Mikael Aweda
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 2,973
- 3,901
Wakuu leo ktk safari zangu za kikazi nilikuwa mkoa wa Pwani wilaya ya Kisarawe kata ya Msimbu na kijiji cha Mwanzo mgumu. Nilipofika habari zilizozagaa kila kona kijiji kizima ni habari ya watu ambao wenyewe wanawaita mabaunsa waliovamia chumba cha kuhesabia kura 27/5/2012 na kupora masanduku yote ya kura na kutokomea kusikojulikana.
Huu ulikuwa ni uchaguzi mdogo wa kijiji cha Mwanzo Mgumu ambao ulikuwa na ushindani mkali kati ya Chadema na CCM.
Habari zinasema tangu awali ilionekana wazi kuwa Chadema wangeshinda kwa mbali. Uchaguzi ukafanyika na kura zikapigwa. Wakati wa kuhesabu kura na kabla hawajafika hata nusu ya kuhesabu kura huku CCM ikiwa na kura 21 na Chadema 103 ndipo mabaunsa hao walipovamia chumba hicho na ikawa mwisho wa stori.
Cha kushangaza mpaka leo watu hao hawajajulikana na haijajulikana walitumwa na Chama kipi kati ya CCM na Chadema mbaya zaidi hakuna aliyekamatwa. Wengi wanahisi kuwa pengine ni CCM kwa kuwa kipindi chote cha kampeni ilionekana kulemewa sana kutokana na mgombea wake kutokubalika. Nasisitiza CCM inahisiwa tu na hakuna ushahidi wo wote uliopatikana kwa sababu nimeongea na viongozi watatu kutoka kijiji jirani cha Bwama na wote wamesema kwamba hakuna anayejua watu hao walikotoka na aliyewatuma.
Huku kijiji kimojawapo cha kata ya Kibuta, (jirani na kata ya Msimbu) wilaya ya Kisarawe mapema kidogo (siyo mwezi huu) kulikuwa na uchaguzi wa serikali ya Kijiji hicho ambapo CCM walishinda kwa kupata kura 107 huku Chadema ikipata 64.
Waandishi wa habari za magazetini ambao ni wanaJF nawapa Changamoto mtupe details ya hii habari. Kutoka chanika (ilala Dsm) ni kama km 50 or Less tu na utakuwa pwani ndani ya kijiji cha Mwanzo mgumu. Mimi sikuwa na Muda wa kukaa kutokana ratiba niliyokuwa nayo.
My take.
Mvutano mkali kati ya CCM na Chadema ktk mkoa wa Pwani (nyumbani kwa baba Riz) na ngome ya CCM inatupa ishara gani 2015?