Watoto!!

Hahahaah!Sasa nikuite nani kufikisha heshima?Mzee DC?Japo haina utamu kama babu naweza nikazoea taratibu kama ndilo unalotaka!Nwyz hapo kwenye kipimo na umri ndo wengi wanapokosea!Mtu anamwadhibu mtoto utadhani kakutana na terrorist mtu mzima mwenzake.Mwisho mtu anaishia kumharibu mtoto kwa kumfanya sugu na kumfanya aamini anastahili kunyanyaswa!Inaua moyo hata kama mtu bado anatembea!
 
Umenikumbusha yule mama aliyemchoma na moto mtoto wake kisa kaiba shilingi 200. Jamani huo si ni unyama, kwani angemchapa viboko viwili vya nguvu si ingekuwa bora!!!! Jamani watoto wanahaki ya kupendwa na kuthaminiwa hata kama siyo wa kwako
 
Kuna watu wengine wana roho sijui za namna gani, mtoto mdogo anateswa kama nini vile!
 
Nimeona mambo mengi ila mengine ni aibu hata kuyasema ilihali wale wanayoyafanya wanaona ni sawa na kawaida tu God forbid

Watu wanafanyiana kicheni pati wajue jinsi ya kulea mume wanasahau watoto.Inabidi sasa ianzishwe sebuleni pati sijui!But seriously...kungekua na semina za kuelimisha watu athari za unyanyasaji wa watoto ingesaidia kwa kiasi fulani!
 
Ni kweli ila tatizo ni kwamba watu hatusomi vitabu na pia hatutaki kujifunza kutokana uzoefu. Kuna vitabu vingi sana vinaeleza jinsi ya ku-deal na watoto wa umri tofauti. Pia kuna suala la migongano kwenye ndoa pale anapopatikana mtoto wa kwanza. Inabidi tujitahidi kujisomea pia.
 
Kila siku tunaongelea mapenzi tunasahau watoto....embu leo tuwe kifamilia zaidi.

Leo kuna kipindi nlikua naangalia kikanisikitisha sana.Kuna mwanamke yeye anamwadhibu mtoto wake kwa kumnywesha pilipili na kumuogesha maji baridi kabisa...wakati mwingine eti anamlisha sabuni.

Nikakumbuka wakati nakua kuna mtoto wa jirani yetu yeye alikua naishi na babu yake, siku moja aliachwa nyumbani alafu akaenda kucheza....babu yake alivyorudi alichofanya ni kumchapa alafu akamweka kwenye gunia lenye yale majani yanayowasha alafu akamtundika wakati chini moto unawaka.Yule mtoto alitoka mwekundu kama nini sijui....sikumbuki kama kuna jirani aliyethubutu kumkemea yule mzee.Nyingine tuliwahi kua na msichana wa kazi ambae alikua na mtoto wa zaidi ya mwaka mmoja.....ilikua tukiwa shule yule dada anamfunga mtoto wake kwenye mguu wa kitanda ili eti asimsumbue.Yule mtoto analia na kukojoa pale pale mpaka analala...tukirudi basi tunakakuta kamelala uvunguni.Anagombezwaaa ila tukiwa hatupo tu anafanya vile vile.
Bila kusahau wale watu wanaoishi na watoto wa wenzao pamoja na wa kwao alafu wanawatreat fofauti.Kuna baadhi ya ndugu zangu nimewahi kuishi nao wa aina hiyo.....unakuta wale watoto wasio na mtu wa kumlilia wananyanyaswa ila wale wakwao na wale wenye ndugu au wazazi wao wenye uwezo wanalelewa vizuri tu.
Na yule aliyevutwa nyusi na mwalimu mpaka macho yakageuka!!

Kusema kweli hizi hali zote zinasikitisha.Kuona mtu mzima anamnyanyasa mtoto kwa sababu yoyote ile na kwa kisingizo chochote kile haifai.Wengi wao hawana wa kumlilia na kushtaki sio kitu ambacho kinaweza kufanyika kirahisi kwasababu kitendo cha kumpeleka mzazi au ndugu anaekulea kwenye vyombo vya sheria mara nyingi itaongeza matatizo zaidi ya kupunguza..

Naomba niwaombeni wanajamii tuwe na huruma jamani.Awe mtoto wako...wa ndugu au jirani jaribu kutokua mnyanyasaji.Kama mzazi kua na ukaribu na mwanao ili hata kama kuna mtu mwingine anaemnyanyasa iwe shuleni, mtaani au nyumbani iwe rahisi kukwambia.Na kwa wale ambao wanaishi na watu ambao sio wazazi halisi wa wanao (mama na baba wa kambo) kua na tabia ya kuongea na mwanao kujua mambo yanayoendelea nyumbani ukiwa haupo.
Mateso ya utotoni hua yanaacha makovu mabaya sana....JALI NA KUA NA HURUMA huo ndo ubinadamu!

