Watoto wa Wasira waliojiunga CHADEMA watoa ufafanuzi juu ya uhusiano wao na Waziri Wasira

Ingekuwa ni wewe ungeenda kulumbana na wanao vyombo vya habari? Angekaa kimpya habari hii ingeshakuwa historia sasa imezidi kuwajenga chadema na hao watoto pia
Habari imeandikwa kwenye vyombo vya habari ulitaka yeye akakanushie wapi kama si kwenye vyombo hivyo hivyo vya habari. Kama kuna chombo cha habari kiliandika "watoto ni wa Steven Wassira" kilikuwa sahihi?
 
Kwahio Mzee wasira anapigwa dongo jingine tena? hata siamini
 
Huyu Easter si ndo alishawahi kuimba Bongo flava ?

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Hoja hapa si kama watoto wa Kaka yake si wake, hoja hapa ni kwamba Baadhi ya vyombo vya habari vilitangaza na kuandika kwamba ni watoto wa Steven Wassira. Steven ana haki ya kuweka mambo sawa na wala hajawakana kama si watoto wa ukoo wao!!

HOJA si watoto wa nani, HOJA ni mabinti wawili LILIAN WASSIRA na ESTHER WASSIRA wamejiunga na CHADEMA baada ya kuona ndio chama kinachotoa matumaini kwa watanzania.
 
Kama ulitazama ITV siku ile ilielezwa wazi kabisa ni watoto wa ndugu yake waziri wasira,sasa sijui ilikuwaje yamekuwa mazito,labda siku hizi habari ni chache.

Hapana tuwe wazi na wa kweli... Nadhani tatizo sio habari tu, tatizo lipo kwa waandishi, wana CCM na wana CDM wenyewe.

Habari ya mabinti wawili kupata card mpya ya CDM alafu tena wamekabidhiwa hizo card na Slaa, unadhani itaacha kutengeneza headlines na hali ni wazi hivyo vyama pinzani kubwa?
 
Hongera sana liliani na ester kwa kujiunga na Chadema
,huo ndio ujasiri tunaohitaji ndani ya taifa hili.Mungu awabariki mfike mbali kisisasa.
 
kama umri wao unaruhusu kugombea ningeshauri mmoja wao agombee jimbo la steven wasira'yule mzee anatakiwa kupotea katika ulimwengu wa siasa

:biggrin1: na ndio itakavokua hivyo..sasa tuone ka mzee atakua tayari kuwapeleka mabwepande ndugu zake
 
Nafikiri wauza magazeti waliweka heading kwa kusudi wanalolijua. Sidhani kama watoto wanataka kusafiria nyota ya Wassira Steven maana huyu profession aliyokuwa nayo ni matusi, kejeli na ukigeugeu. Siasa za matope anazijua sana toka anapambana na Mzee Warioba hapo mwaka 1995. Moja ya kete alizotumia ilikuwa ni lugha ya matusi, dharau, kejeli na kila aina ya kiburi. Mahakama ilimwondolea ubunge kwa style yake na akabaki kuuza samaki pale ferry mpaka alipokumbuka kurudi kwenye chama kilichokuwa kimemtuma kufanya umamluki. Sasa kwenda public na kutoa maelezo ya kwamba hawa sio watoto wake wa kuzaa naona kajidhalilisha mno. Wawe wa kuzaa, wawe wa mjoma, wa shangazi, wa kaka, wa mdogo wake, watoto ni watoto na ni zawadi ya familia na ukoo. Alichopaswa kusema ilikuwa ni kumshukuru Mungu kwanba watoto tunawapa uwanja mpana kujiamulia na sio kukurupuka na kuongea wa jaziba na kuwawekea watu wengine maneno. Hakuna ambapo Dr.Slaa alisema hao ni watoto wa Steven. Kwa kifupi hakuna nyota ya kusafiri kwa Steven Wassira
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI KUHUSU SISI KUJIUNGA NA CHADEMA NA MALUMBANO KUHUSU MAJINA YETU


Tarehe 30/09/2012 mimi Esther Wasira na dada yangu Lilian Wasira tulijiunga na CHADEMA na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CHADEMA Mh. Dr Willibrod Slaa. Tulielezea kwa kirefu sababu za sisi kujiunga Chadema na tukasisitiza kuwa tumeridhika kuwa CHADEMA ni chama chenye dhamira safi ya kuiongoza Tanzania na kwamba ni chama kinacholeta matumaini mapya ya kuijenga Tanzania mpya yenye neema.

