Watuma habari wanatafutwa pia!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,988
Kasi ya kukitoa kijarida nayo imeongezeka baada wa watu wengi kujitokeza kuwa tayari kukisambaza na kwa kiwango kikubwa kunifanya niamini kuwa tunaweza kama tukitaka.

Sasa tunataka watuma habari ambazo hazija/hazitachapishwa kwenye gazeti lolote jingine.

Habari hizo zifuate kanuni za kiuandishi ikiwemo maswali muhimu ya uandishi:

Nini?
Wapi?
Nani?
Lini?
kwanini?
Kwa jinsi gani?

Kwenye habari ambazo zinalenga kuonesha mtazamo wa upande mmoja au msimamo juhudi ziwe zimefanywa kupata majibu ya upande wa pili.

Habari zozote zinaweza kutumwa kwa mhariri(at)klhnews.com na zisizidi 1/2 ya Ukurasa. Habari zote zinakuwa ni mali ya klhnews na zitanukuliwa hivyo. Habari zinaweza kuwa kwa njia ya picha pia. Habari zitakazopewa kipaumbele ni zile zenye kufanya watu wafikiri, waamue na kutenda. Lakini zaidi ya yote habari za nini kinafanyika au kinafanywa nazo zitapewa kipaumbele. Habari za udaku, za lugha ya kejeli, na zisizolenga kumfanya Mtanzania aone, afikiri, aamue na kutenda zitakuwa kwenye kipaumbele cha chini.

Haihitaji kuwa mwandishi alimradi mtu ana uwezo wa kuandika kwa lugha fasaha ya Kiswahili. Kwa wale watakaopenda kuwa maripota wetu kutoka mikoani utapatiwa karabrasha la kukupa mwelekezo tu wa kufanya kile ambacho kinajulikana kama citizen journalism.
 
Back
Top Bottom