Watu wazima wananitisha na maoni yao kuhusu ndoa........

huwa nasema mara nyingi sana humu, ndoa ni kama mkataba, ambao kwa wakristu haufutiki waislamu wanachance ya kuubadili.
ni kiapo mbele ya Mungu wako kwamba utakaa na mtu wake (mke/mume) kwa heshima na kumjali kama kiumbe special wa Mungu.
MAmbo ya mapenzi na mengineyo huwa yanatakiwa yawe vikolezeo tu.
Wewe tuliza kichwa, fanya maamuzi ya mtu wa kukaa naye, REGARDLESS
Kwa mantiki hiyo inabidi utumie busara wakati wa kufanya maamuzi, siyo hisia uongozwe na matamanio, huruma, au woga.
Kuwa jasiri, omba ushauri, angalia kwa makini, fungua macho yote mawili.
Nakutakia mafanikio mema.
Wengi wenye kutegemea wenzi wawaletee furaha ambayo wenyewe hawana, pesa ambazo wenyewe hawana, sifa ambazo wenyewe hawana huishia kuwa disappointed.
Reaction zake huwa ni back and forth. Matokeo yake yanakuwa mzunguko wa kulipizana kisasi, kuonyeshana dharau, au ubabe nk.
Ambao bado kujifunga hebu fungueni macho mjifunze toka kwetu, msirudie makosa ya tangu zamani.
Inakuwaje mtu anataka kufunga ndoa ambayo ni institution ya kizamani kabisa, lakini hataki hata muongozo mmoja wa kizamani? LAzima atafeli tu.
 
Back
Top Bottom