Watu 18 wauawa katika mapigano mapya Somalia

bakuza

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
490
100
Watu 18 wauawa katika mapigano mapya Somalia
Mogadisho091.bmp
Watu 18 wameawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mapigano mapya yaliyotokea kusini magharibi mwa Somalia.
Mwandishi wa Radio Tehran ameripoti kuwa, mapigano yaliyotokea kati ya wanamgambo wa ash Shabab na wanajeshi wa Somalia na Kenya yamepelekea kuuawa watu 18 na wengine kadhaa kujeruhiwa katika eneo la mpakani la Gedo la kusini magharibi mwa Somalia.
Habari hizo zinaongeza kuwa, ndege za kivita za Kenya zikisaidiana na wanajeshi wengine wa nchi hiyo, zinaendelea kushambulia maeneo ya katikati mwa mji huo.
Mmoja wa wakazi wa mji wa Gedo amesema kuwa, mashambulio hayo ya ndege za kivita za Kenya yamewalazimisha wanamgambo wa ash Shabab kurudi nyuma na kukimbilia kwenye vijiji vya pambizoni mwa mji huo.
Watu walioshuhudia wamesema kuwa, wengi wa waliouawa katika mapigano hayo ni wanamgambo wa ash Shabab.
 
Back
Top Bottom