Zakumi,Mimi historia ya Tanzania sijuhi vizuri lakini naichambua kwa vigezo vyangu.
Historia ya nchi nyingi za kiafrika zimepikwa na kuwakuza watu pale isivyo. Nyerere amechukua uongozi wa TAA akiwa na miaka 31 au 32. Ndio kwanza amerudi na hajajijenga. Na zaidi ya hapo alikuwa na familia changa.
Ukichukua umri aliyokuwa nayo na mazingira ya wakati utaona kuwa historia ya Tanzania nayo imepikwa.
Ukienda upande wa Kaskazini ya Tanzania, watu wa mwanzo kuanzisha chama cha ushirika barani Africa, utaona kuwa Tanzania haikusubiri mpaka TANU ianze ili wadai uhuru wao.
Vilevile mapambano ya kudai uhuru Tanganyika yanakuwa Exaggerated. Mwingereza hakuwa na faida yoyote ya kukaa Tanganyika.
Alichofanya Nyerere ni kuunganisha pamoja juhudi zote za kupigania uhuru kote nchini chini ya TANU. That was no small feat, Karl Peters notwithstanding.