Watu wa JK sasa wanawalaumu Waandishi wa Habari.

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Nani kumfuata Chenge? (Tanzania Daima)




na Mwandishi Wetu



KUNA kila dalili kwamba, mkakati maalum wa kuwasafisha kwa zamu mawaziri wanaoandamwa na tuhuma za kifisadi ndani ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete unaendelea.

Habari ambazo Tanzania Daima imezipata kutoka vyanzo kadhaa vya habari ndani ya serikali na miongoni mwa wanasiasa zinaeleza kwamba, bado kuna mawaziri wengine zaidi ndani ya serikali ambao wataanza kushughulikiwa na kufuatiliwa nyendo zao baada ya kuanguka kwa aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge.

Tayari majina ya mawaziri ambao wataingia katika mkumbo huo wa ‘tuhuma nzito za kifisadi’ yameshaanza kuandaliwa na kinachosubiriwa sasa ni mabadiliko ya mawaziri yanayotarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa.

Baadhi ya wanasiasa waliozungumza na Tanzania Daima waliyataja majina ya baadhi ya mawaziri ambao iwapo watarejeshwa katika Baraza la Mawaziri atakaloliunda tena Rais Kikwete, wanaweza wakakabiliwa na tuhuma nzito za ufisadi ambazo hatimaye zitawalazimisha kujiuzulu.

Pamoja na kuendelea kuwapo kwa hofu ya mawaziri wengine kufuata mkumbo wa kuanguka, viongozi kadhaa waliozungumza na gazeti hili wameeleza kwamba, hali hiyo imesababisha kuanza kwa mapambano makali ya kisiasa miongoni mwa makundi ndani ya CCM na serikalini katika kuiangalia hali hiyo na namna ya kukabiliana nayo.

Baadhi ya wanasiasa waliozungumza na Tanzania Daima kwa siku kadhaa sasa wameanza kueleza wasiwasi wao kuhusu mtazamo wa Rais Kikwete katika kukabiliana na mwenendo huo wa mambo ambao kwa kiwango kikubwa unaonekana kuitikisa serikali na kuanza kuwatia hofu baadhi ya wanasiasa.

Chanzo cha kuaminika cha habari kutoka Ofisi ya Rais Ikulu kinaeleza kwamba, kundi moja ndani ya serikali limefikia hatua ya kumtaka Kikwete kuanza kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo inayoweza kuimaliza na kuiyumbisha kabisa serikali yake.

Mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Rais Kikwete aliyezungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki iliyopita alisema, baadhi ya viongozi serikalini wameanza kuwalaumu wanasiasa na wanahabari kuwa chanzo kikuu cha kumegeka kwa Serikali ya Kikwete kutokana na tuhuma hizi za kifisadi.

“Unajua kinachoonekana sasa ni kwamba, ninyi waandishi mmeacha kabisa kuandika mambo mengine ya msingi yanayohusu uchumi na maendeleo ya kijamii, na mmekazana kuwatafuta watu uchawi na kuandika madhambi yao. Hali hii ni lazima idhibitiwe. Uandishi wa aina hii haupo duniani kote zaidi ya hapa,” alisema ofisa huyo wa juu serikalini.

Alipotakiwa kueleza iwapo tuhuma dhidi ya mawaziri na baadhi ya wanasiasa hazimgusi Kikwete mwenyewe moja kwa moja, ofisa huyo alisema takriban masuala yote mazito yanayohusu ufisadi yanayozungumzwa katika siku za hivi karibuni, ukiacha sakata la Richmond yalitokea wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

“Leo hii mnamtuhumu Chenge kwa mambo yaliyotokea zama za Mkapa. Ukiacha suala la Richmond, tuhuma takriban zote dhidi ya ufisadi wenu huu haziigusi Serikali ya Kikwete leo, ni za watangulizi wake. Sasa kwanini mnamhusisha rais?” alisema ofisa huyo.

Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya CCM aliyezungumza na Tanzania Daima kuhusu mwenendo huo wa mambo hivi sasa, alisema tayari baadhi ya makada wa chama hicho na watu walio karibu na Kikwete wameshamuonya kuhusu haja ya kuanza kuchukuliwa kwa hatua za dharura za kukabiliana na wimbi la mawaziri kujiuzulu kutokana na kashfa.

Mwana CCM huyo ambaye kwa miaka mingi amekuwa karibu kikazi na Kikwete, alipoulizwa msimamo wa rais kuhusu matukio haya ya mawaziri wake kubebeshwa tuhuma nzito za ufisadi, alikataa kueleza lolote zaidi tu ya kusema:

“Hali hii kwa kweli imeanza kututisha baadhi yetu, na tuna wasiwasi ambao tayari tumeshamfikishia Jakaya, tukimtaka achukue hatua za kuzuia hali hii ya watu kuchafuana.

“Tumemueleza JK waziwazi sisi kama taifa hatujafikia hatua ya kutoa uhuru mpana wa namna hiyo ambao ni jambo la hatari, kwani baadhi ya wenzetu wameanza kutumia uvumilivu wa rais kujenga uzushi dhidi ya wenzao. Unajua huyu mtu siku zote ni liberal,” alisema mwana CCM huyo.

