Watu Hupata Wapenzi Wanaowastahili

Ndo hapo sasa. . .
Au unamkubali mtu ukiwa unajua fika ni mnywaji ilaa baadae unaanza kulalamika kuhusu trip zake za bar.
another problem that faces people who throw themselves in a relation with people who don't match their expectation: expecting change in the partner's behavior wakati wenyewe hawako tayari for a change in our level of tolerance.
Na ndio maana uito wa Companeiro hautasikika leo. they still hope that the person will change...
 
Ndo hapo sasa. . .
Au unamkubali mtu ukiwa unajua fika ni mnywaji ilaa baadae unaanza kulalamika kuhusu trip zake za bar.

huu mfano ulioutoa unasamaraizi mada nzima, mtu akiuelewa basi somo lote limeeleweka!
 
Ule msemo wa 'people get the president they deserve' (watu hupata rais aliye stahili yao) una ujumbe muhimu katika MMU. Kama una mpenzi ujue yeye ndiye stahili yako. Hivyo, acha kudai eti oh huna bahati ya kuwa na mtu mzuri maishani. Hukulazimishwa kuwa naye. Na hulazimishwi kuendelea kuwa naye tu. Daima uamuzi ni wako. Tulia. Tafakari. Chukua hatua. Usihofu. Fanya maamuzi magumu. Ndio. Leo leo. Usisubiri kesho maana kesho haiji.

.....umesema kweli tupu. Mapenzi ni maamuzi.
 
Ndo hapo sasa. . .
Au unamkubali mtu ukiwa unajua fika ni mnywaji ilaa baadae unaanza kulalamika kuhusu trip zake za bar.

.....lol, ulevi, uvutaji sigara nk ni tabia zinazobadilishika bana
 
haiwezekani. watu waache kulalamika. walichonacho ndicho wanachokistahili. kama vipi watimue.

.....dahh,....

Hapana bana. Mgomba huo, palilia. Siwezi nunua jumba kuu kuu nikaacha kulitia lipu na rangi ati ndio majaaliwa yangu.

Nikijikubalisha udhaifu unaobadilishika ina maana mie ndie nahitaji ushauri nasaha kuliko yeye.
 
Napenda kale kamsemo kakizungu kana kizungu zungu, lakini kana saidia.

Birds of a feather flock together :A S thumbs_up:
 
na hasira, kisirani, wivu, uongo, kutotulia, ubazazi n.k je?

.....hayo ni mapungufu yanayoweza kupungua kadri mapenzi yanapozidi na kuendelea.
Umegundua? Ukitaka kutomla kuku wewe anza kumchambua jana kala nini, kalala wapi, nk nk?

Kiti moto anagombewa japo mchafu tena ala mavi yake na ya wenzake. Hutaona mapungufu ya mtu mpaka utake, na kuachana nae ni visa tu. Love is choice.
 
Hasira nayo ni tabia?

Yote hayo yanaweza kutoweka iwapo mhusika ataona amepata sababu ya kuacha au yamemchosha yeye mwenyewe.

Umeona ee Lizzy?.....Mapenzi ni 'kujikubalisha' na mapungufu ya mwenzio kama yeye alivyojikubalisha na ya kwako.

Love is 'seeing the imperfect partner perfect'...kuna mambo mtakubaliana yapunguzwe, na mengine yaachwe. Yale yatayoshindikana, kama ni kweli unampenda na kumthamini, itakubidi uyakubali ni majaaliwa yako. ;)
 
Last edited by a moderator:
Na kweli wifi, lol! If he thinks you are worth it, ataweza ku-adjust ili muwe na furaha as long as its not an unnecessary demand.
Inawezekana Mbu ila mpaka mhusika aamue na sio mke/mune amlazimishe kwa malalamiko yasoisha.
 
Na kweli wifi, lol! If he thinks you are worth it, ataweza ku-adjust ili muwe na furaha as long as its not an unnecessary demand.

...".he/she thinks you WORTH ku adjust ili muwe na furaha"....

Quote of the week.

Wengi hupuuzia hili. Enzi za ujana hata mimi nilijidanganya ati mtu akini PROMISE, ndio mwisho wa mdahalo, .....lakini na uzee huu?! sidanganyiki.

I can only measure uzito wa penzi letu linavyothaminiwa kwa vitendo na mienendo yenye kuleta furaha miongoni yetu, japo kutakuwa na setbacks mbili tatu 'zinazokubalika'

Kama hatotaka ku-"adjust" mapungufu yake. yanini kujibebesha 'kabati la matatizo?'
 
Maisha yetu ya kibongo bongo tunapambana humo humo bora yende yakhe
Kufa na Tai Shingoni..
..Nakumbuka wakati wa nasaha za wazazi wa pande zote utasikia
Jamani maisha ya ndoa yana milima na mabonde .
Wanangu muwe wavumilivu
Vumilianeni.. Companero wewe vip upande wako?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom