Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,013
- 10,170
Leo majira ya mchana kuna jamaa wamepora begi la hela na kuanza kukimbia nalo katikati ya jiji la Mwanza huku wakikimbia kwenda kugawana wakati wananchi wengine wakifukuzia mchongo jamaa wakatumia mbinu ya kuchua mabunda kadhaa na kuyarusha hivyo wananchi wengine wakabaki wanagombea hela jamaa wakasepa. Nimeiweka kwenye tetesi kwa kuwa sijathibitisha kwa undani japokuwa nilikuta tukio limefanyika dakika kadhaa zilizopita huku wananchi wakijadili hili tukio, labda wenye habari kamili watujuze maana sijaiona hii habari hasa kwa Star tv