Watoto wafanyiwa unyama gerezani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Fidelis Butahe
WATOTO wenye umri chini ya miaka 18 wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali au waliohukumiwa huwekwa sehemu moja na watu wazima katika Gereza la Segerea, Dar es Salaam na baadhi yao kuingiliwa kinyume na maumbile na kuharibiwa vibaya.


Tuhuma hizo nzito dhidi ya magereza zilibainika wakati Kamati ndogo ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi, ilipokuwa ikiwasilisha kwa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kile ilichokiona katika gereza hilo baada ya kufanya ziara.


Kamati hiyo ilitoa taarifa yake katika kikao kilichofanyika Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam wiki iliyopita ambacho pia kilihudhuriwa na maofisa mbalimbali wa Jeshi la Magereza akiwemo Kamishna wake Mkuu, Augustino Nanyaro.


Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kuwa Kamati hiyo ya Ukimwi ilieleza kwamba watoto chini ya miaka 18 wanaofika katika gereza hilo kwa makosa mbalimbali, utambulisho wao huonyesha kuwa wana miaka 19 hadi 20.


Taarifa hizo zilidai kwamba watoto hao ambao hukaa na wakubwa mchana, usiku huhamishiwa sehemu nyingine na kuingiliwa kinyume na maumbile kutokana na mazingira yalivyo ya kukosa pa kukimbilia.


“Waligundua mengi sana, walisema kuwa watoto hao wengi wameharibika sehemu zao za siri. Kutokana na hali hiyo wanaowafanyia vitendo hivyo huwatumia pia kuingiza simu, sigara, bangi na dawa za kulevya gerezani. Wanaingiza vitu hivyo kwa kutumia sehemu zao za siri zilizoharibiwa,” kilisema chanzo cha habari kutoka kamati hiyo na kuongeza:


“Unajua huwa wameharibika kwa hiyo sehemu zao huwa wazi na kubwa kiasi kwamba ni rahisi kuficha simu, bangi, sigara na dawa za kulevya bila kujulikana.”


Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Rosweeter Kasikila alipoulizwa jana kuhusu tuhuma hizo alisema katika kikao hicho walipendekeza wakubwa kutengwa na watoto na kushauri upelelezi wa kesi kufanywa mapema ili kupunguza msongamano wa watuhumiwa.


“Hali siyo nzuri yaani sehemu ya kuwekwa watu 40 wanawekwa watu 180. Jambo ambalo hatukulipenda ni jinsi watoto walivyokuwa wakiwekwa sehemu moja na watu wazima kwa sababu hujifunza mambo mengi ambayo si mazuri kwa umri wao” alisema Kasikila.


Alisema kitendo cha watoto kukaa sehemu moja na watu wazima ndicho kinachosababisha hata kufanyiwa vitendo vichafu ikiwa ni pamoja na kuingiliwa kinyume na maumbile.“Tulieleza wazi kwamba watoto wanatakiwa kutengewa sehemu yao kwa sababu wakiwa wao wenyewe si rahisi kufanyiwa vitendo hivyo,” alisema Kasikila.


Kwa mujibu wa chanzo chetu, katika kikao hicho maofisa wa magereza walipoulizwa kuhusu umri wa watoto hao walisema jambo hilo lipo ila hushindwa kufanya lolote kwa kuwa vielelezo vinavyoletwa huonyesha kuwa umri wao umezidi miaka 18.


Habari zaidi zilieleza kwamba maofisa hao walisema hali hiyo inatokana na mfumo uliopo na kwamba unatakiwa kufanyiwa kazi.


Naibu Kamishna wa Magereza, Fidelis Mboya alipoulizwa kuhusu hali hiyo, licha ya kukiri, alisema asingependa kueleza kwa undani mpaka apelekewe maswali kwa maandishi.


“Nitumie maswali kwa maandishi ili na mimi nijibu kwa maandishi, hili jambo ni ‘very sensitive’ (nyeti sana), lete maswali nitakujibu kwa maslahi ya taifa,” alisema Mboya.


Matukio ya utata wa umri
Suala la umri wa watuhumiwa na hata wafungwa limekuwa gumzo katika siku za hivi karibuni baada ya mawakili wa mwigizaji wa filamu, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba, kuwasilisha ombi lao Mahakama Kuu ikitaka iamuru kesi ya msanii huyo isikilizwe katika mahakama za watoto kwa madai kuwa mteja wao bado ni mtoto.


