Watu wamechoka na chaguo la Mungu?

Shetani ni mjanja sana!kajigeuza malaika kuwaadaa viongozi wa dini!aibu kwao!dini biashara sa hivi
 
Napata shida kuhusu kauli zilizodai kuwa JK ni chaguo kutoka kwa Mungu au ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa Watanzania. Kweli hali tuliyonayo ni adhabu tosha kwa WTz.
 
Napata shida kuhusu kauli zilizodai kuwa JK ni chaguo kutoka kwa Mungu au ni adhabu kutoka kwa Mungu kwa Watanzania. Kweli hali tuliyonayo ni adhabu tosha kwa WTz.

Nyie ndo hamjui hili nai chaguo la MIUNGU
yahaya hussein na wenzake
 
Watu wamechoka na chaguo la Mungu?

Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KWA muda wa wiki moja sasa, Rais Jakaya Kikwete yupo mkoani Mbeya akiendelea na ziara yake ya siku 10, kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya mkoa huo. Pamoja na kukagua shughuli za maendeleo, rais pia anapata fursa ya kuzungumza na wananchi.

Katika kuzungumza huku, kwa kuwa hii ni mara yake ya kwanza kwenda Mbeya tangu achaguliwe kuwa Rais, ni dhahiri kuwa anatumia wasaa huo kuwashukuru wananchi wa mkoa huo kwa kumpa kura. Amekuwa akifanya hivi kila mkoa anaotembelea.

Pia, kwa upande mwingine, ratiba ya rais kuzungumza na wananchi, inatoa fursa ya aina yake kwa wananchi nao kuzungumza na rais. Bila ya shaka, katika mazungumzo yao, wananchi hao wamekuwa wakimsuhukuru rais kwa kuwatembelea. Baada ya hapo, hufuata mlolongo ya malalamiko yakionyesha kero na matatizo wanayokabiliana nayo.

Ni dhahiri kuwa kero za watu wa mkoa wa Mbeya ni nyingi sana kwa sababu zimerundikana kwa muda mrefu. Hii inatokana na Rais Kikwete, kuaharisha ziara ya kuutembelea mkoa huo. Kumekuwa na maneno mengi sana kutokana na hilo, ingawa kwa sasa, inaelekea kuwa linageuzwa kuwa suala la kisiasa zaidi.

Katika ziara hiyo ya mkoani Mbeya, Rais Kikwete, amekumbana na mkasa wa aina yake pale msafara wake uliporushiwa mawe na wananchi wa kijiji cha Kanga wilayani Chunya, baada ya wananchi kumsubiri siku nzima lakini alipopita hapo hakusimama kuwasalimia. Wananchi hawa walimsubiri kwa hamu kubwa rais wao, ili wamweleze yao ya moyoni, lakini aliwapita akiwaachia vumbi tu.

Bila ya shaka, subiri yao ilitokana na ratiba waliyopewa ikionyesha kuwa rais atasimama hapo na kuwasalimia. Ndiyo maana walijiandaa. Kama wangekuwa wameambiwa kuwa rais hatosimama hapo, sidhani kama wangejisumbua kukaa kumsubiri.

Kimsingi hatua hiyo ya wananchi kuurushia mawe msafara wa rais, ni jambo lisilokubalika katika jamii ya kistaarabu. Lakini pia ni jambo la hatari yenye kutia aibu kwa viongozi, akiwamo kiongozi mkuu wa nchi, ambaye kila kukicha amekuwa akihimiza uvumilivu, mshikamano na umoja baina ya Watanzania.


Jamii ya watu waliostaaribika hawapaswi kufanya kitendo kama hicho, bali hutumia njia za kistaarabu kufikisha ujumbe wao. Licha ya kuwa ni aibu yenye kusababisha hasara, vurugu kama hizo zinaweza kusababisha mtu kukamatwa, kushitakiwa na kufungwa jela kwa muda mrefu. Pia tabia hiyo inaweza kusababisha majeraha kwa watu wengine ambao hawahusiki kabisa na hasira za wananchi.

Wananchi walianza kwa kuwazomea mawaziri na watendaji Serikali waliokuwa wakitembea mikoani kutangaza uzuri wa bajeti mwaka jana. Hiki kilikuwa ni kitendo cha kihistoria. Lakini mwitikio wa wananchi ulipaswa kuwa somo kwa viongozi hawa.

Baada ya matukio hayo, walipaswa kukaa na kujiuliza kulikoni wananchi ambao walikichagua chama chao kwa kura nyingi, wameanza kuzomea? Sijui kama hili lilifanyika.

Wananchi walikerwa na ziara hizo ambazo zilikuwa zikitumia mamilioni ya shilingi huku wao wakiogelea katika lindi la umasikini. Waliamini kuwa fedha zilizotumiwa na mawaziri kuzunguka mikoani, zingeweza kutumika kuboresha zahanati, kununua dawa, kujenga shule, barabara, huduma za maji na nyingine ambazo ni mbaya.

Hasira za wananchi hao zinaelekea kukua hivi sasa na hata kufikia kuonyesha chuki za wazi kwa kiongozi mkuu wa nchi ambaye wamethubutu kuurushia mawe msafara wake kwa kile kinachodaiwa kuwa rais hakusimama eneo lao ili wamweleze matatizo waliyo nayo.

