Wauguzi nao watangaze mgomo?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Binafsi nilitarajia kuwa serikali ingeonesha uwezo wa kuwa mchangamfu kushughulikia madai ya madaktari bila kulazimishwa zaidi na migomo. Bahati mbaya sana serikali yetu inaonekana kutoamini kuwa katika hili imeshindwa (it has lost). Bado wanaamini kwa vile wao ni "serikali" basi wanaweza kufanya lolote. Tunapoenda kuelekea siku saba za mgomo wa madaktari uwezekano mkubwa sasa wa kushinikiza serikali utajitokeza endapo wauguzi nao wataamua kutangaza mgomo.

Kwa kweli, ikifika hapo manake ni kuwa tuna matatizo makubwa zaidi ya kiuongozi. Huu mgomo wala usingefika hapa na kama tungekuwa na viongozi makini na wenye busara wala usingeanza kabisa. Lakini umefika hapa kwa sababu kuna watu ambao hawaamini kabisa kuwa wanatakiwakuongoza siyo kutawala.

Endapo wauguzi nao watatangaza mgomo serikali itajikuta inalazimishwa kuconcede mambo makubwa zaidi wakati huo kuliko kama ingekubali kabla ya wauguzi kugoma. Jamani, wauguzi wakigoma manake ni kuwa hali imewazidi na maji yamefika shingoni. Wao na mabingwa au wafanyakazi wengine wa afya wakiamua kusimama na madaktari kutakuwa hakuna jinsi tena isipokuwa kujiuzulu mara moja hadi kwa Waziri Mkuu na baraza la Mawaziri kuvunjika.

We are at the precipice of a disaster! We change or perish!

Naomba wauguzi wasitangaze mgomo mara moja kusikiliza serikali itafanya nini hiyo kesho; endapo serikali itatangaza madaktari wote waliogoma wamejifukuzisha kazi then wauguzi wanaweza kutangaza kugoma in solidarity. Lakini kama Rais atakubali kujiuzulu kwa Hadji, Katibu Mkuu na Mganga Mkuu mara moja basi safari ya kumaliza mgogoro huu itakuwa imeanza na tutarajie kabla ya mwisho wa wiki madaktari wote kurudi kazini baada ya baadhi ya madai kukubaliwa na kutiwa sahihi kuwa yamekubaliwa kati ya madaktari na serikali. Uamuzi kwa kweli hadi hivi sasa uko kwa serikali.
 
Nimeanza ku doubt 'umakini' wako

Mwanakijiji...........

ulitarajia nini? kwa serikali ipi?

wewe unachochea migomo ukiwa na imani serikali hii itasikia? kweli?

at what price?
 
Mm umetafutwa sana kule kwenye thread ya cck na hukuonekana huko. Sasa naona ff amekufuata na huku. Bado matola, pasco, mchambuzi na wengineo watakufuata huku ili ueleze msimamo wako kuhusu cck, kwani unatuchanganya sasa.
 
tunangoja tuone sera za cck kuhusu migomo, jee ni hizi za "kukaanga mbuyu na kuwacha wenye meno watafune" au itaishia njiani? Maana ccj ilijaribu ikafa "untimely premature".

mpe mpeeee vidonge vyake, akikimbia akikijificha ujumbe tayari delivered!
 
Tunangoja tuone sera za CCK kuhusu migomo, jee ni hizi za "kukaanga mbuyu na kuwacha wenye meno watafune" au itaishia njiani? maana CCJ ilijaribu ikafa "untimely premature".

CCK is another hoax:eyebrows:
 
Wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wametoa msimamo mpya kwamba hawako tayari kufanya kazi na madaktari kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ). Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Tawi la MHN, Paul Magesa alisema madaktari hao hawana uwezo wa kufanya kazi katika hospitali hiyo ya taifa ambayo ndiyo kubwa nchini kwa kuwa inahudumia wagonjwa walioshindikana katika hospitali wanazotoka.

"Ifahamike kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni ya rufaa na inapotokea wagonjwa walioshindikana katika hospitali nyingine inakuwaje leo wakaletwa madaktari kutoka katika hospitali hizo kuja kutibu?" alihoji Magesa na kuongeza: "Sisi tulishafanya kazi nao mwaka 2005 na tunawafahamu wengi hawajui mambo mengi, watakuja kutuuliza na kutuongezea kazi za kufanya... tunaomba katika hili Serikali isikwepe tatizo, ilishughulikie kwa maslahi ya taifa," alisema.

Sasa nao wauguzi wakigoma kufanya kazi na wanajeshi, hakuna pia wauguzi huko jeshini ambao Pinda anaweza akawaita chap chap ku-cover?
 
Wauguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wametoa msimamo mpya kwamba hawako tayari kufanya kazi na madaktari kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ). Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Tawi la MHN, Paul Magesa alisema madaktari hao hawana uwezo wa kufanya kazi katika hospitali hiyo ya taifa ambayo ndiyo kubwa nchini kwa kuwa inahudumia wagonjwa walioshindikana katika hospitali wanazotoka. “Ifahamike kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni ya rufaa na inapotokea wagonjwa walioshindikana katika hospitali nyingine inakuwaje leo wakaletwa madaktari kutoka katika hospitali hizo kuja kutibu?” alihoji Magesa na kuongeza: “Sisi tulishafanya kazi nao mwaka 2005 na tunawafahamu wengi hawajui mambo mengi, watakuja kutuuliza na kutuongezea kazi za kufanya... tunaomba katika hili Serikali isikwepe tatizo, ilishughulikie kwa maslahi ya taifa,” alisema. Sasa nao wauguzi wakigoma kufanya kazi na wanajeshi, hakuna pia wauguzi huko jeshini ambao Pinda anaweza akawaita chap chap ku-cover?

Magesa deserves my congrats for a very strong comment.
 
Back
Top Bottom