Watu hawa hawajui madhambi ya jk au ni unafiki wa watanzania?????

Mkatavimeo

JF-Expert Member
Jan 3, 2011
2,150
868
Wana JF, nimeziangalia hizi picha nikapata huzuni kubwa sana! naomba mnijuze, hivi hawa wanaomchekea JK na kushikana nae mikono ni kweli wanampenda au unafiki na njaa zao vinawafanya wajipendekeze wakijua watapata chochote kitu wasogeze maisha yao?
GO9G0145[1].JPG View attachment 25462View attachment 25463

Compare hizo picha na hiyo attachment tafadhali.
 
Attachments

  • Picha%20za%20kusikitisha[1].doc
    1.4 MB · Views: 114
Picha hizi zinatisha sana na laiti CCM wangekuwa wanaongozwa na watu wenye hekima leo hii wangetangaza kujiuzulu na kukivunjavunja chama. Pia kama Msajili wa vyama vya siasa angekuwa na hekima kama mfalme Sulemani angekifutia usajili Chama cha Mapinduzi kwani kimewaletea umasikini, maradhi na dhiki za kila aina wananchi wa Tanzania tofauti na matarajio ya Katiba ya nchi na katiba ya chama chenyewe. Kwenye katiba zote hakuna sehemu inayosema kuwa chama kikiingia madarakani kazi yake ni kufilisi mali za wananchi na kuwaongezea umasikini na ugumu wa maisha. Mpaka hapo CCM imeshavunja katiba ya nchi na katiba yake pia. CCM ifutwe au wananchi waamue cha kufanya.
 
Sielewi mantiki ya mwanzisha mada.
Pamoja na kwamba wapo wanomchukia JK (ukiwemo wewe) lakini pia wapo wanaompende(kutokana na sababu zao)
So cha kuchangaa hapa ni nini?
 
Sielewi mantiki ya mwanzisha mada.
Pamoja na kwamba wapo wanomchukia JK (ukiwemo wewe) lakini pia wapo wanaompende(kutokana na sababu zao)
So cha kuchangaa hapa ni nini?

NDIBALEMA!

(a) Hapo kwenye RED, inaonyesha jinsi gani uwezo wako wa kufikiria ni mdogo, na unakimbilia kwenye conclusion, kabla hujafanya utafiti wa kutosha! Swala hapa sio kumchukia au kumpenda, bali ni uelewa wa madhambi ya JK kwa wananchi, then kumuunga mkono au kutomuunga mkono.

(b) Hapo kwenye BLUE...kutokana na kukurupuka kwako, unashindwa kuandika maneno ya kueleweka!
 
Wengi wanasukumwa na njaa zao tu. Hakuna mtu anampenda JK kwa namna nyingine mbali na kuganga njaa. Waulize UVCCM utajua nasema nini!
 
Wana JF, nimeziangalia hizi picha nikapata huzuni kubwa sana! naomba mnijuze, hivi hawa wanaomchekea JK na kushikana nae mikono ni kweli wanampenda au unafiki na njaa zao vinawafanya wajipendekeze wakijua watapata chochote kitu wasogeze maisha yao?
View attachment 25461View attachment 25462View attachment 25463

Compare hizo picha na hiyo attachment tafadhali.

Mkuu utakufa mapema sana kama una chuki ya namna hiyo. Hivi wewe akili yako inakutuma watanzania wote wanamchukia Rais wao? Weka akilini kwamba huwezi kupendwa na wote na huwezi kuchukiwa na wote. Hata Slaa wapo wana CDM ambao hawampendi kabisa, tena wengine tunao humu jamvini.
 
Watanzania asilimia kubwa sana hawajui mauozo ya JK na serikali yake, so sio kosa lao kumsabahi.

Kuna wengine baada ya kushikana nae mkono hawanawi kabisa manake wanaona baraka zitaondoka, hawajui wanajiletea mikosi tu.
 
Mkuu utakufa mapema sana kama una chuki ya namna hiyo. Hivi wewe akili yako inakutuma watanzania wote wanamchukia Rais wao? Weka akilini kwamba huwezi kupendwa na wote na huwezi kuchukiwa na wote. Hata Slaa wapo wana CDM ambao hawampendi kabisa, tena wengine tunao humu jamvini.

... iliitwa maisha bora ... tumaini lililorejea ! Leo hii wengine wanaita bora maisha... tumaini ambalo halikuwepo .. ukiacha... UKWERE!
Tofauti ya UKWERE na kabla ya hapo UKAPA na huenda kabla ya hapo enzi za yule mhubiri wa RUKSA unaweza kutana na mtu akasema ni WAISILAMU wawili na mtu mmoja ili mradi ni tafsiri ya mtu. Wapo wengine watasema huyo ni mcheza mdundiko, mla panya na ......

