Set your course by the stars, not by the lights of every passing ship - Omar Bradley
Jamani tuwe makini, this is INFORMATION AGE. Kama ilivyokuwa wakati wa INDUSTRIAL AGE, kwa sasa information is power. Kama kuna malalamiko tujifunze kusikiliza na kufanya linalowezekana kuondoa shaka iliyoanza kujengeka miongoni mwa wanajamii.The best y'all can do is whine behind the backdrop of the internet. Waafrika Ndivyo Tulivyo.
Sasa hoja hii ina zaidi ya mwezi, mwanzishaji kimyaa. Anasubiri ijifie? Anasubiri iingie kwenye archive kisha aseme "Imefutwa kabisa"? Ni bora uendelee, none is moving this thread to anywhere. Be fair, kuandika kuwa utaamishwa kuwa-protect watoto wa wakubwa ni kutukosea tu moderators. Ni vema uendeleze mjadala. Mchangiaji akitukana basi ndipo hoja yake hufutwa, ama mwanzishaji akibadili mtizamo na kushauri hoja ifungwe itafungwa. Ama vinginevyo hoja ikijaa udaku bila data zaidi na kuwa mada ya salaam n.k basi hakika itahamishiwa kuleee...
Lete data, hakuna asiyeongeleka. Ila tuwe fair katika hoja. Kila mtanzania ana haki ya kuheshimiwa utu wake. Haijalishi kazaliwa na Mkapa, Nyerere, Malecela, Mbowe n.k. Ili mradi tusiwatukane na kuwachafulia majina kwa makusudi. Ukitoa hoja tarajia kupingwa ama kuungwa mkono, ni two way traffic.
Karibu GT
Hivi ktk nchi zilizoendelea hakuna upendeleo kweli?
Kwa uzoefu wangu mimi nimeuona upendeleo kila nchi niliyoishi na kila sehemu niliyofanyia kazi.....
Hivi ktk nchi zilizoendelea hakuna upendeleo kweli?
Kwa uzoefu wangu mimi nimeuona upendeleo kila nchi niliyoishi na kila sehemu niliyofanyia kazi.....
So? kwani hii ndio inahalalisha upendeleo (uhalifu)? Kwani siku hizi makosa mawili yanatengeneza kweli?
No! Haihalalishi upendeleo hata kidogo. Mimi binafsi naupinga upendeleo wa aina yoyote ile na kwa nguvu zangu zote alizonijalia Mnyazi Mungu. Pointi niliyokuwa natengeneza ni kwamba upendeleo ni moja ya hulka/ silka za binadamu, upo tokea enzi na enzi na utaendelea kuwepo no matter what. Pundit aka Mjuzi wa mambo alisema kwamba upendeleo ktk nchi zetu hizi za Kiafrika ndio unasababisha sisi Waafrika tuwe na hali tuliyonayo sasa. Ndio na mimi nikasema mbona hata kwenye nchi zilizoendelea upo lakini na bado wameendelea? Kuwepo kwa upendeleo kila sehemu ya dunia ni kithibitisho tosha kuwa hiyo ni asili yetu (sisi binadamu). Nimeeleweka?
Kwa mfano wapi (be specific) kuna upendeleo wa aina hii??
nafikiri ni mfano sahihi kwa sababu anayeweza kuona magavana wawili ambao ni ndugu anaweza kufikiria walipeana. Hivyo kama kuna Lowassa mwingine anachaguliwa kwenye kiti kingine cha Ubunge kama ilivyo kwa Kawawa na Malima hakuna anayeweza kupiga kelele. Au kama alivyo mdogo wake Mkapa ambaye naye ni Mbunge..
Middle,
1. Unamaanisha kuwa Watz wengi wanaopata nafasi kusoma na wapo JF kwa UK, US na kwingineko ni watoto wa wakubwa?
2. Tanzania kutafuta Mchawi bwana- hawa watoto wa vigogo wao sii Watz? Waishi na kufanya kazi wapi? Mbinguni? Ni % ya Civil Service ni watoto wa vigogo? Isije onekana kama ni ubaguzi!
Je twaweza kuona connection ya matatizo na kashfa benki kuu na uwepo wa watoto wengi wa vigogo kwenye taasisi hiyo nyeti? Binafsi hadi hivi sasa najaribu kujiambia kuwa hayo majina ni ya kutunga tu na watu hao hawapo Benki Kuu. Najaribu kujilazimisha kuamini kuwa hakuna watoto au ndugu wa kina Lowassa Benki Kuu.
Kama wapo binafsi ningependa kujua wako vitengo gani na wana position gani ili kujua kama maamuzi yao yanaweza kwa namna fulani kutiwa kiza na nafasi za wazazi au ndugu zao serikalini.
Hadi hivi sasa jina ambalo linaweza kunishtua sana ni la Lowassa, Sumaye, na Mkapa. Tunaposikia kashfa Benki Kuu na upotevu wa mabilioni ya shilingi hatuna budi kujiuliza kama hawa "ndugu zetu" waliona jambo lolote na walifanya nini kuliumbua na kuhakikisha linakomeshwa?
Hofu yangu ni kuwa kama ni kweli hawa wapo na wengine ambao hawatumii majina ya ubini wa familia zao basi uwezekano kuwa hawakujua mambo ya Tangold, Meremeta, Deep Green na makampuni mengine kama 40 hivi yaliyoanzishwa ili kuchota fedha za Umma itakuwa ni nasibu ya mwaka!
Binafsi naamini kwa moyo wangu wote Watanzania tumeshindwa kuisimamia Benki Kuu na short of firing the senior management hatuwezi kufika mahali popote pale.
Na wakishawatimua wote hao, serikali lazima iwahamishe na kupangua nafasi zote za makao makuu ya benki kuu na ikibidi walete watu toka nje kuja kuiendesha Benki Kuu kwa Mkataba maana sisi wenyewe tumeshindwa!