watu 32 wanashikiliwa wakihusishwa na mauaji ya mwandishi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Walikua njiani wakielekea mbeya wakitokea kwenye vurugu Iringa.
hayo yameelezwa na Adivera Senso msemaji wa jeshi la polisi.
source ni bbc.
 
hivi polisi kweli wana akili au wanaota yaani polisi anafatua bomu mbele ya michael Kamhanda RPC mwenye sifa ya uaaji nchini Tanzania sawa na Selemani KOva halafu wanataka kuficha ukweli kwa kusingizia watu wengine kwenye nchii hii inaongozwa na kichaa na BBC siku hizi imepoteza credibirity tangu Tido aondoke limekuwa chaka la propaganda la chama cha mabwepande
 
Walikua njiani wakielekea mbeya wakitokea kwenye vurugu Iringa.
hayo yameelezwa na Adivera Senso msemaji wa jeshi la polisi.
source ni bbc.
Hapo kwenye bold sijaelewa kidogo!!!Unamaanisha hao watu walienda Iringa kufanya vurugu!!???Funguka zaidi
 
hivi polisi kweli wana akili au wanaota yaani polisi anafatua bomu mbele ya michael Kamhanda RPC mwenye sifa ya uaaji nchini Tanzania sawa na Selemani KOva halafu wanataka kuficha ukweli kwa kusingizia watu wengine kwenye nchii hii inaongozwa na kichaa na BBC siku hizi imepoteza credibirity tangu Tido aondoke limekuwa chaka la propaganda la chama cha mabwepande

Hapo wana counter CNN but Aljazeera please toeni maana ninawaaminia mno kwa duniani.
 
Walikua njiani wakielekea mbeya wakitokea kwenye vurugu Iringa.
hayo yameelezwa na Adivera Senso msemaji wa jeshi la polisi.
source ni bbc. Hapo polisi wamechemka kwani waliua ni polisi na sio raia wema
 
...Duh! Yale yale!! Kama yaliyotokea kule South Africa ambapo miners walifunguliwa mashtaka kwa mauaji yaliyofanywa na polisi...lakini baada ya Wananchi kuja juu mashtaka hayo dhidi ya miners yamefutwa. Sheria Tanzania kwa kweli zinatia kichefuchefu cha hali ya juu. Ushahidi wa picha unaonyesha kabisa wahusika wa mauaji yale lakini polisi inataka kuwabambikia kesi Watanzania ambao hawakuhusika kabisa na mauaji ya Mwangosi....Na Serikali hii dhalimu iko kimyaaa kuhusu uonevu wa hali ya juu unaofanywa dhidi ya hawa Watanzania wenzetu 32.
 
Hata Kova alituambia wamemkamata aliyemteka Dr. Ulimboka. Wauaji wao, wachunguzi wao
 
hawa wasasaivi 32 watakuwa wamalawi! watadai kuwa huyu mwaandishi wa habari ndo anaechangia mzozo wa mpaka! mtasikia tu, nyie ngojeni! mana hawana akili hawa polisi, alafu wanafikiri watu weupe wanaakili chafu kama zao, mpaka wanaanza tunga uongo!UN ndo wajionee sasa mana waliambiwa ya dr uli, wakawa wanauza sura tu
 
Na hao jamaa 32 wakishafikishwa mahakamani itakuwa si ruksa kulizungumzia swala hili. Sasa na sisi tukikubali hata kwa jambo lililo wazi hivi, basi tatizo litakuwa ni sisi wenyewe. Tunaomba wanahabari mtuongoze katika kulipigia kelele hili na kuwawajibisha wahusika wote kwa kuhusika kwao ama nafasi zao. TUMECHOKA SASA
 
ndio tatizo la watendaji wengi wakuu wa polisi kuwa na elimu ya darasa la 7, wengi wa maofisa wa polisi ninawafahamu walipata kazi kwa kigezo cha urefu.
 
wanataka kusema polisi hawahusiki, kweli serikali watanganyika imetugeuza mazezeta.!
 
Naomba kuuliza swali kwanza kabla ya kuchangia mada. Waliokamatwa ni kwa kosa la mauaji au kosa la kufanya mkutano bila ruhusa ya polisi?
 
Back
Top Bottom