Uamuzi huo ulikuja baada ya awali, kugonga mwamba katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Lakini, tayari katika Bkutano wa Bunge la Aprili 14, 2010 aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Mgeni Jadi Kadika wakati akiuliza swali alitaka kujua Serikali haioni kuwa kuna ulazima watoto kujengewa magereza yao au kuwekwa sehemu maalumu.


Alisema hilo linatakiwa kufanyika kwa kuwa watoto hao wanapokuwa gerezani hukutana na wafungwa wenye tabia mbalimbali kama wizi, ubakaji, ujambazi na kwamba watoto hao wanaweza kuiga tabia hizo.


Akijibu swali hilo aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Khamis Kagasheki alisema kwa mujibu wa Sheria zinazoratibu, kuongoza na kusimamia masuala ya mahabusu, wafungwa watoto wanapopelekwa magerezani wanapaswa kutenganishwa na wakubwa.


Kagasheki alinukuu Kanuni za Uendeshaji wa Jeshi la Magereza (The Prisons Standing Orders) ya 2003, Kifungu Namba 502, vifungu vidogo vya (ii) na (iii), wafungwa watoto wanapopelekwa magerezani wanatenganishwa na wafungwa wakubwa.

Watoto wafanyiwa unyama gerezani
 
Hivi yale magereza ya watoto watukutu kazi yake ni nini?

Kama lile lililoko kule mbeya.
 
Hivi yale magereza ya watoto watukutu kazi yake ni nini?

Kama lile lililoko kule mbeya.
Magerza hayo ya watoto watukutu yamewkwa kaa show hayatumiki labda tuwaulize Viongozi Wahusika wapate kutujibu Serikali hatuna Viongozi wetu ni majina matupu utendaji wa kazi haupo mkuu.. LEGE

Inasikitisha sana...
Hatuna Viongozi wenye huruma na wanachi wao ndio maana Seriakali inaendeshwa hivyo hivyo ujuavyo mwenye nguvu mpishe apite mkuu.. sweke34
 
Last edited by a moderator:
Hivi yale magereza ya watoto watukutu kazi yake ni nini?

Kama lile lililoko kule mbeya.
hii inaweza kuwa ni suluhisho la muda tu kwani kwenye watoto watukutu na sio watukutu kuna matatizo pia ya wale waliokubuhu na wale wasio kubuhu, sasa waliokubuhu watahamishia ubabe wao kwa hao wengine, jingine kuharibiwa kwa watoto kuna anzia na hawa watoto wa barabarani, waliotelekezwa na wazazi au na hali maisha ambapo wengi huanza kufanyiwa hivyo vitendo humo mabarabarani. sasa kutatua hili tatizo serikali inatakiwa ichukue hatu za muda mfupi na za muda mrefu, kwa mfano kwa sasa kambi nyingi za jeshi zipo tupu, kwanini serikali isiwapeleke watoto wa mitaani huko wakapata makazi na kuzalisha japo chakula chao cha kula, mabweni yapo ya kulala. hata watakapotoka huko wamekuwa na kujua kuzalisha. kuna wengine utasikia ametoroka nyumbani au amefukuzwa na ndugu asijue pa kwenda , akiishia mtaani ndio huko anajifunza tabia mbovu au anafanyiwa vitendo viovu.
watu wengi tanzania watoto kwa vijana wanapotea njia kwa sababu hatuwapi njia mbadala au matumaini ya kwenda mbele zaidi ya wao kuhangaika wenyewe.
 
Fidelis Butahe

"Waligundua mengi sana, walisema kuwa watoto hao wengi wameharibika sehemu zao za siri. Kutokana na hali hiyo wanaowafanyia vitendo hivyo huwatumia pia kuingiza simu, sigara, bangi na dawa za kulevya gerezani. Wanaingiza vitu hivyo kwa kutumia sehemu zao za siri zilizoharibiwa," kilisema chanzo cha habari kutoka kamati hiyo na kuongeza:


"Unajua huwa wameharibika kwa hiyo sehemu zao huwa wazi na kubwa kiasi kwamba ni rahisi kuficha simu, bangi, sigara na dawa za kulevya bila kujulikana.Watoto wafanyiwa unyama gerezani

Huu ni unyama wa hali ya juu sana.

Hivi huko Gerezani hakuna watu au Askari ambao wanalinda. Sasa wanalinda nini au nao wanashiriki katika kufanikisha vitendo hivi.

Na hao wanaofanya hivi vitendo huo majumbani kwao hawana watotot au wadogo zao wa umri huo???



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom