Waume na Wake zetu

Mi naona solution ni kuishi maisha ya kizamani yale ambayo yanasema baba ndo kichwa cha familia hivyo basi kama hajarizika na mama ruksa kuongeza mama wa pili yaani mama mdogo haya ndo yalikuwa maisha ya ndoa za kiukweli haya siku hizi mnayo sema eti nyumba iwa na usawa ni kuiga tamaduni ngeni za kizungu ambapo sisi ni weusi kabisa.

cku hizi magonjwa kila kona mpokezane kijembe kwa namna hiyo?
 
Tatizo kubwa sasa hivi watu wamekuwa opportunist sana, wanangalia maslahi sana kuliko mapenzi ya kweli, Hakuna uvumilivu na watu wanaangalia/wanafuata matamanio zaidi kuliko mapenzi ya kweli.
Upande wa maslahi, wanawake wengi wana dream wapate bwana mwenye pesa zaidi kuliko bwana mwenye mapenzi ya kweli na wana usemi wao kuliko kuishi maisha marefu yenye tabu, heri uishi maisha mafupi yeneye raha.
UVumilivu hakuna kabisa, ikitokea kwenye ndoa kipato kinashuka au matatizo yanatokea basi hiyo ishakuwa sababu, ndoa hii haifai, mara nateseka bure
Matamanio zaidi kwa upande wa wanaume, amekutana na mwanamke kwa sababu ana bboty la kutosha au hips au ana miguu mizuri bila hata kuangalia/ kuchunguza tabia za mwenzi wake baada ya mwezi utasikia mtu anaoa, ukimuuliza mbona ghafla utasikia demu mwenyewe si umemuona katimia idara zote sasa nasubiria nini. Ndoa kama hizi huwa chungu sana huko mbeleni coz hujamjua mwanamke vizuri wewe umeingia kichwa kichwa tuu baadaye tabia halisi za mwanamke zikianza kuonekana basi ugomvi kila siku.
 
kila ndoa ina matatizo yake na hata ufanye vipi hayawezi kwisha 100% , ndoa haiwezi kuwa perfect kwa sababu ndoa inajumuisha watu wawili ambao sio perfect.

matatizo kama kutwangana ngumi, kutukanana matusi ya nguoni na kuitana majina machafu, kununiana na kunyimana unyumba kwa siku nyingi, kutoka nje ya ndoa nk nk nadhani huwa yanakuwa yanahusiana sana na sababu zilizopelekea kuoana pia imani potofu kuhusu ndoa, watu wanaingia kwenye ndoa wakiwa na expectations za ajabu, wengine wanasahau kama kwenye macho yao kuna boriti wanakazana kutoa kibanzi kwenye jicho la mwenzake

pia wakati wa kudate kuna mambo ambayo huwa yanajificha, wengi hawawi wazi kupretend kwingi, wanawake hawanuni nuni ovyo, wanamfanyia kazi za ndani boy friend bila manung'uniko yoyote wala hawatoi mapendekezo ya kuwa na house girl wanaume wanakuwa romantic mpaka basi, outing kika wiki nk nk lakini wakioana mambo yanakuwa kinyume matokeo yake kwenye ndoa mtu anaonekana kama stranger wakati wamedate miaka mingi tuu

ndoa za wazazi wetu na experiences tunazopata utotoni pia huchangia sana ku shape ndoa zetu ziwe nzuri au mbaya
 
Ebu leo hii katafute bibi na bwana harusi watarajiwa waulize KWA NINI UNAOA AU KUOLEWA? nafikiri hakuna jibu utapata zaidi ya utumbo.

We are business oriented in marriage, mkeo anafanya kazi UN au mume ana biashara kubwa basi lazima tukandamizane tunafiti. Hivi kweli hela ni udumisho au suluhisho la ndoa?

Ndiyo hayo madhara yanatukumba, upendo ni ule unaotoka moyoni siyo kwa kuangalia gari, nyumba, bishara, kazi au familia. Tumtangulize Mungu kwa yote, tunahitaji maombi ili tuweze kufikia standard GOOD MARRIAGE.

PRAYERS is an answer.
 
NDOA-Walioko ndani wanatamani kutoka, na walioko nje wanatamani kuingia!
 
Better To be alone and be happy, than Be with somebody and be unhappy allyour life!-Lucky
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=WXpLUp4WmoQ"]http://www.youtube.com/watch?v=WXpLUp4WmoQ[/ame]
 
Hivi huwa tunapata waume na wake zetu ambao kweli ni sehemu ya mbavu zetu na nyama zetu? Nauliza hivi kutokana na mikasa iliyopo kwenye ndoa kama vile kudundana/kupigana; kuvunjika kwa ndoa; kutoka nje ya ndoa; kukosa uvumilivu; kukosa subira; kukosekana kwa heshima ndani ya ndoa n.k.
Nini kifanyike?
Hapa mi naona ndoa ziwe banned tuu,hakuna la ziada,kilichobaki hamna kutokea mademu,mapenzi yawe kama bidhaa nyingine tuu,lihalalishwe soko tuwetunajisevia once tunapopata hitaji,hii itasaidia hata kuepusha vifo vya ghafla,sababu vingi huletwa na mawazo,na kitu chochote kinachohusisha hisia huleta mawazo,mabinti wengi sana hujisikia fahari once wanapoolewa na kusahau kilichowaweka kwenye ndoa,hivyo solution ni kwamba kusiwe na kutongozana,na hii itapunguza gharama zisizo za muhimu,kama kupotezea muda watu kwaajili ya vikao vya ndoa ambayo italeta gharika baada ya miezi michache kufungwa!!"let it be a commodity,and if possible a cheapest one!!!"
 
