Watumwa majumbani wakombolewe

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Mwaka huu 2009 tunakumbuka miaka zaidi ya 200 ya kusimamishwa kwa biashara ya utumwa iliyohusisha meli za kiingereza na nchi nyinginezo. Ingawa miaka zaidi ya 200 imepita, je utumwa huo twauendeleza wenyewe?
Utumwa mfumo wa unyonyaji wa kutumia nguvu za watu bila malipo wala hiyari yao wenyewe au kumiliki mtu/watu wengine kama bidhaa. Mara nyingi tunapozungumzia utumwa tunafikiria kuhusu biashara ya pembe tatu tuliyofundishwa na waalimu wetu wa siasa au historia shuleni. Tulifundishwa kwamba watumwa walikamatwa kutoka vijijini mwao na kuuzwa kwa wafanya biashara ambao waliwapiga mnada gulioni Bagamoyo, Mombasa na Unguja. Pili tunaelezwa kuwa watumwa walisafirishwa kwenda visiwa vya Shelisheli hadi Karibea na Amerika kwenye mashamba ya miwa na kadhalika. Baada ya hapo waalimu wetu walitueleza jinsi watumwa walivyoteseka huko mashambani na wanyapara wao walivyowapiga, kuwafanyisha kazi na kuwavuna. Malipo yao yalikuwa sembe na maharage kidogo ili kesho tena waje kulima.

Utumwa Wa Waafrika Kwa Waafrika
Baada ya hapo somo linaruka tunaambiwa kuwa biashara hiyo haramu ya utumwa ilisimamishwa kutokana na juhudi za mwingereza William Wilberforce.
Ukifuatilia wanahistoria weusi watakueleza jinsi jamii za kiafrika zilivyoishi vema ki-ujima wakipeana mali na kufanya kazi pamoja kwa ujamaa na undugu. Lakini ukitafiti ukweli wa mambo, utakuta jambo ambalo hatukufundishwa kwa kina ni dhana ya utumwa na jinsi utumwa ulivyobobea katika mila na desturi zetu za kiafrika. Kabla hata mzungu wa kwanza hajanunua mtumwa mmoja, tayari kulikuwa na biashara ya utumwa Afrika. Mababu zetu waliuziana watumwa wao kwa wao kama vifanyia kazi. Walioathirika zaidi na biashara hiyo ni wale ambao hawakuzaliwa katika ukoo wa watemi (au ma-Mangi), waliokuwa na na ufukara, mateka wa vita, ardhi ndogo, walioonekana kama wakorofi na waliokuwa wana ubishi au waliomuudhi mtawala wa enzi hizo basi walikiona cha mtema kuni.

Wanahistoria wengine wanasema kwamba kuna watumwa Afrika waliojiuza wenyewe kwa mabwana zao kwa sababu hawakuweza kulipa madeni makubwa waliyokuwa wanadaiwa mara nyngine baba alidaiwa deni kubwa ambapo ilibidi yeye na mama na watoto wotw wauzwe ili kulipa madeni hayo. Wengine walijiuza wenyewe maana walidhania kufanya kazi kwa Mangi watakula nyama ya ngombe na mbege kwa sana lakini wakijilimia wenyewe ndizi za kuchemsha.

Waarabu walipokuja barani Afrika walipata mazingira mazuri ya kuendeleza biashara hiyo ambayo ilikuwa inaongezeka umaarufu na kuwavutia washika dau wa enzi hizo. Waarabu waliongeza nguvu ya soko la utumwa na mababu zetu waliwauzia watumwa wengi wanaume kwa wanawake. Wanaume walienda kufanya kazi mbalimbali kama kulima, kubeba mizigo au kupigana vita kwa mabwana zao. Wanawake watumwa walienda kufanya kazi za nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwatimizia mabwana zao haja binafsi.

Badala ya kwenda mbali sana huko na biashara ya pembe tatu, mimi nadhani tujiangalie wenyewe na jamii yetu jinsi tunavyoendeleza utumwa leo ingawa biashara ya utumwa (inasemekana) iliishasimamishwa.
Yule Dada-usafi!

