Watu wanapotamani kukusahau!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Huko katika himaya ya Kirumi kulikuwa na watawala kadhaa. Kati ya hao kulikuwa na watawala wakiitwa Caligula na Nero.


Huyu Caligula alimuua baba yake mama yake na kaka zake wawili ili aweze kutawala. Huyu Nero naye ili awe Mtawala aliwahi kuwauwa mama yake na mkewe wa zamani. Watawala hawa walichukiwa sana kuliko kitu kingine kiasi kwamba hata habari zao zilifutwa kabisa kwenye rejea ya viongozi wa himaya ya Kirumi.

Hebu fikiria, kwa kutamani madaraka mtu anafikia mahali historia yake inaamuliwa kufutwa ili vizazi vimsahau kabisa.

Je kwa hapa kwetu hatuna aina ya viongozi ambao ingekuwa ni vyema majina yao yakaondolewa kwenye vitabu vya rejea ili pindi watakapokufa wasahaulike kabisa?
 
Back
Top Bottom