Waandishi wa habari walijaribu sana kutudodosa kujua tuna uhusiano gani na Waziri Steven Wasira. Tulielezea wazi kuwa mahusiano yetu ya kifamilia hayahusiki na sababu na dhamira yetu ya kujiunga CHADEMA. Hata hivyo tulielezea kuwa Waziri Steven Wasira ni baba yetu mdogo ambaye alinyang'anyana ziwa na baba yetu mzazi, wakili George Wasira. Tulidhani hiyo ilitosha na lisingekuwa swala tena la kujadili na badala yake hoja ya kujadiliwa ingeweza kuwa sababu tulizozieleza za kujiunga CHADEMA.

Tunasikitishwa sana na malumbano yaliyofuata baada ya hapo kuhusu kama sisi ni watoto wa Wasira au la. Kama tulivyoeleza, tumejiunga CHADEMA kwa sababu tulizozieleza hapo awali na wala si kwa sababu nyingine yeyote. Hatujajiunga CHADEMA kumdhalilisha mtu, kumfedhehesha mtu au kukipatia umaarufu CHADEMA kwa vile tu tunatumia jina la Wasira. CHADEMA ni chama cha siasa tena chenye wanachama na wafuasi wengi Tanzania hivyo si kashfa bali ni fahari kubwa mtu kujiunga CHADEMA na tena ni ushahidi wa mtu kujitambua. Pia CHADEMA ni Chama maarufu sana Tanzania kwa sasa hata pengine ni maarufu kuliko CCM hivyo hakihitaji kujipatia umaarufu kwa mgongo wetu. Sisi tunawaheshimu sana wazee wetu na tutaendelea kuwaheshimu ila linapokuja swala la chama cha kujiunga linabaki kuwa hiari yetu kwa kuzingatia sera za chama na uwezo wa chama husika katika kujenga Tanzania tunayoitaka na hilo ndilo lililotupeleka CHADEMA. Na hii ni haki yetu ya msingi kabisa inayolindwa na Katiba ya nchi hii chini ya ibara ya 20(1).

Ikumbukwe kuwa mmoja wa Waanzilishi wa CHADEMA ni Mzee Wasira. Dhamira ya kuanzisha CHADEMA ilikuwa ni kushika dola na hili ndilo CHADEMA imekuwa siku zote inajaribu kuwashawishi Watanzania kuwa sasa wamekomaa na wanastahili kuchukua dola. Kwa vile kuchukua dola ilikuwa ndio ndoto ya baba yetu mzazi Mwanzilishi wa CHADEMA, sisi kama watoto tumejiunga na M4C ya CHADEMA ili tuweze kutimiza ndoto ya baba yetu kuwa CHADEMA siku moja ichukue jukumu la kuiongoza Tanzania.


Kwa maelezo zaidi wasiliana na:

Lilian Wasira 0719 604156

Esther Wasira 0655 048797

Hongereni kwa maelezo ya kutosha kwani hayo maelezo yenu hayakuhitaji mtu yeyote aje ayajibu wala kukanusha
kipekee nimeshangaa mzee Wasira akijikanyaga eti kuwa akina Esther na mwenzake si watoto wangu bali ni watoto wa kaka yangu.Safi kwa uamuzi wenu mliouamua always AIM HIGHER@ M4C
 
Mzee Wasira huwa ana hulka ya ubabe nakujiona anajua sana kuliko mtu mwengine,huyu Mzee amelewa madaraka,
 
Haya ndio matatizo ya gutter politics... Katika haya mambo ya kisiasa msingi wa familia yoyote ni mshikamano hasa wakati wa kashfa mbali mbali ziwe za kweli ama uongo. Sielewi uhusiano wa hao mabinti na Waziri Wassira, ila ukweli utabaki lazima kutakuwa na kidoa kimeingia sababu tu ya baadhi ya waandishi waliandika habiri katika misingi ya ushabiki!

