Waumini Anglikana sasa wataka akaunti za Askofu Baji zizuiliwe

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
Waumini Anglikana sasa wataka akaunti za Askofu Baji zizuiliwe
Maingwa Mohamedi na Hussein Semdoe,Tanga

WAUMINI wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dayosisi ya Tanga, wametoa tamko la kutaka kuzuiliwa kwa akaunti zote za Askofu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Dk Philip Baji.

Waumini hao pia wanataka kiongozi huyo azueliwe kusafiri nje ya nchi hadi hapo tuhuma dhidi yake zitakapopatiwa ufumbuzi.

Tamko hilo limetolewa na waumini wa dinare ya Maramba wilayani Mkinga na wenzao wa Tanga.

Katika barua yao, iliyosainiwa na mchungaji William Mbuji ambaye ni Mwenyekiti wa Dinare ya Maramba na mchungaji Aidano Mtoi ambaye ni Katibu, wamesema tuhuma za ubadhilifu wa fedha za wafadhili zinazomkabili ni Dk Baji ni nzito na kwamba zinapaswa kushughulikiwa.

Uongozi wa dinare hiyo umesema pamoja na mambo mengine, umeamua kusitisha taratibu za uwasilishaji wa fedha za DCF, kwaresma, msamaria mwema na michango mingine, kama njia ya kumshinikiza kiongozi huyo kujiuzulu.

Kwa upande wao, waumini wameamua kusimamisha michango yote kutoka kwenye mitaa yao hadi hapo uongozi mpya utakapoweka taratibu nzuri zitakazojenga imani kwa kanisa.

Walisema kwa sasa fedha zinazotokana na michango hizo zitatunzwa katika akaunti za mitaa.

" Hatuna imani na utendaji wako (Baji) kwa hivyo utoke ili tujenge upya uhusuiano na marafiki zetu,“ ilisema sehemu ya barua yao ya Februari 19 mwaka huu kwenda kwa askofu huyo.

Waumini pia wanataka mali zote zinazodaiwa kuchukuliwa na kiongozi huyo isivyo halali yakiwemo magari, nyumba na pikipiki zizuiliwe hadi hapo taratibu za kisheria zitakapokamilika.

“Tamko hili la upendo katika kujenga heshima ya doyasisi yetu ili mambo yote yafanyike kwa utaratibu, jambo hili siyo tu kuwa ni kero kwetu sisi waumini lakini pia halimpendezi Mungu“ ilisema sehemu ya barua hiyo.

“Tunawasilisha tamko la pamoja lililotokana na kikao chetu cha pamoja tulipokuwa tukijadili hali hii iliyotuletea maumivu makubwa katika dinare. Tunataka taratibu za kikatiba zifuatwe ili Dk Baji aondoke madarakani ili kuinusuru dayosisi yetu kimaadili, kiuchumi na kijamii," ilisema taarifa hiyo.

Mapema mwezi huu walei kutoka makanisa 9 kati ya 14 ya Dayosisi ya Tanga, waliandamana kwenda makao makuu ya kanisa hilo mjini Korogwe na kumkabidhi Dk Baji barua ya kutaka ajiuzulu ndani ya siku tano.

Tuma maoni kwa Mhariri
 
Ina maana dayosisi hiyo haina uongozi ila askofu wao? Inakuwaje fedha za wafadhili zinatapanywa na mtu mmoja, kwani wafadhili walimletea yeye kwenye akaunti yake kwa dhumuni gani? Kwa kawaida kuna kamati nyingi na watia sahihi wengi. Utaratibu wa mapato na matumizi huwa bayana, hata kiongozi mkuu anapoitaka hela kutoka fungu lisilokuwa kwa shughuli hiyo hawapewi ila kwa kibali maalum ambacho sio mtaka pesa anatoa kibali hicho bali authority nyingine. Kunani Tanga?

Wa kulaumiwa sio Askofu peke yake, ni genge la watu akiwamo na mtunza pesa, Katibu na kadhalika. Askofu naye ni binadamu na anao uhitaji. Msipomwekea viunzi anaweza kujisahau.
 
Hawa wa Anglican bana si mchezo wengine wale wa kanda ya kusini miaka ya tisini walishawahi ng'oana meno pale Njombe kwenye mkutano wao wa kuchagua askofu hahahahahaahh jamani kweli hata kwenye dini watu wanagombea mkate wa siku
 
Back
Top Bottom