Lizy umeniudhi sana! basi tu sina chakukufanya! Mada ni nzuri sana lakini umeisemea kama wewe unapenda hao watoto wateseke! Umesema wanaotesa watoto (wazazi wakipelekwa mbele ya sheria ni kuongeza matatizo?) Kwa hiyo wewe unafikiri ulivyoshauri hapa jamvini ndo taarifa zimewafikia walengwa?? hujui wanaoteseka wako kijijini au mijini ambao hawajui hata maana ya jamii forums hata ukimwambia internet anakwambia umenitukana!!! Una kitu serious sana ambacho mtu akisoma tu anapandwa na uchungu hapa ni kutafuta njia ya kuwasaidia hawa watoto! Tukisema kila mtu aweke story moja ya hivyo hapa jamvin mpaka utalia machozi! mimi umenihukiza kwa sababu ya lugha ya upoleeeeeee wakati unazungumzia kifo! Sasa basi mimi nimekasirika naanzisha kampuni ya kusaidia hawa watoto! ngoja sasa:embarassed2:
 
Sipiyu tatizo sio wanachofanya au wanachosema ila ni adhabu tunazowapa!Kuna picha nimeona jana mtoto ameungua matakoni kwa kukalishwa kwenye jiko la mkaa!Hata kama huyo mtoto angekua ameua bado hastahili adhabu ya aina hiyo!Besides..mtu kama huyo aliyekutwa akiandika mambo ya kimapenzi alitakiwa kukalishwa chini akaelezwa kosa lake lilipo bila kusahau uwepo wa mzazi wake pale.Kuna mwl aliwahi kumchapa mwanafunzi mpaka mkono ukachanika..japo sikumbuki kosa lake ila nna uhakika halikua kubwa!

Dada Lizzy, yote hayo unayosema ni sawa lakin tunapaswa kugeuza shilingi upande wa pili kuhusu hao watoto hasa wa siku hizi.

Sikubalian na adhabu za kuumiza au kudhuru watoto kimwili au kiakili iwe kwa kosa lolote, lakin kwa upande mwingine wa hao watoto pia lazima uangaliwe. Juzi hapa tumeripotiwa habari ya mtoto kuua mama ake mzazi kwa sababu kaificha ipod yake.

Tunapaswa kuwalinda watoto kwa pande zote, wasifanyiwe uovu, wasidanganywe na pia wasifanye uovu na wasidanganye
 
Kusema ukweli inasikitisha!
pale unapoona watoto wakinyanyasika,haijalishi ni wako ama si wako
ni unyama wa hali ya juu..yani Lizzy umenikumbusha yule wa nyusi uwiii nimesisimuka
kuna watu wana roho za ajabu.
watoto malaika wa Mungu jamani watu wanashindwa kufahamu hilo
wanahitaji mapenzi kutoka kwa watu wote wanaowazunguka
Nakumbuka kuna haus gal alikuwa akininyima chakula mimi na kaka yangu nikiwa na umri wa miaka mitano afu akiona mida ya baba na mama kurudi anatupa pipi na kutwambia tusiseme..siku tukisema kehso yake tutafinywaa na kunyimwa tena chakula..
si vizuri jamani, na mwanangu pia wakati hata hajaanza kukaa msichana wa kazi anamkalisha mtoto kwa uchungu shingo inainama huku akilia ye anamwambia msichana mwenzake 'kanadeka sana haka katoto kaende huko kwanza si uchungu wangu''..huyo mwingine alivyonihadithi.siku hiyohiyo alifunga virangi ila nililia sana..
jamani jamani tuendako sio..sasa jiulize wa namna hii wako wangapi.
Nimesoma hii sredi nimetokwa na machozi yametoka..duh!
 
Lizy umeniudhi sana! basi tu sina chakukufanya! Mada ni nzuri sana lakini umeisemea kama wewe unapenda hao watoto wateseke! Umesema wanaotesa watoto (wazazi wakipelekwa mbele ya sheria ni kuongeza matatizo?) Kwa hiyo wewe unafikiri ulivyoshauri hapa jamvini ndo taarifa zimewafikia walengwa?? hujui wanaoteseka wako kijijini au mijini ambao hawajui hata maana ya jamii forums hata ukimwambia internet anakwambia umenitukana!!! Una kitu serious sana ambacho mtu akisoma tu anapandwa na uchungu hapa ni kutafuta njia ya kuwasaidia hawa watoto! Tukisema kila mtu aweke story moja ya hivyo hapa jamvin mpaka utalia machozi! mimi umenihukiza kwa sababu ya lugha ya upoleeeeeee wakati unazungumzia kifo! Sasa basi mimi nimekasirika naanzisha kampuni ya kusaidia hawa watoto! ngoja sasa:embarassed2:

