Watu wanasema hakuna mapenzi ya kweli je ni kweli? Yamemtokea jamaa yangu pale IFM

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,909
32,335
Wakuu wa MMU.

Jamaa yangu mmoja alikuwa na mpenzi wake pale chuo cha IFM alikuwa anampatia huduma zote na alikuwa anaamini siku mmoja atakuwa mke wake wa ndoa.

Lakini jamaa yangu akawa anasema huyo mwanamke wakati mwingine anakuwa amini kama kweli anapendwa na huyu mwanamke siku mmoja akaamua kumjaribu kama anapendwa...Maongezi yalikuwa hivi.

Jamaa: Hallow sweet...

Bint: Poa.

Jamaa: Baby tunaweza kuonana leo?

Bint: Hapana leo naenda kumpokea baba airport.

Jamaa: Na kesho je baby!

Bint: Sitaweza kesho namsindikiza mama harusini.

Jamaa: Basi nitairudisha au nitamtumia mdogo wangu kijijini.

Bint: Nini hiyo Sweet wangu jamani?

Jamaa: Nilikununulia simu ya Blackberry Touch Mlimani City jana.

Bint: Aaah Baby wangu jamani asante nitakuja leo hata ukitaka nilale huko huko nitalala Sweet.

Jamaa: Vipi huendi tena kumpokokea baba na kumsindikiza mama harusini?

Bint: Hakuna kitu nilikuwa nakutania tu baby wangu.

Jamaa: Na mimi nilikuwa nakutania.

Bint: Nyoo! Usinipigie simu tena na wala nisikusikie tena unanitafuta.

Jamaa akaamua kujitoa na kuaongalia ustaarabu mwingine.
 
Kungekuwa na double like ningekugongea mkuu. Wanawake wa sikuhizi ni kudeal nao kwa umakini wa hali ya juu yaani wapo kifedha mno!!!!!

Hii ni kutokana na umaskini ulijijenga katika akili zao hata katika zama hizi ambazo mwanamke yupo mbali sana.
 
Hii umeitoa kwenye jokes mkuu,ila we ni great thinker kwa ulivoitengeneza congrats
 
Kaka huu ndio ukweli halisi wa mahusiano ya Vyuoni. Kitendo cha madenti kuchelewa kupata mikopo/ Hali ngumu ya maisha kwa wanafunzi wawapo chuoni ndio inayowalazimu hawa madada zetu kutafuta plan B ili kuweza kupata baadhi ya mahitaji yao. Ukweli ni kwamba wengi wao wanakuwa na mafiga matatu. Baada ya kumaliza masomo huwa wanaangalia ustaarabu mwingine.
 
Kungekuwa na double like ningekugongea mkuu. Wanawake wa sikuhizi ni kudeal nao kwa umakini wa hali ya juu yaani wapo kifedha mno!!!!!

Hii ni kutokana na umaskini ulijijenga katika akili zao hata katika zama hizi ambazo mwanamke yupo mbali sana.

duh hiyo kali kweli kweli...yaani ingekuwa mimi ningemnyoosha....wadada wanapenda sana kupewa vitu vya dhamani na bado wanataka haki sawa...ipatikane wapi kwa mtindo huu?
 
Zawadi ni chachandu katika mapenzi ila kwa namna ambayo huyo mwanamke anafanya ni ulaghai wa mapenzi.
 
Hiyo ni kama hii:-
Boy: Baby I love you so much I can cross the ocean for you.
Girl: That's so sweet. Can you come over to my place?
Boy: No I can't
Girl: Why not?
Boy: Its raining!
 
Rawama zimezidi mapenzi ya vyuoni, binti kidato cha 4 anawapenzi wawili form 6 anamwacha mmoja wa form4 anaongeza wa form 6 na wa mtaani mmoja kwasababu matumizi yameongezeka akifika chuo anamwacha aliyekuwa nae form 4 anabaki na wa form 6 kama naye anaendelea na masomo na yule wa mtaani, kisha anaongeza mmoja au wawili akiwa chuo. Sasa unatarajia mapenzi ya kweli yatoke wapi?
 
Back
Top Bottom