Imekuwa ni sifa kutaja watoto wa mkubwa fulani kajiunga CDM nadhani in a way kama kuonesha kuwa watoto hawawakubali wazazi wao na vyama vyao (mara nyingi kutoka CCM). Ile habari ya juzi kuhusu hao mabinti ilielezwa in the lines ya kuonesha Waziri Wassira kana kamba ni baba yao mzazi, kumbe NDIO ni ndugu lakini sio baba yao Mzazi.

Nam support Wassira kuliweka wazi kuwa wale sio wanawe na kwamba wa ndugu yake... ingawa kauli yake inaonesha wazi ni namna gani amekereka; na nawapongeza pia akina binti Wassira kuliweka hili wazi na kulipa ufafanuzi na kutowa upande wao wa shillingi. Haya mambo hayatakoma, yataendelea tu ili mradi ushabiki wa majina makubwa katika siasa yakiendelea kushobokewa... Mambo ya aibu basi tu.

Now you're talking......
Jana niliyaongea haya almanusura nitolewe macho
Hawa watoto ni wanasheria na nihaki yao kujiunga CDM lakini pia walipaswa kutumia akili kuepusha conflicts za ukoo kwa kutokubali kutumiwa kama mtaji wa kisiasa kwa kile kinaonekana kumdhihaki wasira
What is so special kwa wao kwenda makao makuu kupokewa na Slaa Huku wamezungukwa na media?
 
Now you're talking......
Jana niliyaongea haya almanusura nitolewe macho
Hawa watoto ni wanasheria na nihaki yao kujiunga CDM lakini pia walipaswa kutumia akili kuepusha conflicts za ukoo kwa kutokubali kutumiwa kama mtaji wa kisiasa kwa kile kinaonekana kumdhihaki wasira
What is so special kwa wao kwenda makao makuu kupokewa na Slaa Huku wamezungukwa na media?
Kwamba wanatumika kisiasa ni maoni yako tu lakini haikatazwi kupokea kadi na kuzungumza na media. Kwanza wao ni watoto wa mwasisi wa chadema na pia ni wanaharakati wa kike, vijana wasomi, hiyo ilitosha kuivuta media. Na inaonekana media ilikuwa karibu kwa kuwa walienda kumuuliza Dr Slaa kuhusu kushindwa umeya mwanza
 
Now you're talking......
Jana niliyaongea haya almanusura nitolewe macho Hawa watoto ni wanasheria na nihaki yao kujiunga CDM lakini pia walipaswa kutumia akili kuepusha conflicts za ukoo kwa kutokubali kutumiwa kama mtaji wa kisiasa kwa kile kinaonekana kumdhihaki wasira What is so special kwa wao kwenda makao makuu kupokewa na Slaa Huku wamezungukwa na media?

Haya mambo its all about timing... Weapon so lethal in politics hasa kama you have the rite moves... Dr. Slaa na wana CDM wanajua hilo na hata mabinti Wassira walijua hilo. Jina la Wassira is what carried weight to the news, hapo result ni kuwa tayari hawa dada wamejijengea jina Kisiasa kishabiki.... INASIKITISHA.

But believe me you hapo mmoja wao akiamua kugombea nafasi ya uongozi hata ya ubunge tayari wana full support ya Chama cha CDM na wanachama wao... Bila kujali kama kunaweza kuwa na possibility ya upandikizi, bila kujali kama wana uwezo huo wa kuongoza na bila kujali wana kuwa kuna wengine wanaweza kuliko hao. Yoote tu kwa ajili ya kukidhi kiu ya ushindi katika gutter politics ya ready made followers...
 
Anakasirika nini si kuna wakati alijiunga na NCCR anachoshangaa nini watoto wa ndugu yake kujiunga na CDM?
 
Back
Top Bottom