Watoto waletwa kujaza viti Karimjee Hall-Katiba

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,923
Nimeona kwenye taarifa ya habari ya habari ya saa 2 ITV kuwa watoto wengi waliletwa kuanzia asubuhi saa 11 ili kujaza viti. TV imeonyesha watoto wakiwa wamelala na fujo kuzuka baada ya watu kuhoji jambo hilo. Ilibidi polisi waingilie.

Imezidi kuelezwa kuwa watoto hao walikuwa wakipiga kelele na kuzomea sana pale watu walipokuwa wakitoa maoni yao dhidi ya mswada huo.

Inaelekea kuwa kuna watu ambao wako tayari kufanya lolote ili mswada huo upite kama ulivyo bila kupingwa.

Tutafika kweli?
 
Unashangaa nini? Si Tambuu Hasa alitangaza kwamba leo ccm italeta wafuasi wao kwa sababu Chadema jana walileta wao.

Mikutano ya ccm na ya JK huudhuriwa na umati wa rika gani?
 
Nimeona kwenye taarifa ya habari ya habari ya saa 2 ITV kuwa watoto wengi waliletwa kuanzia asubuhi saa 11 ili kujaza viti. TV imeonyesha watoto wakiwa wamelala na fujo kuzuka baada ya watu kuhoji jambo hilo. Ilibidi polisi waingilie.

Imezidi kuelezwa kuwa watoto hao walikuwa wakipiga kelele na kuzomea sana pale watu walipokuwa wakitoa maoni yao dhidi ya mswada huo.

Inaelekea kuwa kuna watu ambao wako tayari kufanya lolote ili mswada huo upite kama ulivyo bila kupingwa.

Tutafika kweli?

kwa style hii hatutafika, ni jambo la aibu sana! hivi kuna upunguani kiasi gani kwa serikali yetu?! yaani hata hao polisi hawakuweza kuwatoa hao watoto kwani ni wazi walikuwa wamesinzia kwenye mabenchi n wengine waliamua utoka nje baada ya kuchoka kwa yale yaliokuwa yakiendelea kwa vile yalikuwa hayawahusu! watoto hao wanakadriwa kuwa kati ya umri wa miaka 11 na kumi na 14!

jana nilipata shida sana kulala kutokana na zile vurugu za tegeta, dodoma na karimjee, ni wazi kwamba tunakoelekea ni kubaya mno na serikali haina habari na hilo na sidhani kama wanajua cha kufanya (cause if they knew the would have protected all these). u wapi usalama wa taifa wenye kunia mema na taifa hili?!

hivi ni nani sasa ambaye anaweza kutoa mwongozo juu ya hili taifa tuepuke huko kubaya tunakoelekea?!
 
Ndiyo maana naipenda Tz?

Si mliona baada ya Babu Loliondo kusema kaoteshwa na Mungu kesho yake na wengine wakaoteshwa....!

Jana wamezomewa na sasa wamejibu mapigoooooooo!

TAMBUENI HAYA YA KATIBA NI MCHEZO, ILA USIPOCHEZWA VIZURI HATA WALE WANAODHANI WATASHINDA WANAWEZA KUSHANGAA MATOKEO.....!
 
wametolewa shule gani japo wanapaswa nao kutoa maoni kama watoto lakini kufundishwa kuzomea,nchi ndio imeshavurugika patamu hapo, nahofia kukatwa panga kabla sijaona daraha la kifamboni ebo labda nitaiona Kigoma ikiwa Dubai
 
Kitendawili! Akiwa CUF kule Temeke alikuwa akikusanya vibaka mtaani na viroba vya mawe ktk pick up yake kuwapiga CCM, leo yuko CCM anakusanya watoto wadogo wajaze viti ili watu wenye akili zao wasipate nafasi ya kukaa na kushiriki suala muhimu la kujadili hatma ya Taifa lao, na hata hao wachache watakao bahatika kuingia ndani na kuchangia mada basi wazomewe.
 
na Dodoma unaambiwa walikuwa 30 ilivyofika kwenye saa tano wakabaki 15 wananchi wamewaachia watowe maoni wenyewe baada yakuwavurumishia mabomu ha ha ha CCM kwisha
 
Hapa ni kaaaazi kweli kweli.....hakika nchie yetu tamu na nzuri ajabu ya Tanzania inakwenda pabaya tena pabaya sana. Mungu aturehemu na tusalini sana
 
CCM wameishiwa mbinu mpaka wanaleta watoto saa 11 asbh. Hii ni dalili ya cham kufa!
 
Yaani suala nyeti la katiba,limegeuka mchezo wa kitoto...this is hard to comprehend! May God help us
 
Kweli CCM mishipa yao ya aibu imeshaoza haifanyi kazi kabisa, yaani watu wazima wanatoa mawazo ambayo ukiyasikia unabaki kushangaa tu, eti ndio viongozi wetu, yaani tunataka kuunda katiba mpya, halafu huyo aliyesababisha tutake kuunda katiba mpya (kwa kuchakachua kwake) eti ndio atupangie hizo hadidu za rejea, hii ni akili au matope, sasa kuna sababu gani ya kujadili kitu ambacho matokeo yake tunayajua. Rais ambaye wote tumeuona uwezo wake wa kufikiri ndio atupangie nini cha kuweka kwenye katiba.

Shauri yenu CCM Gbagbo mwenzenu siku hizi anaishi shimoni kama nyoka, au hamsikilizi habari.

'A FOOL LEARNS FROM HIS OWN MISTAKES, A WISE MAN LEARNS FROM OTHER PEOPLES MISTAKES'

Baadaye, nakwenda kwa wakubwa. politiki siwezi.
 
Kweli CCM mishipa yao ya aibu imeshaoza haifanyi kazi kabisa, yaani watu wazima wanatoa mawazo ambayo ukiyasikia unabaki kushangaa tu, eti ndio viongozi wetu, yaani tunataka kuunda katiba mpya, halafu huyo aliyesababisha tutake kuunda katiba mpya (kwa kuchakachua kwake) eti ndio atupangie hizo hadidu za rejea, hii ni akili au matope, sasa kuna sababu gani ya kujadili kitu ambacho matokeo yake tunayajua. Rais ambaye wote tumeuona uwezo wake wa kufikiri ndio atupangie nini cha kuweka kwenye katiba.

Shauri yenu CCM Gbagbo mwenzenu siku hizi anaishi shimoni kama nyoka, au hamsikilizi habari.

'A FOOL LEARNS FROM HIS OWN MISTAKES, A WISE MAN LEARNS FROM OTHER PEOPLE'S MISTAKES'

Baadaye, nakwenda kwa wakubwa. politiki siwezi.
 
jana nilipata shida sana kulala kutokana na zile vurugu za tegeta, dodoma na karimjee, ni wazi kwamba tunakoelekea ni kubaya mno na serikali haina habari na hilo na sidhani kama wanajua cha kufanya (cause if they knew the would have protected all these). u wapi usalama wa taifa wenye kunia mema na taifa hili?!

Unawatafuta? Wamelala fofofo wanagawana wanawake na wanaume. Akili zao kama za watawala wao!
 
Back
Top Bottom