamanda wa kipolisi wa mkoa huo, kwa makosa ya kuvamia maeneo ya watu, kulishambulia jeshi la polisi wakati likiingia kutekeleza zoezi hilo kwa kutumia silaha za jadi ambazo ni panga, shoka, upinde na mawe pamoja na kukutwa na pombe haramu ya gongo.

Aidha, zaidi ya makazi ya kudumu na siyo ya kudumu 500 yamebomolewa kufikia jana katika operesheni hiyo.

Kamanda Kenyela aliiambia NIPASHE jana kwamba operesheni hiyo haikupata upinzani wowote kwa siku ya jana.

“Leo (jana) tumeingia hapa Nakasangwe tukianzia kwenye kitongoji cha Kaza Roho kwa amani, na hatukupata mtu wa kutuzuia, kuturushia chochote na kwa kweli kuko shwari kama unavyoona.Wengi wa wananchi waliopo wanatoa vifaa vyao na sisi hatuna tatizo la kumzuia mtu anayetoa mali yake, kwa kuwa lengo letu sisi kama tulivyokuwa tumewaambia toka awali, ni kuwa hatutaki watu wa kuvamia maeneo ya wenzao,” alisema.

Alisema polisi jana haikurusha bomu hata moja la kutoa machozi wala risasi katika eneo hilo kwa kuwa hali ilikuwa shwari.

Kamanda Kenyela alisema wakati wa operesheni hiyo jana walifanikiwa kuvunja nyumba moja ambayo iligundulika kuwa ndiyo ilikuwa inatumiwa na wavamizi kama Ofisi ya Serikali ya Mtaa huo katika kitongoji cha Kaza Roho ambapo walikuta mihuri, nakala ya hati za mauziano ya maeneo ya watu zilizokuwa zikisimamiwa na serikali hiyo bandia, nakala ya barua ‘feki’ zilizokuwa zikiwatambulisha wananchi wa maeneo hayo kama wakazi halali pamoja na ubao wa matangazo.

Aidha alisema kwamba waliweza kuvunja vile vile shina la wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) la Kinondo C lililokuwa limejengwa kwenye eneo la mmiliki aliyekuwa amevunjiwa nyumba yake na wavamizi, kufukuzwa na mbuzi wake 50 walichinjwa na wavamizi hao.

Alisema polisi pia wamewakamata wanawake watatu na dalali wao waliokuwa wameletwa kuonyeshwa eneo la kununua ambalo linamilikiwa na mtu mwingine.

Kamanda Kenyela aliwaasa wananchi wanaomiliki maeneo yao katika eneo hilo na maeneo mengine jijini Dar es salaam, kutoyaacha kwa muda mrefu bila kuyatembelea wala kuyaendeleza kwani yanapobaki hivyo, yanageuka kishawishi kwa baadhi ya watu kudhani hayana wenyewe na hivyo kuyavamia.




CHANZO: NIPASHE

 
hesabu ya karibu kila mmoja kwenye hao mia ataleta mtu 6 kujiunga kwenye jahazi la ukombozi cdm toka kwa mkoloni mweusi nape
 
Kwani CDM kinashabikia uporaji wa ardhi za watu?


tatizo la ardhi limetengenezwa na ccm ...nchi yetu ni kubwa hatuna haja ya kugombea ardhi mipango tu kaka ya cdm itarekebishwa kiulaaiini ...fikiria toka mtwara hadi dar au moro hadi dar mapori tuuuuuu

pakipimwa kila mahali miuundo mbinu ikawekwa nini tabu ....hakuna wafugaji wala wakulima kugombana ukzingatia pesa ya kupima unalipa wewe mwananchi ..umeme unalipa nguzo millioni maji unalipa watoto siku hizi tunasomesha wenyewe dawa tunanunua wenyewe pesa yetu ya kodi wanajilipa wenyewe kwenye viyoyozi

 
Inasikitisha sana kuona watanzania wakinyanyaswa katika nchi yao eti ni wavamizi! Huwa najiuliza wale wahamiaji haramu wa kutoka rwanda (zaidi ya elfu 30 kwa mujibu wa vyombo vya habari) kule Karagwe ambao wananchi wanawalalamikia mbona hawafurumushi kwa nguvu za ziada kama zinazofanyika huko madale, mabwepande n.k?
 
Back
Top Bottom