Mkuu pole sana
Nadhani bibie hajaweza ku-cover kila sehemu ya hii topic ya watoto kutokana na makosa yake ya kibinadamu au wakati anaandaa hii issue hakuweza kuangalia na watoto wa vijijini.
Mimi binafsi mpaka nafika hapa naona ni bahati sana. Kwa makuzi niliyokulia na vipigo nilivyopata kila siku ya utoto wangu, naona nilistahili kuwa kichaa kama sio mwendawazimu.
Binafsi sijavutiwa na namna hii topic kama topic ilivyoelezwa hasa ikizungumzia matatizo ya malezi kwa watoto lakin sina ulazima wa kuiona mbaya maadamu imeelezea sehemu ya matatizo kwa watoto, japo sio yote. Ina mwelekeo mzuri hata hivyo
 
Ni kweli ila tatizo ni kwamba watu hatusomi vitabu na pia hatutaki kujifunza kutokana uzoefu. Kuna vitabu vingi sana vinaeleza jinsi ya ku-deal na watoto wa umri tofauti. Pia kuna suala la migongano kwenye ndoa pale anapopatikana mtoto wa kwanza. Inabidi tujitahidi kujisomea pia.
Meja ni wachache sana kwenye jamii yetu wanaoweza kukaa chini na kusoma kitabu kuhusu watoto!Baba yuko baa..mama yuko bize hata muda hana!
 
Mazunguse ndugu yangu amini nikikwambia kwamba ningefurahi sana hawa watu wangeadhibiwa!Ila kutokana na nnayoyajua siwezi kusema kwamba sheria itakua suluhisho kwa wote maana Tanzania bado hatujabobea kwenye swala zima la kujali watoto.Kama hao ndugu zangu wangeenda kushitaki huo ungekua mwisho wa msaada waliokua wanapewa.Wangeenda wapi?Mtaani kungewafaa zaidi ehh?Inabidi ufikirie faida na hasara kwa hao watoto baada ya kushtaki!
 
CPU kama umefuatilia muendelezo wa thread utaona maongezi yangu na DC kuhusu kuwarekebisha watoto..nikaongelea ni jinsi mimi binafsi nilivyonyooshwa.Tambua kwanza kilicho ni-inspire kuandika hii thread ni manyanyaso kwa watoto.Kuwarekebisha ni kitu kinachojitegemea na kama ikibidi itakuja kivyake vyake.
 
Kwako tena CPU pole na samahani kwa kutoweza kukuridhisha kwa topic.Ila hii nia yake ilikua kuangalia mabaya kwa upande wa wazazi...ningeunganisha na ya watoto mngeishia kuniambia nipunguze paragraph!Kwa sababu sahihi na wakati maalumu labda ntageuza upande!Siwezi kua nazo zote at once.Alafu hiyo mifano yangu niliipatia kijijini!Usidhani maisha ya kijijini siyajui...miaka saba sio midogo kwahiyo jua nimeona mengi ya kule.
 
SweetDada pole mara mbili.Wadada wa kazi nao ni wakuwaangalia sana.Kumwachia mtoto mdogo inabidi mwanzoni uwe na tabia ya kushtukiza uwepo wako kama hauna mtu mwingine nyumbani!Sisi tulilazwa na njaa siku moja mama alikua msibani kisa yule dada alikua hataki kuwasha jiko la mkaa..umeme umekatika na mafuta ya taa hakwenda kununua mchana!Tulisema akaonywa hakudhubutu tena.Nwyz jaribu kua namwanao karibu na uwe unamkagua usikute anafinywa na kupigwa ukiwa haupo!
 
Well ni shida ya familia nyingi za kikwetu kuwabagua watoto wasiokuwa wa familia ile; mie nilikuwa likizo napita kwa ndugu yangua ambaye alikuwa na watoto wa umri wangu; basi jioni akirudi na zawadi aaingaia nazo chumbani na wanawe wanagawiwa huko na kama ni matunda utaambulia kuona maganda yakitoka chumbani.........na kuna wakati nilikuwa nazuiwa likizo nyingine nisiende hapo kwani hakuna nafasi.......
 
Ukweli ni kwamba familia nyingi zinapata watoto bila utayari wa kuelea hao viumbe......
Hongera Lizzy...using ya head rightly
 
Sasa mtu kama humtaki mtoto wa mtu kwako unamkubali wa nini??Bora hivyo walivyokua wanasema kumejaa kuliko kuwachukua na kuanzisha matabaka ndani ya familia.Ni ubinafsi tu unaotusumbua maana ukifikiria kama angeongeza machungwa au maembe mawili wote mkapata angepungukiwa nini???Kuna vitu kama nguo ambavyo ni ghali kidogo hivyo mtu unaweza kuelewa.Ila matunda....dah kweli binadamu tumeumbwa tukaumbika!!!
 