Ebu leo hii katafute bibi na bwana harusi watarajiwa waulize KWA NINI UNAOA AU KUOLEWA? nafikiri hakuna jibu utapata zaidi ya utumbo.

We are business oriented in marriage, mkeo anafanya kazi UN au mume ana biashara kubwa basi lazima tukandamizane tunafiti. Hivi kweli hela ni udumisho au suluhisho la ndoa?

Ndiyo hayo madhara yanatukumba, upendo ni ule unaotoka moyoni siyo kwa kuangalia gari, nyumba, bishara, kazi au familia. Tumtangulize Mungu kwa yote, tunahitaji maombi ili tuweze kufikia standard GOOD MARRIAGE.

PRAYERS is an answer.
Caroline hapa umeandika ukweli mtupu kwani nina mfano hai kuhusu hili, mimi nina rafiki yangu wa kike aliyesoma Sociology lakini yeye anakwambia piga ua lazima aolewe na mwanaume aliyesoma Accounts. Sasa hapa ndio najiuliza kweli hapa kutakuwepo ndoa kwasababu hata ukimuomba Mungu tayari wewe umeshaweka chaguo lako mbele iwe isiwe. Na kiimani inasemekana kuwa ukilazimisha kitu kitokee kitatokea lakini hakitokuwa chenye baraka na amani.
 
Hapa mi naona ndoa ziwe banned tuu,hakuna la ziada,kilichobaki hamna kutokea mademu,mapenzi yawe kama bidhaa nyingine tuu,lihalalishwe soko tuwetunajisevia once tunapopata hitaji,hii itasaidia hata kuepusha vifo vya ghafla,sababu vingi huletwa na mawazo,na kitu chochote kinachohusisha hisia huleta mawazo,mabinti wengi sana hujisikia fahari once wanapoolewa na kusahau kilichowaweka kwenye ndoa,hivyo solution ni kwamba kusiwe na kutongozana,na hii itapunguza gharama zisizo za muhimu,kama kupotezea muda watu kwaajili ya vikao vya ndoa ambayo italeta gharika baada ya miezi michache kufungwa!!"let it be a commodity,and if possible a cheapest one!!!"
Niliwahi kuongea na Dokta mmoja akaniambia kuwa wanaume wengi wenye wake na wapenzi wanapoteza maisha pale mahusiano yao yanapokuwa sio conducive kuliko wanaume. NA akaongeza kuwa wanaoathirika kisaikolojia zaidi na mateso ya ndoa na mapenzi ni wanaume kuliko wanawake. Hapa alitolea mfano wa FUMANIZI kuwa mwanume anaumia zaidi anapomfumania mke kuliko
 
Matamanio zaidi kwa upande wa wanaume, amekutana na mwanamke kwa sababu ana bboty la kutosha au hips au ana miguu mizuri bila hata kuangalia/ kuchunguza tabia za mwenzi wake baada ya mwezi utasikia mtu anaoa, ukimuuliza mbona ghafla utasikia demu mwenyewe si umemuona katimia idara zote sasa nasubiria nini. Ndoa kama hizi huwa chungu sana huko mbeleni coz hujamjua mwanamke vizuri wewe umeingia kichwa kichwa tuu baadaye tabia halisi za mwanamke zikianza kuonekana basi ugomvi kila siku.
Ni kweli kuna hili tatizo pia la kuchagua mke/mume kutokana na influence ya marafiki na ndugu kwa upande mmoja. Wanawake kwa Wanaume wamekuwa na kasumba ya kutegemea assesment kutoka kwa rafiki zao kama huyu mchumba anafaa kuwa mke au mume. Unajua effect yake ni nini mtazamo wangu mimi au mtu ninayempenda mimi sio unayempenda mimi kwahiyo ni vigumu ku-reccommend kuwa anakufaa au hakufai, the end result ndio hiyo kugombana, kunyimana unyumba, kutukanana na kufukuzana kila kuchapo
 