Jamii zetu za wafanya kazi Darisalamu ni kawaida kuwa na mfanya kazi wa nyumbani ambaye mara nyingi huitwa dada, mfanyakazi, housigeli au dada-usafi. Suala la kuwa na msaidizi wa kazi za ndani ni la kawaida. Shida ninayoona mimi ni pale watu wazima wenye nguvu na afya, wanafanya kazi benki au hospitali au dukani wanarudi nyumbani halafu wanakaa kwenye kiti wakisubiri maji yaletwe ya kunawa mikono, chakula kiletwe, wale, baada ya hapo maji ya kunywa yaletwe, soda ikanunuliwe dukani kwa mchaga, maji ya kuoga yawekwe. Baada ya kuoga waende kulala kwenye kitanda kilichotandikwa na mfanya kazi. Asubuhi wanaamka wanakuta staftahi imeandaliwa, viatu vimepigwa rangi (au kama wana mchuma umeoshwa tayari), nguo zimefuliwa na kupigwa pasi, kazi yao kuvaa na kuondoka tena.

Mfanya kazi huyo hana jumamosi au jumapili, tena kama ana ndugu karibu anaonywa asiwatembelee kwa madai kwamba ataharibika. Watashauri kuhusu haki zake na hivyo "kumpa kichwa." Au watamshawishi atafute bwana mpya. Je mwisho wa mwezi mfanyakazi huyu analipwa bei gani? Shilingi elfu kumi hadi elfu ishirini. Ukiwauliza wamiliki mtumwa huyo kwamba kwa nini wanamlipa hela ndogo hivyo watasema "angekuwa kwao hata elfu tano kwa mwezi asingepata."

Wakati tunakumbuka kusimamishwa biashara ya utumwa, ni vema kuzingatia kwamba ingawa biashara ilisitishwa, bado utumwa unaendelea kwa mitindo mingine na aina anuai. Kwani jamii ya wamiliki watumwa ni vilema hawawezi kunawa mikono wenyewe? Hawawezi kupika wenyewe? Hawawezi kufua nguo wenyewe? Kwa nini wasiwatumia wasaidizi wa kazi kama mara tatu kwa juma waje kufua au kufanya kazi fulani na walipwe kwa kazi hizo? Au ni rahisi wakikaa ndani ya nyumba na kulipwa elfu kumi mwisho wa mwezi wakati mwenye nyumba analipwa laki tano kwa mwezi? Utumwa wa jinsi hii hauwezi kusitishwa na serikali au Wilbeforce ila itabidi jamii iamue kuacha uvivu na kujifanyia kazi wenyewe, na ikihitajika usaidizi basi wasaidizi walipwe kwa haki kama binadamu si kama watumwa. Biashara hii ya utumwa tusipoiacha, itavuka mipaka tena kama ilivyotokea hapo enzi, kwani wahenga wanasema historia inajirudia. Tujikomboe!
 
Umesahau pi akuwa hawa wafanyakazi wa ndani hubughudhiwa na kudhalilishwa na wanaume wa humo nyumbani ( baba, watoto wa kiume nk)nadhani hata hapa hapa JF kuna memba maarufu aliwahi kusema amempa mimba hausigeli..... sasa sijui unataka tuzungumzie lipi kati ya haya mengi.
Kwa uchache napenda kuchangia afuatayo:
1.MshaharaWafanyakazi wa majumbani ni kweli wananyonywa sana lakini ni tatizo la kimfumo zaidi.Mfumo mzima wa malipo Tanzania ni wa kinyonyaji ( sekta ya umma, binafsi ).Chukulia mfanyakazi wa serikali mwenye mshahara wa sh 200,000 kwa mwezi, unategemea amudu vipi kulipa kima cha chini? Hata Sheria ya Ajira haimwingizi mfanyakazi wa ndani katika stahili ya minimum wage.Unadhani ni kwanini?Kwa wale wenye vipato vizuri, mara nyingi wengi huwapatia wasaidizi wa ndani mshahara wa kuridhisha hata kama hautoshelezi.

2. Muda wa kazi
Kweli wafanyakazi wengi huonekana kufanya kazi bila muda maalum wa kuanza au kumaliza kazina watu wengi hudai kuwa wanakuwa overworked.Mimi nadhani hii ishu inategemea na mazingira ya kazi.Kuna wafanyakazi wengine hulala kutwa wakati waajiri wako kazini na kujifanYa bize wakiona saa za kurudi zimekaribia.Waajiri nao wanalijua hili, so its only fair waendelee na kazi.Ila kwa wale ambao wanajituma, ni haki wapumzike muda muafaka.Watu wengi ikiwa ni pamoja na mimi mwenyewe tuna wafanyakazi wanaoingia asubuhi na kuondoka jioni kurudi majumbani na hata weekend wako off.Wengine wana part time help.Kwa hiyo mambo yanabadilika polepole.
3. Waajiri kutokusaidia kazi
Inategemea... siungi mkono hili bali nadhani ni jambo la tabia na utu wa mtu.Na huwezi kumbadili mtu tabia.
Kwa sasa niishie hapa.
 
Back
Top Bottom