Kitendo hicho kinaonyesha jinsi wananchi walivyokata tamaa ya maisha kiasi cha kuwa tayari kufanya vitendo vya hatari ambavyo wakati mwingine vinaweza kusababisha vifo au vilema vya maisha.

Kama askari waliokuwapo kwenye ziara hiyo wangeamua kuwafyatulia risasi wananchi hao kwa vyovyote hali ingekuwa mbaya zaidi na pengine tungeshuhudia vurugu tunazoziona kwenye vyombo vya habari zikitokea nchi nyingine mbalimbali ndani na nje ya bara la Afrika.

Dalili za hasira za wananchi na kuishiwa kwao uvumilivu zilionekana tangu mwanzo wa ziara hiyo pale wakazi wa Mwanjelwa, Mbeya walipousimamisha msafara kwa kulala barabarani. Hao walimtaka rais awafikishe mahakamani mafisadi walioiba fedha za EPA, wala rushwa na kutimiza ahadi zake za maisha bora ambayo sasa zinaonekana kutotekelezeka. Alipowajibu na wao kwa kuonyesha kutoridhishwa na majibu yake, inadaiwa kuwa walizomea.

Ni jambo lililo wazi kuwa kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo ugumu wa maisha unavyozidi na hata wananchi waliokuwa wakimudu kula milo mitatu kwa siku hivi sasa wanapata mlo mmoja.

Wakati wananchi hao wakipata mlo mmoja kwa siku, kila kukicha, watendaji wa Serikali wamekuwa wabunifu kutafuta magari ya kifahari na samani na kununua kwa bei ghali bila kujali kilio cha maisha magumu ya wananchi.

Hivi sasa Serikali imenunua magari mapya aina ya Toyota Land Cruizer V8 kwa ajili ya mawaziri wake, ambayo bei yake kila moja haipungui sh milioni 100.

Kila kukicha nchi imekuwa na migomo ya wafanyakazi isiyomalizika, huku juhudi za kuitatua migomo hiyo zikionekana kuwa ni dhaifu na hata watendaji wa Serikali nao wanaelekea kutokuwa na mbinu mpya za kutatua matatizo. Sasa wamegeuka kuitegemea mahakama!

Kwa ujumla, nchi inaelekea kubaya na ni vema Rais Jakaya Kikwete, akasoma alama za nyakati, na kuchukua hatua mufaka ili kukomesha hali hii. Kama asipoangalia, hali itegeuka kuwa mbaya zaidi na akichelewa kuchukua hatua, itafika mahali atashindwa kabisa kuwa na udhibiti wa hali ya mambo.

Watanzania ni mashahidi wazuri wa ahadi alizozitoa rais Jakaya Kikwete. Mojawapo ikiwa ni ile ya kuzalisha ajira milioni moja, jambo ambalo kwa hivi sasa linaonekena kuwa gumu kwani watu wengi hivi sasa wanapoteza ajira zao.

Leo hii Rais kikwete anapouambia umma kuwa ameongeza ajira kwa Watanzania kuanzia kwa wafanyakazi wa ndani, wafanya usafi bustanini, wachunga ng’ombe na wengineo ni jambo la kushangaza sana.


Ajira wanazoitaka Watanzania si hizo alizozitaja, bali ni zile zinatotambulika na zenye mchango mkubwa kwa taifa kwa maana ya kuingiza mapato yanayotokana na kodi za mishahara ya wafanyakazi pamoja na kuwa na pensheni mtu akifukuzwa au kustaafu kazi.

Ajira hizo anazojisifu nazo rais Kikwete zilikuwapo tangu zamani, hivyo hakuwa na haja ya kujisifia kuwa ameongeza ajira kwa Watanzania.

Leo hii Serikali imekuwa ikiimba wimbo wa uchumi kupanda, lakini ukiangalia maisha ya mwananchi wa kawaida yanazidi kwenda mrama siku hadi siku. Mambo kama haya yanawafanya wananchi wajuione kama wanahadaiwa.

Moja kati ya dai walilolitoa wananchi wa Mbeya walipomzuia Rais Jakaya Kikwete ni kuhitaji maji ambayo aliwaahidi alipokuwa akiwaomba kura zao lakini mpaka sasa bado hawajayaona.

Kwa hali ilivyo hivi sasa, inaelekea rais Kikwete ameelemewa na mambo mengi na anashindwa kuzitekeleza ahadi zake alizozitoa alipokuwa akipita kuwaomba wananchi ridhaa zao za kumchagua kukalia kiti cha urais kwa tiketi ya CCM.

Wananchi waliamini ugumu wa maisha utatoweka pindi wakimpa kura Rais Kikwete, ndiyo hao hao waliokata tamaa ya maisha na kuamua kumrushia mawe au kuwazomea watendaji wake.

Inasikitisha kuona nchi ya Tanzania yenye rasilimali za kila aina ikiendelea kuwa maskini kwa sababu ya rasilimali zake kubinafsishwa kwa wawekezaji kwa bei za kutupa.

Kurushiriwa mawe huko ni dalili mbaya zaidi kwani inaonyesha kuwa kama wananchi hao wangekuwa na silaha za kisasa basi mambo yangekuwa mengine.

Nahisi watu wa mbeya walishaona shida ya huu uongozi muda mrefu. Je ukombozi utaanzia mbeya?
 
Back
Top Bottom