Hata hivyo, mwana CCM mwingine aliyezungumza na Tanzania Daima kuhusu matukio haya ya viongozi kulazimishwa kujiuzulu alisema, baadhi ya makada wenzao wameshaanza kujiuliza iwapo matukio haya hayana baraka za Kikwete ambaye ndiye Mwenyekiti wa taifa wa CCM na rais mwenyewe.

“Tumeanza kupata hofu kwamba, kuna uwezekano kuwa Bwana Mkubwa (rais) amekuwa akiunga mkono na kushangilia kuanguka kwa marafiki zake na mawaziri wanaokumbwa na kashfa mbalimbali katika siku za hivi karibuni,” alieleza mwana CCM huyo ambaye alifikia hatua ya kuuliza iwapo kulikuwa na mawasiliano kati ya wanahabari na Ikulu.

Hata hivyo, mwanasiasa mmoja ambaye ni kiongozi wa juu Umoja wa Vijana wa CCM aliye karibu na Chenge, alilieleza Tanzania Daima kwamba, mwanasiasa huyo alikuwa ameshaanza kujiandaa kutoa ufafanuzi kuhusu dola za Marekani zaidi ya milioni moja zilizokutwa katika akaunti yake katika visiwa vya Jersey nchini Uingereza.

Kada huyo wa CCM alisema pia kwamba, tayari mwanasiasa huyo alikuwa ameshaanza kuwasiliana na kiongozi mmoja wa juu wa dini ambaye ndiye anayehusishwa na fedha hizo kama hatua ya mwanzo ya kujisafisha dhidi ya tuhuma hizo nzito.

“Mzee ameshaanza kuwasiliana na mtu ambaye aliziingiza fedha hizo katika akaunti yake mwaka 2002 kwa malengo mahususi, kabla ya kuwatangazia Watanzania ukweli kuhusu akaunti hiyo ambayo imeshaanza kuchunguzwa iwapo ina uhusiano na fedha zinazoaminika kutolewa kwa rushwa wakati serikali iliponunua rada ya kijeshi kutoka Uingereza,” alisema kada huyo wa CCM.

Tanzania Daima ilipowasiliana na Chenge kwa simu jana alasiri kuzungumzia kuhusu suala hilo, alimtaka mwandishi kumpa muda wa kupumzika na kumwacha atulie kutokana na uzito wa masuala anayokabiliana nayo.

“Ndugu yangu sasa hivi ninakabiliwa na majukumu mazito, siwezi kuzungumza chochote kuanzia leo, kesho, kesho kutwa au mtondogoo kwa vile siko katika nafasi nzuri… nawaomba mniache... Sasa hivi niseme nini? Muda ukifika sawa... lakini ungekuwa wewe ungeweza kujibu nini katika kipindi kama hiki, niacheni tu ndugu zangu,” alisema Chenge.

Alipoelezwa na mwandishi wa habari hizi kuwa kulikuwa na taarifa kuwa alipanga kukutana na waandishi wa habari hivi karibuni kutoa ufafanuzi wa fedha zilizokutwa kwenye akaunti yake, alikana na kusema hana mpango wa aina yoyote wa kukutana nao kwa sasa.

“Nani kakwambia nakutana na waandishi wa habari? Sina mpango wa aina hiyo na wala hakuna kitu kama hicho kwa sasa… nipeni muda ndugu yangu, nakutakia kazi njema,” alisema Chenge.

Akizungumza na Tanzania Daima kuhusu kujiuzulu kwa Chenge na tuhuma za ufisadi, Mwenyekiti wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe alieleza kushangazwa na hatua ya vyombo mbalimbali vya habari kumweka kando Kikwete katika tuhuma hizi.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA, alisema ni jambo lisilowezekana kwa Kikwete ambaye ana vyombo vya usalama kuwateua watu wenye tuhuma nzito, na yeye mwenyewe akaendelea kubakia kuonekana mtu safi.

“Ndege wenye mbawa zinazofanana huruka pamoja. Kikwete hawezi kutenganishwa na ufisadi huu. Angekuwa si mmoja wao asingekubali kukaa meza moja na watu ambao wanakabiliwa na tuhuma nzito za rushwa,” alisema Mbowe.

Mwenyekiti huyo wa CHADEMA alisema, iwapo Kikwete angekuwa safi, basi asingesubiri mpaka watu watuhumiwe ndipo akubali kujiuzulu kwao kabla yeye mwenyewe hajachukua hatua ya kuwafukuza kazi.

Mbowe anatoa kauli hiyo, ikiwa ni siku moja tu baada ya viongozi wa ushirika wa vyama vinne vya upinzani kuandamana hadi katika Tume ya Maadili ya Viongozi na kutaka kupata maelezo kuhusu mali alizonazo Rais Kikwete na viongozi wengine kadhaa wa juu.
 
Fisadi mtoto Heshima mbele:

Kwani baba yake ni waziri? Au miongoni mwa waliotajwa yupo mzazi wako? Mwaka huu mmeshikwa pabaya hakuna kupumua.
 
Amang'ana ghasarikele tata taitakya, hatuwezi kuwa na serikali kila kukicha fulani kajiuzuru, this is the time for us to think,ila huyu Kikwete kama vile anakajua kamchezo ka kuwatosa jamaa zake, ama mnaonaje jamani?
 
Back
Top Bottom