alisema nini shiekh takadir?
Hujui aliyowatahadharisha wana TANU kuhusu alivyoanza kumuona Nyerere akiwaondoa Waislam mmoja baada ya mwingine kwa majungu. Shehe Takadir akalizungumza hilo bayana, Nyerere akalia katika mkutano na kusema Takadiri ni MTAKA DINI.
Tangu siku hiyo akatengwa kabisa, manake ilionekana ukiwa karibu na Shehe Takadiri ni msaliti. Na kuna siku kundi lilitoka na kuelekea kwa Takadir lililopangwa na Nyerere likaenda mpaka nyumbani kwa huyu Marhum, likaanza kumzomea, kumkejeli, kumtusi kwa kila lugha mbaya. Akatoka ndani kwake na kuwaambia waliokuwepo (wengi Waislam), MTANIKUMBUKA.
Kweli aliyosema yalitokea, UDINI ulioonyeshwa na Nyerere ndio huo aliusema Takadir, hivyo kweli alisema Marhum Shehe Takadir.