Watumishi wa Serikali ndo kusema wako juu ya sheria???

Konzogwe

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
434
155
Wakuu jana nikiwa safarini kuja Dar nilishangazwa na ubabe wa watumishi wa umma!
Pale Mikumi Morogoro kuna bonge la Hotel ya Veta iliyo umbali kama mt10 toka barabara kuu ya Tanzam.Tuliingia pale ili kula na kunywa kisha tuendelee na safari,ilikuwa yapata saa 3 usiku.Wakati tunatoka,tukiwa ndani ya landcruiser mkonga nyeupe yenye namba zinazoanza na DFP---.Dereva wetu aliingia barabara kuu kwa spidi kubwa sana na nusura agongane na gari dogo Toyota cardina.
Kilichofuata pale cardina lilienda mbele na kufunga barabara kisha akashuka jamaa mmoja na kuanza kumtukana dereva wetu matusi ya kila aina,******,unafirwa na zaidi ya hayo!
Kwa mujibu wa sheria za barabara,dereva wetu kweli alikuwa na makosa na kwa kujua hilo alijitahidi kuomba msamaha kwa kurudiarudia lakini yule jamaa ndo kwanza anatukana.
Mara dereva wetu akawasha gari na kuendesha kwa speed akalipita lile cardina nae akapaki na kuziba njia na akashuka akitamba:"HILI GARI NI LA SERIKALI! UTASHINDANA NA SERIKALI! HAYA HEBU FANYA UNALOTAKA KUFANYA" dereva wetu aliyasema hayo huku akimsogelea kutaka kumpiga.
Huyu jamaa nae kwa kuona hivyo,akaanza "USINIBABAISHE! HATA MIE NI WA SERIKALI,MIMI NI POLISI! NAITWA AFANDE JOEL WA KITUO CHA MIKUMI KAMA HUAMINI ULIZA HAWA WATU WOTE WANANIJUA!(washuhudiaji).NITAKUWEKA NDANI SASA HIVI ****** MKUBWA! KWANZA UNAENDESHA UMELEWA! TANGULIA KITUONI!!"
Basi ikawa vurugu tupu kila mmoja akitamba yeye ni wa SERIKALI.Tuliokuwemo kwenye cruiser tukashuka kuamulia hata walokuwemo kwenye cardina wakashuka kuamulia.
Mimi najiuliza,kumbe ukiajiriwa na Serikali hata ukitenda kosa serikali ni ngao yako! Maana kila mmoja serikali,serikali.Nikasema kumbe ndo maana yule mbunge wa Morogoro alimchapa makofi yule mkata maji kisa yeye mkubwa serikalini! Tena nikamkumbuka marehemu Ditto aliua kwa shida za barabarani kisa yeye ni mkubwa serikalini!!
Inashangaza.Kuanzia leo natafuta ajira serikalini ila mimi sitafanya kama wanavyofanya hawa.Kwani niliwaona wote wamekosa uadilifu hasa yule AFANDE JOEL WA MIKUMI POLICE STATION.
 
Kwa mujibu wa Sera ya Ajira na Menejimenti katika Utumishi wa Umma ya mwaka 1999, na kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 pamoja na Marekebisho yake ya mwaka 2008, ikisomwa pamoja na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma Toleo la Pili za mwaka 1994 pamoja na Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, pamoja na Kanuni za Maadili katika Utumishi wa Umma kama zilivyotolewa na Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma zote zinasisitiza yafuatayo:

1. Mtumishi wa Umma anapaswa kuzingatia Miiko ya Utumishi wa Umma ikiwa ni pamoja na kutofanya kitendo au vitendo vinavyokwenda Kinyume na Utumishi Umma,
2. Mtumishi wa Umma hatakiwa kufanya kitendo au vitendo vitakavyopelekea Utumishi wa Umma kudharaulika
3. Mtumishi wa Umma anatakiwa kujiweka katika Maisha au utaratibu wa maisha ambao hautampelekea kushindwa kuwa na Utumishi uliotukuka,
4. nk.

Kwa kuzingatia Misingi hiyo ya Rejea za Sera, Sheria na Kanuni zinazolinda Utumishi wa Umma. Watumishi hao wote walifanya makosa. Na kwa mujibu wa Sheria hiyo na Kanuni hizo makosa yao adhabu yake ni kufukuzwa kazi.

Nikushauri ndugu yangu katoe taarifa kwa Mwajiri wa Dereva wenu ili aweze kuchukuliwa Sheria.
Na kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni zake za Mwaka 2007 Mwenye Mamlaka ya kumchukulia hatua za kinidhamu Dereva huyo ni Mkuu wa wake wa Idara. Nikusihi nenda katoe taarifa hizo kwa Mkuu wake wa Idara ili aweze kuchukuliwa hatua stahili.
 
Back
Top Bottom