Watuhumiwa 69 wafikishwa mahakamani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,293
33,078
Wakazi 69 wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wamefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Songea kujibu mashitaka ya kushiriki katika mkusanyiko usio wa halali na kuharibu mlango mmoja wa jingo la CCM la

Manispaa hiyo wenye samani wa Shilingi 150,000 na kuchana bendela moja ya CCM yenye samani ya Sh. 20,000.
Katika Mahakama hiyo ambayo ilifurika watu waliofika kusikiliza kesi hiyo upande wa mashitaka ulioongozwa na

Mwanasheria wa Serikali kanda ya Songea, Edison Mwavanda, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Ruvuma, Elizabeth Missana, ulidai kuwa washitakiwa wote 69 bila halali Februari 22, mwaka huu walikusanyika bila kuwa na kibali kwa nia ya kuvunja amani.

Washitakiwa wote 69 baada ya kusomewa mashitaka yao yote mawili na kesi yao ilihairishwa hadi Machi 8 Mwaka huu itakapotajwa. Washitakiwa 37 wako inje kwa dhamana wakati 32 wamerudishwa maabusu baada ya kukosa wadhamini.

KUFUATIA vurugu zilizotokea mjini Songea Jumatano wiki hii, na kusababisha vifo vya watu wawili, Jeshi la Polisi makao makuu limetuma timu ya maofisa wanane kusaidiana na kamati iliyoundwa na mkoa wa Ruvuma kuchunguza tukio hilo.

Watu hao waliuawa wakati wakiandamana kwenda katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma kulalamikia mfululizo wa matukio ya mauaji ya wakazi wa mji wa Songea na watu wasiofahamika.

Polisi walitumia risasi za moto na kuwaua watu hao, kuwajeruhi wengine zaidi ya 40 na kuwakamata wengine zaidi ya 50.
Kutokana na hali hiyo, Uongozi wa mkoa uliunda kamati hiyo ambayo itafanya kazi kwa siku saba na kutoa taarifa.

Aidha, Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linawashikilia askari polisi wanne kwa matumizi mabaya ya silaha na kusababisha mauaji hayo.

Kamishina wa Jeshi la Polisi nchini, Paul Chagonja, alisema kuwa moja ya hatua ambazo zimeshachukuliwa na Jeshi la Polisi ni pamoja na kukutana na viongozi mbali mbali kuanzia ngazi ya mtaa kwa ajli ya kujipaga kukabiliana na vitendo vyote vya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuendeleza utaratibu usio na kikomo wa ulinzi shirikishi.

Aidha, tayari utaratibu huo umeshaanza kufanyiwa kazi kwa Kamishina Chagonja kukutana na waendesha pikipiki zinazofanya biashara ya kubeba abiria ambao ndiyo waathirika zaidi wa matukio hayo ya mauaji.

Alisema kuwa baadhi yao wamekiri kuwa sio waaminifu na wanashirikiana na wahalifu kufanya vitendo hivyo na wako tayari kuwadhibiti. Utaratibu huo uliwahi kuwepo siku za nyuma na kusaidia kutatua tatizo pamoja a kuimarisha umoja wao.

Kamishina Chagonja, ambaye pia ni Mkuu wa mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi, aliwataka wananchi kwa ujumla ashiriki katika kutatua tatizo lililopo na siyo kutoa lawama wala kupandwa na hasira na kuwaomba kutii sheria pasipo shuruti.

Pia aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini,viongozi wa mila na watu mashuhuri kushiriki kikamilifu katika kutatua na kuimarisha hali ya utulivu ambayo inahitaji kurejeshwa.

CHANZO: NIPASHE
 
Vipi kuhusu hao polisi walioua raia bila makosa wao watafikishwa mahakamani lini?au roho za watu hazina thamani sawa na hiyo ya 170,000 kwa maana ya mlango na bendera vyote mali ya c.c.m?

Hii ni Tanzania yetu wote,msije kuifanya wote sisi na nyie tuione chungu!i hate ukaburu wa namna hii
 
Back
Top Bottom