Ukweli ni kwamba familia nyingi zinapata watoto bila utayari wa kuelea hao viumbe......
Hongera Lizzy...using ya head rightly

Asante St.RR!1:lol:

Hapo napo ndo maana mara nyingi nikimuona mtu na kundi kubwa la watoto ambao wote ni wake hua nakasirika sana utadhani inanihusu.Maana mtu hajui kesho itakuaje matokeo yake anampelekea mtu mwingine mzigo wa watoto matokeo yake wanaishia kunyanyasika.Angalau kamoja au wawili hata mambo yasipoenda sawa bado wanaweza kua manageable kwa kiasi kikubwa kuliko watano na kuendelea.

Ila ndo hivyo tena wengine ni wale wanaokutana na ndugu ambao hata kama mali ziliachwa nawachukua wao.Inasikitisha sana kwakweli.
 
Kila siku tunaongelea mapenzi tunasahau watoto....embu leo tuwe kifamilia zaidi.

Leo kuna kipindi nlikua naangalia kikanisikitisha sana.Kuna mwanamke yeye anamwadhibu mtoto wake kwa kumnywesha pilipili na kumuogesha maji baridi kabisa...wakati mwingine eti anamlisha sabuni.

Nikakumbuka wakati nakua kuna mtoto wa jirani yetu yeye alikua naishi na babu yake, siku moja aliachwa nyumbani alafu akaenda kucheza....babu yake alivyorudi alichofanya ni kumchapa alafu akamweka kwenye gunia lenye yale majani yanayowasha alafu akamtundika wakati chini moto unawaka.Yule mtoto alitoka mwekundu kama nini sijui....sikumbuki kama kuna jirani aliyethubutu kumkemea yule mzee.Nyingine tuliwahi kua na msichana wa kazi ambae alikua na mtoto wa zaidi ya mwaka mmoja.....ilikua tukiwa shule yule dada anamfunga mtoto wake kwenye mguu wa kitanda ili eti asimsumbue.Yule mtoto analia na kukojoa pale pale mpaka analala...tukirudi basi tunakakuta kamelala uvunguni.Anagombezwaaa ila tukiwa hatupo tu anafanya vile vile.
Bila kusahau wale watu wanaoishi na watoto wa wenzao pamoja na wa kwao alafu wanawatreat fofauti.Kuna baadhi ya ndugu zangu nimewahi kuishi nao wa aina hiyo.....unakuta wale watoto wasio na mtu wa kumlilia wananyanyaswa ila wale wakwao na wale wenye ndugu au wazazi wao wenye uwezo wanalelewa vizuri tu.
Na yule aliyevutwa nyusi na mwalimu mpaka macho yakageuka!!

Kusema kweli hizi hali zote zinasikitisha.Kuona mtu mzima anamnyanyasa mtoto kwa sababu yoyote ile na kwa kisingizo chochote kile haifai.Wengi wao hawana wa kumlilia na kushtaki sio kitu ambacho kinaweza kufanyika kirahisi kwasababu kitendo cha kumpeleka mzazi au ndugu anaekulea kwenye vyombo vya sheria mara nyingi itaongeza matatizo zaidi ya kupunguza..

Naomba niwaombeni wanajamii tuwe na huruma jamani.Awe mtoto wako...wa ndugu au jirani jaribu kutokua mnyanyasaji.Kama mzazi kua na ukaribu na mwanao ili hata kama kuna mtu mwingine anaemnyanyasa iwe shuleni, mtaani au nyumbani iwe rahisi kukwambia.Na kwa wale ambao wanaishi na watu ambao sio wazazi halisi wa wanao (mama na baba wa kambo) kua na tabia ya kuongea na mwanao kujua mambo yanayoendelea nyumbani ukiwa haupo.
Mateso ya utotoni hua yanaacha makovu mabaya sana....JALI NA KUA NA HURUMA huo ndo ubinadamu!

Akina dada/mama wa humu mtanisamehe kama nitakosea. Kila linapotokea teso la kutisha kwa mtoto lazima jinsia ya ke inahusika. Na wengi ni wale ambao wameshazaa. Huwa naambiwa uchungu wa mwana aujuae mzazi, je mwanao ni yule wa kumzaa tu, wengine wote wakubwa wenzzio.
Nafikiri pamoja na kuwa na harakati za haki sawa muambizane pia juu ya adhabu stahiki, siyo ya kukomoana.
 
Back
Top Bottom