Ukiachana na hayo, umaskini iliokithiri ni reality na so far hakuna efforts za kweli chini ya CCM kuondoa kadhia hiyo. Wanachumia matumbo yao tu.
Siku ile hawa masikini wakutupwa watakapoamka na kuachana na porojo wanazokubali kwa njia ya sahani ya ubwabwa, kanga na upuuzi mwingine ndio siku ya ukombozi wao itakapowadia. Kabla ya hapo, kazi kweli kweli! Umasikini wao wanauendeleza wenyewe!
 
Wana JF, nimeziangalia hizi picha nikapata huzuni kubwa sana! naomba mnijuze, hivi hawa wanaomchekea JK na kushikana nae mikono ni kweli wanampenda au unafiki na njaa zao vinawafanya wajipendekeze wakijua watapata chochote kitu wasogeze maisha yao?
View attachment 25461View attachment 25462View attachment 25463

Compare hizo picha na hiyo attachment tafadhali.
Haya wala yasikushangaze mkuu... kwani mbona hata Gadaffi ana watu wanaomuunga mkono... hata Iddi Amin naye aikuwa na wafuasi waliokuwa wakimshangilia. lakini siku ikifika, hayo yote nayo yatapita
 
Baadhi ya mambo ambayo JK yuko right,hili ni mojawapo "asilimia 70 ya Watanzania ni bendera fuata upepo"
 
Ndiyo upuuzi wa watu wanaofikiri kwa kutumia matumbo. Jk ana lipi la kufanya watu wahitaji kushika mkono wake!!! Unafiki mtupu!!
 
NDIBALEMA!

(a) Hapo kwenye RED, inaonyesha jinsi gani uwezo wako wa kufikiria ni mdogo, na unakimbilia kwenye conclusion, kabla hujafanya utafiti wa kutosha! Swala hapa sio kumchukia au kumpenda, bali ni uelewa wa madhambi ya JK kwa wananchi, then kumuunga mkono au kutomuunga mkono.

(b) Hapo kwenye BLUE...kutokana na kukurupuka kwako, unashindwa kuandika maneno ya kueleweka!

Mkuu wapambe wana nguvu kuliko wenye mali
 
Baadhi ya mambo ambayo JK yuko right,hili ni mojawapo "asilimia 70 ya Watanzania ni bendera fuata upepo"
kila mtu hujiona yuko sahihi maana mawazo yako unaona wewe ndo unajua zaidi "fuatilia kwa makini hoja za mwanasiasa unaempenda kisha zifanyie utafiti kwa undani kutokana na mitandao mbalimbali" kisha utaona wewe uko kundi gani
 
Sioni tatizo watu kusalimiana na rais wao. japokuwa wewe humpendi au unajidai eti madhambi yake lakini bado JK anawafuasi wengi tu. Usijidanganye. sema nyinyi wachache mna midomo mirefu sana mkisaidiwa na vyombo vyenu vya habari. Pole.
 
Ninakumbuka JK mwenyewe kabla ya uchaguzi mkuu aliwahi kufanya utafiti wake (dont ask methodology used in his research). Bottomline utafiti wake ulionesha matokeo yafuatayo.
  1. 25% ya Watanzania wote WANAMPENDA
  2. 25% ya Watanzania wote WANAMCHUKIA
  3. 50% ya Watanzania wote ni BENDERA HUFUATA UPEPO.
I honestly believed he was damm right with his findings
 
Sioni tatizo watu kusalimiana na rais wao. japokuwa wewe humpendi au unajidai eti madhambi yake lakini bado JK anawafuasi wengi tu. Usijidanganye. sema nyinyi wachache mna midomo mirefu sana mkisaidiwa na vyombo vyenu vya habari. Pole.

Hiyo pia inaonyesha nawewe jinsi gani unachuki tena utakufa mapema kwani nivibaya mtu kushangaa mwenzake aliyepungukiwa maono akajikuta katumbukia shimoni mwa mafisadi.
 
Maneno haya ya mbunge mmmoja bunge lilopita yamenifanya nitafakari sana na kuona yalikuwa na maana sana kuwa "kwa watanzania wengi ukisema amani wanafikiri unazungumzia kinyume cha vita" kumbe siyo- Amani ni pamoja na kushiriki katika maendeleo yako na kupata stahili yako katika keki yetu ya taifa siyo wengine kuishi kama wako peponi na wengine wanona kuzimu hapa hapa duniani kwa maisha wanayoishi. Ikatoneshwa na maneno ya Mh Mkullo waziri wa fedha kuwa "Kila mtu atakula kwa jasho lake" … haya yote yanakuambia nini wewe Mtanzania?
 
Back
Top Bottom