Ni wewe kweli Fidel unaongea haya na yanatoka moyoni?Na unaposema hakutoshi,kwani toka mwanzo hukumchunguza uone kama atakutosha au laa.Na ukimwambia unataka uongeze mwingine anakukubalia au unatumia mabavu.Na what if akikuambia na wewe humtoshi na yeye anataka aongeze mwingine?Shaurilo mpwa,utamaliza mabucha na nyama ni ileile tatizo ni mapishi tu.
Na hili ndilo alilolifanya Mrs Mtaba, sasa jaribu kuangalia effect yake kwenye ndoa pale unapofanya malipizi. Ni tatizo kubwa kwani hata SAMAHANI NA NIMEKUSAMEHE yakipita lakini siku hizi ni zaidi ya bure nothing is going to change so far
 
nimeipenda hii thread maana inalenga kabisa maisha ya ndoa ya sasa, ingawa mie bado sijaingia huko lakini naona na kuyasikia kuhusu ndoa za sasa mkuu
Hata mimi mtoa mada sijaoa ila umri unanielekeza uko sasa ninatilia shaka sana haya yanayoitwa maisha ya ndoa kwani naona watu wakilia na kuomboleza kwaajili ya hili tendo. Jaribu tu kufanya tathimini hapa hapa JF ni watu wangapi wamelia kwaajili ya ndoa zao na wengine kujuta kwanini walienda umo ndani. Ogopa sana neno NINGELIJUA ni baya sana hasa kwa maisha ya ndoa. Hivi unapomuona dada yangu MJ1 akibubujikwa na chozi unajisikiaje? Unapomuona Striker Geoff anaomboleza kwaajili ya ndoa unapata picha gani? Na wengine wengi sasa we need to learn na kumuomba MUNGU atupe mke/mume kutoka kwake kama ambavyo imeandikwa katika kitabu kitakatifu kwenye kitabu cha Methali.

Naogopa sana kuingia kwenye ndoa halafu nije kuwa na haya matendo kama signature yako inavyosomeka "Kuwa na Mashori wengi si kipimo cha Urijali, kama mwanaume wa kweli, nyumbani wapate Ugali"
 
4.watoto wadogo wameanza nao kuoa na kuolewa mfano ni ngumu sana kwa kijana wa miaka 21 anamwoa msichana wa miaka 18 hii ni hatari sana kwan watu wote hawa hawajamaliza KUONA
HAYA NI MAONI YANGU
hizi ndoa za hivi ziko sana hasa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nenda UDSM, Tumaini, SUA, SAUT, Ruaha, UDOM, n.k
Na wakiachana baada ya muda ukija mtu mwingine ukampata mke au mume wa hivi ambaye alishaishi kinyumba na mwanaume au mwanamke mwingine ndio unawakuta wana frustration na mawazo ya kufa mtu wanakuwa kama scraper kwa kutojiamini kwa sababu mioyo na roho zao zimeshajeruhiwa kwa mapenzi na ndoa za kinyemela.
 
Hivi huwa tunapata waume na wake zetu ambao kweli ni sehemu ya mbavu zetu na nyama zetu? Nauliza hivi kutokana na mikasa iliyopo kwenye ndoa kama vile kudundana/kupigana; kuvunjika kwa ndoa; kutoka nje ya ndoa; kukosa uvumilivu; kukosa subira; kukosekana kwa heshima ndani ya ndoa n.k.
Nini kifanyike?

...bandika ukutani kwako maneno haya, na ikiwezekana uyatamke mara tatu kwa siku;

' usimfanyie mwenzio yale usopenda kufanyiwa!'
 
Problems ni kwamba most people inter into marriage with their natural mind, but it requires a spiritual mind because its spiritual relationship.

So Sipo don't be scared of getting married, just go with spiritual mind I'm sure it will work it na itakuwa paradise ndogo hapa duniani.
 
...bandika ukutani kwako maneno haya, na ikiwezekana uyatamke mara tatu kwa siku;

' usimfanyie mwenzio yale usopenda kufanyiwa!'
Ni maneno yenye hekima kubwa sana nafikiri kama wote wangekuwa wanatekeleza haya basi tungekuwa tunaishi mahali penye usalama wa mwili, akili na roho pia.
 
Sipo ndoa si rahisi kama unavyohisi. Ndoa si suala la kuupata ubavu wako tu bali na nyiwe kuwork hard kuhakikisha huo ubavu unafit kila siku. Kwa sababu unaweza kuupata ubavu wako na nyama yako kisawa sawa but ukizembea kuutunza tu basi huchakaa.

Marriage is a working out through out. It has to be natured
MJ1 sio kuutunza bali kutunzana! Hakuna mmoja kwenye ndoa ambaye ndie ana jukumu la kumtunza mwingie tu. Kila mwanandoa anawajibika kumtunza mwingine kisaikolojia, kimwili, kiakili, kimahitaji n.k
 
mimi kama mwanasheria nimesoma sheria ju ya Ndoa ya Mwaka 1971 kweli , vipigo havijandikwa kwenye sheria mama ya Ndoa ya 1971 na hata katiba inasema mtu aki,osea apelekwe Mahakamani kulingana na kifungu kikubwa cha 13 cha Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania kama ilivyobadirishwa mwaka 2005 inasema haki sawa ya Kisheria.
Vijinaume vinavyodunda wake zao vinajifanya vyenyewe ndio mahakama na ndio polisi na ndio serikari( Nguzo tatu za Taifa ni Mahakama, Bunge na Excutives( President and the excutives)
Kwa hiyo mwanume huyo huyo anatunga sheria anaitafusiri( Mahakama) na anainforce
tembelea blogy yangu ya www.mwanasheriajames.blogspot.com upate mawazo mengi
 
Back
Top Bottom