Waume na Wake zetu

Sipo

JF-Expert Member
Jul 25, 2008
2,139
91
Hivi huwa tunapata waume na wake zetu ambao kweli ni sehemu ya mbavu zetu na nyama zetu? Nauliza hivi kutokana na mikasa iliyopo kwenye ndoa kama vile kudundana/kupigana; kuvunjika kwa ndoa; kutoka nje ya ndoa; kukosa uvumilivu; kukosa subira; kukosekana kwa heshima ndani ya ndoa n.k.
Nini kifanyike?
 
maadili yamemomonyoka
watu tumekosa maadili ya ndoa
kwanza utasikia kuna baadhi ya watu wanasema naoa/naolewa kuondoa mkosi hata nikiachika /nikiachwa mradi ndoa nimeionja
Je ukiingia kwenye ndoa na mawazo hayo hiyo ndoa mtashindwa kudundana /kutukanana /na kufukuzana kwa mateke na magumi
Thamani ya ndoa imepotea
 
FL1 hapa kwenye maadili ni kweli hasa kwa sisi vijana, narejea zile niziitazo ndoa za kinyemela!!
Pia kama kuna hawa wanaolewa ili kuondoa mkosi, ni tatizo kwa kuwa hapana shaka wanakuwa wamedondokea popote pale walipodondokea ili kuondoa nuksi barkishi. Tunahitaji kuangalia tulipotoka ili kuwa na ndoa imara
 
Ndoa ina mambo mengi sana jamani! Mungu atusaidie........
Samahni Kibweka hivi haya mambo mengi ndiyo yanasababisha haya masaibu yote au ni maadili kumomonyoka kama asemavyo FL1? Na in brief tushirikishane haya mambo mengi ili iwe msaada kwetu sote
 
Sipo ndoa si rahisi kama unavyohisi. Ndoa si suala la kuupata ubavu wako tu bali na nyiwe kuwork hard kuhakikisha huo ubavu unafit kila siku. Kwa sababu unaweza kuupata ubavu wako na nyama yako kisawa sawa but ukizembea kuutunza tu basi huchakaa.

Marriage is a working out through out. It has to be natured
 
Mi naona solution ni kuishi maisha ya kizamani yale ambayo yanasema baba ndo kichwa cha familia hivyo basi kama hajarizika na mama ruksa kuongeza mama wa pili yaani mama mdogo haya ndo yalikuwa maisha ya ndoa za kiukweli haya siku hizi mnayo sema eti nyumba iwa na usawa ni kuiga tamaduni ngeni za kizungu ambapo sisi ni weusi kabisa.
 
zamani watu wakitaka kuingia katika ndoa, huwekwa kitako wakafunzwa kuhusu ndoa, wakapewa maadili yanayotakiwa kufanywa huko kwenye ndoa, wakafunzwa namna kuishi na mume/mke, wakaonywa kuhusu vishawishi, marafiki nk....

leo hii mtu anamuokota mtu tu mtaani, hajamchunguza, hajasikiliza wazazi, wanaoana kisa anajua kutoa chakula cha usiku vizuri tu!lazima tusifike kwa ndoa za namna hivi
 
Mi naona solution ni kuishi maisha ya kizamani yale ambayo yanasema baba ndo kichwa cha familia hivyo basi kama hajarizika na mama ruksa kuongeza mama wa pili yaani mama mdogo haya ndo yalikuwa maisha ya ndoa za kiukweli haya siku hizi mnayo sema eti nyumba iwa na usawa ni kuiga tamaduni ngeni za kizungu ambapo sisi ni weusi kabisa.

ooh Fidel80 mmh una mawazo gani tena hayo ya kuongeza small haouse wakati wewe ni kijana wa kileo kabisa
 
Kwa ulimwengu wa sasa wachache wanapata ambao ni sehemu ya nyama zao na ubavu wao.Lakini kupata ubavu wako wa ukweli sio guarantee kuwa hamtapata matatizo au hamtakwaruzana.Ukipata wa kufit ubavu wako ina maana umempata atakayekuwa na uwezo wa kuyavumilia madhaifu yako yote bila malalamiko.
Lakini siku hizi watu hawasubiri apate wa ubavu wake kwa sababu tunaangalia sana material things kama kazi nzuri,pesa,sura nzuri,elimu n.k.vilevile watu wanaoana kwa sababu ya pressure tu kma akiona muda umeenda na wenzie wameoa au kuolewa na yeye anaingia kwenye ndoa na yeyote atakayetokea.Na muda nao unachangia,watu wanaweza kukutana kwenye daladala na ukashangaa baada ya mwezi washatangaza ndoa,sasa hawa kweli watakuwa wameyapima maji?
Na hapa kwenye ndoa watu wengi huwa wanajuta kwa sababu ya makosa haya na wanaishi misery life the rest of their lives.
Uchaguzi wa mwenzi wa ndoa unahitaji umakini na msaada wa Mungu.
 
ooh Fidel80 mmh una mawazo gani tena hayo ya kuongeza small haouse wakati wewe ni kijana wa kileo kabisa

Haya mawazo mama niendelevu angalia baba zetu walivyo ishi enzi hizo angalia nyie vijana wa kileo mnavyo ishi yaani bla bla kibao kuongeza wife kwani dhambi si makubaliano ya nyie 2 unamwambia mke wa kwanza nataka niongeze mwingine wewe naona hunitoshi.
 
Ni wewe kweli Fidel unaongea haya na yanatoka moyoni?Na unaposema hakutoshi,kwani toka mwanzo hukumchunguza uone kama atakutosha au laa.Na ukimwambia unataka uongeze mwingine anakukubalia au unatumia mabavu.Na what if akikuambia na wewe humtoshi na yeye anataka aongeze mwingine?Shaurilo mpwa,utamaliza mabucha na nyama ni ileile tatizo ni mapishi tu.
 
Haya mawazo mama niendelevu angalia baba zetu walivyo ishi enzi hizo angalia nyie vijana wa kileo mnavyo ishi yaani bla bla kibao kuongeza wife kwani dhambi si makubaliano ya nyie 2 unamwambia mke wa kwanza nataka niongeze mwingine wewe naona hunitoshi.

hapa unatufurahisha tu dada na kaka zako teh teh teh
 
hapa unatufurahisha tu dada na kaka zako teh teh teh

Hehehe ukweli najua iwa unauma lakini ndo hivyo kama Mr. wako ana mega ovyo ovyo si ukae nae chini mjadili swala zima yawezekana wewe humtoshelezi ili kumpa nafasi mwambie achukue mke wa pili ili awe huru kumega kwa nyie wawili na si mara hapa kesho Mburahati kesho kutwa Mbagala
 
nimeipenda hii thread maana inalenga kabisa maisha ya ndoa ya sasa, ingawa mie bado sijaingia huko lakini naona na kuyasikia kuhusu ndoa za sasa mkuu
 
1.suala la ndoa wanaolijua vizuri ni walioko kwenye ndoa
2.ndoa ndoana mana yake ukiingia kwenye ndoa ni sawa na samaki kwenye ndoana huna ujanja wa kufanya lolote nje ya ndoa.
3.ndoa nyingi siku hizi huwa na mapungufu mengi sana mfano kutoaminiana baina ya wanandoa na n.k
4.watoto wadogo wameanza nao kuoa na kuolewa mfano ni ngumu sana kwa kijana wa miaka 21 anamwoa msichana wa miaka 18 hii ni hatari sana kwan watu wote hawa hawajamaliza KUONA
HAYA NI MAONI YANGU
 
Back
Top Bottom