Watumishi wa mizani wakamatwa kwa rushwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
TAkukuru%2813%29.jpg

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)


p { margin-bottom: 0.08in; }
Watu wanne wakiwemo maofisa wawili wa ofisi ya mizani mkoa wa Pwani, wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Pwani, baada ya kudaiwa kupokea rushwa na kuyaruhusu malori usiku yakiwa yamesheheni mzigo wa magogo.
Akizungumza na gazeti hili, shuhuda wa tukio hilo, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wanaotumia barabara hiyo, alisema kuwa sakata hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana kati ya saa 8:00 na 9:00 kwenye mizani hiyo iliyopo Vikindu mkoa wa Pwani.
Akisimulia zaidi, alisema kuwa, majira hayo, magari hayo yalifika katika kituo hicho cha ukaguzi yakitokea maeneo ya pori la Rufiji ambao inadaiwa kuwa ndiko magogo hayo yalipotolewa. Alisema ukaguzi ulifanyika na magari hayo yaliruhusiwa kuondoka.
Alisema mtuhumiwa huyo alipata kipigo na kuchukuliwa na mwenzake.
Aidha, shuhuda huyo alieleza kuwa, inaonekana kuwa, mzigo huo wa magogo haukuwa na kibali kutoka Ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii iliyopo maeneo hayo. Alisema hadi jana magari yote manne yalikuwa yameegeshwa nje ya ofisi hiyo ya mizani huku yakiwa yamefungwa na maturubai.
Shuhuda huyo aliliambia gazeti hili kuwa, wakati magari hayo yalipofika kwenye kituo hicho mara ya kwanza, alikuwa hapo na gari nyingine ambayo dereva wake aliombwa rushwa ya Sh. 250,000 na mtuhumiwa Kalenga.
Alisema baada ya gari la kufika hapo ilipasuka tairi moja, hivyo wakati wa ukaguzi mtuhumiwa Kalenga alimwambia dereva wake ili amruhusu atoe kiwango hicho cha fedha.
“Mtuhumiwa huyo alikubali na alipima gari kisha alimbadilikia dereva na kumwambia achague moja, kuandikiwa faini ya Sh. 500,000, au atoe fedha hiyo ili yaishe,” alisema.
Alisema dereva wake alikubali kulipa faini hiyo na waliipeleka jana.
Shududa huyo alisema licha ya kuwepo kwa tatizo hilo la rushwa, pia baadhi ya maofisa wa hapo wamekuwa wakiwalipisha faini kwa fedha za kimarekani badala ya shilingi na kusababisha usumbufu kwa kwao.
Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Pwani, Gabriel Mwikola, akijibu lalamiko hilo la ulipaji wa dola alisema kuwa, karatasi za faini zote hapa nchini zimeandikwa kwa mfumo dola lakini utozaji kufanyika kwa fedha ya kitanzania.
Aidha, Mwikola alipoulizwa kuhusiana na sakata la ukamatwaji wa malori hayo, alisema ofisi yake imepata taraifa hizo na tayari imeshatuma mainjinia kwenda eneo la tukio kufanya uchunguzi.
Alisema kuwa, maofisa wake kwa kushirikiana na wa Takukuru Mkoa wa Pwani walifika eneo hilo juzi kwa ajili ya kupima magogo hayo.
"Wakati wa kupima watuhumiwa waliletwa ili kushuhudia tukio hilo, taarifa iliyoletwa ofisi kwangu ambayo kwa sasa inashughulikiwa , inaonyesha kuwepo kwa ongezeko kubwa la magogo kwenye magari hayo," alisema.
Kwa upande wa Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Pwani, Laurence Ndalichako, akizungumza na gazeti hili alisema kuwa, hadi sasa jumla ya watu wanne wanawashikilia kwa uchunguzi wa tukio hilo.
Alisema watu wawili ni kutoka Tanroads ambao siku hiyo walikuwa kwenye mizani hiyo na wawili waliokuwa wamebeba mzigo huo wa magogo.
Ndalichako alisema kutokana na mzigo waliokutwa nao watu hao inawezekana kunaudanganyifu wa kibali walichokuwa nacho watu hao .
"Kila gari baada ya kupimwa lilikuwa limezidisha mzigo kwa kiwango cha juu zaidi, kwa mfano gari moja lilikutwa na mzigo mita za ujazo 50 badala ya 10, lingine lilipaswa kuwa na ujazo wa 20 lakini mzigo ulifika hadi 50," alisema.
Alisema wanaamini faini waliyowatoza bado ni ndogo na inawezekana upande wa maliasili nao wanaweza kuwatoza zaidi.
Ndalichako alisema hadi juzi jioni wahusika wa magogo hayo walikuwa wametozwa kiasi cha Sh. milioni 19 kama faini.



CHANZO: NIPASHE
 
Rushwa iliyonenepa imelala kwenye hizi mizani!
Wafanyakazi wa eneo hili ni miungu watu pindi wakikushika!...na wana mbinu nyingi sana za kufanikisha azma yao ya kuiibia serikali!
Serikali Toeni mfano kupitia wafisadi hao!
 
Back
Top Bottom