Watoto wa vigogo na upendeleo wa ajira nyeti serikalini

Acheni kutuchukia sisi watoto wa vigogo...hamna aliyewakataza madingi zenu kuwa vigogo
 
mimi naamini kuwa, kama data zipo za ukweli ni bora hoja hiyo ikawasilishwa hapa ili ijadiliwe, itakuwa na faida kubwa sana kwa jamii ya kitanzania kuwa 'haogopwi mtu', ukizingatia ukweli kwamba haiwezekani katika nchi yenye watu zaidi ya milioni thelathini tenda kubwa zikaenda kwa watu ambao wanatoka kwenye familia za wakubwa na matajiri tu, kwanza haitoi hata fursa kwa watu wengine kujikwamua kiuchumi na hii itaishia kuongeza utofauti kati ya maskini na matajiri
 
Acheni kutuchukia sisi watoto wa vigogo...hamna aliyewakataza madingi zenu kuwa vigogo

Nyani, wachache wameonyesha chuki kwenye thread, wengi wao wanaonyesha shauku tu la kujua mambo yaliyopelekea baadhi ya mambo kutendeka ki dhuluma...

Usiwe na hofu ndugu, kama wewe huna tenda ya kugawa madawa kwenye clinic zote za wilaya Tanzania au kama unashikilia tenda hiyo baada ya kutangazwa kwenye magazeti na TV na kuonekana tayari unajua mambo ya madawa na una kampuni ya usafirishaji, basi wewe huna la kujibu au kuongelewa, kwani kila chako kitakuwa cha haki.

Game Theory, vipi tena... mbona huleti data? Fichua tu yote unayo ona ni maovu lakini si mambo ya mahusiano kati ya 'watoto wa wakubwa' na wapenzi wao au ndugu zao.

SteveD.
 
Middle,
1. Unamaanisha kuwa Watz wengi wanaopata nafasi kusoma na wapo JF kwa UK, US na kwingineko ni watoto wa wakubwa?

2. Tanzania kutafuta Mchawi bwana- hawa watoto wa vigogo wao sii Watz? Waishi na kufanya kazi wapi? Mbinguni? Ni % ya Civil Service ni watoto wa vigogo? Isije onekana kama ni ubaguzi!

Kwa maoni yangu wana haki ya kushika nafasi yoyote kubwa na kupata tenda yoyote ile.

Je, nafasi hizo kubwa wanazozipata wanazipata kihalali!? Je wana qualifications na experience zinazotakiwa katika ajira hizo? Tenda wanazozipata nazo wamezipata kihalali!? Kwa uzoefu gani waliokuwa nao!? Je zilitangazwa kihalali ili Watanzania wenye uwezo wa kuomba tenda hizo nao watume maombi yao!? Kwa mfano mtoto wa Apson hajawahi kusimamia ujenzi wa jengo lolote lile achilia mbali hata kibanda cha kuku, je ana uwezo kweli wa kusimamia tenda ya ujenzi wa bank kuu Z'bar au ndio gharama zitakuwa sawa na kujenga majengo mawili kama hayo New York na London!? Maana Twin Towers tumeambiwa kama zingejengwa London au New York gharama zingekuwa ndogo kulinganisha na gharama halisi za kujenga Dar.
 
sasa GT mbona umeingia mitini tena, au huna issue katika hili ulikuwa mkwara tu?

mimi naamini kuwa, kama data zipo za ukweli ni bora hoja hiyo ikawasilishwa hapa ili ijadiliwe, itakuwa na faida kubwa sana kwa jamii ya kitanzania kuwa 'haogopwi mtu', ukizingatia ukweli kwamba haiwezekani katika nchi yenye watu zaidi ya milioni thelathini tenda kubwa zikaenda kwa watu ambao wanatoka kwenye familia za wakubwa na matajiri tu, kwanza haitoi hata fursa kwa watu wengine kujikwamua kiuchumi na hii itaishia kuongeza utofauti kati ya maskini na matajiri

Nyani, wachache wameonyesha chuki kwenye thread, wengi wao wanaonyesha shauku tu la kujua mambo yaliyopelekea baadhi ya mambo kutotendeka ki dhuluma...

Usiwe na hofu ndugu, kama wewe huna tenda ya kugawa madawa kwenye clinic zote za wilaya Tanzania au kama unashikilia tenda hiyo baada ya kutangazwa kwenye magazeti na TV na kuonekana tayari unajua mambo ya madawa na una kampuni ya usafirishaji, basi wewe huna la kujibu au kuongelewa, kwani kila chako kitakuwa cha haki.

Game Theory, vipi tena... mbona huleti data? Fichua tu yote unayo ona si maovu lakini si mambo ya mahusiano kati ya 'watoto wa wakubwa' na wapenzi wao au ndugu zao.

SteveD.

There isn't any dataz ni maneno tu na porojo. Mwenye dataz aweke hapa.
 
kweli watu hawana data ila walisikia tu kuwa kinje ndio hivyo,kinje yeye hana anamfanyia kazi mama yake stend ya mabasi ya ubungo na kukusanya ushuru wa parking,lakini hasa mwenye hiyo tenda ni mama yake.kuhusu jeshini kinje hausiki hata kidogo kama ndivyo anavyojigamba basi ni kutafuta ujiko tu,yeye anatumika kama kidampa tu.
 
Mimi nadhani ni vizuri kama kuna data za kweli zijadiliwe bila hofu. Kama ni coincidence haya yametokea basi itatusaidia kuondoa manung'uniko na pia wale wanaotajwa kama watoto wa wakubwa kusafishwa.

Sasa hivi kuna email ina circulate kila mahali kuhusu wale watoto wa vigogo wa BOT. kwa hiyo kuwajadili hapa aidha ni njia ya kuwatenganisha waliopata kihalali na waliopata kwa mgongo wa wazazi wao.

Iwapo 'jamaa' katumia ofisi 'ikulu' kufanya biashara itakuwa hili la ajira za vimemo!!!!
 
Mimi nikidhani maana ya KadaMpinzani inasimamia - Mwanachama wa CCM lakini upande unaoitakia mema Tanzania, hivyo kupingana na Ufisadi ama Uongozi mbaya ndani ya CCM.

Kumbe KadaMpinzani ni UNAZI!.
 
Mimi nikidhani maana ya KadaMpinzani inasimamia - Mwanachama wa CCM lakini upande unaoitakia mema Tanzania, hivyo kupingana na Ufisadi ama Uongozi mbaya ndani ya CCM.
Kumbe KadaMpinzani ni UNAZI!.

MKANDARA.........

hahahaha umeniacha SpeeChLess with BIG SMILE on MY FACE.
weekend njema kaka
 
Mimi nadhani ni vizuri kama kuna data za kweli zijadiliwe bila hofu. kama ni coincidence haya yametokea basi itatusaidia kuondoa manung'uniko na pia wale wanaotajwa kama watoto wa wakubwa kusafishwa.
Sasa hivi kuna email ina circulate kila mahali kuhusu wale watoto wa vigogo wa BOT. kwa hiyo kuwajadili hapa aidha ni njia ya kuwatenganisha waliopata kihalali na waliopata kwa mgongo wa wazazi wao.

Iwapo 'jamaa' katumia ofisi 'ikulu' kufanya biashara itakuwa hili la ajira za vimemo!!!!

Na vitu hivi ndivyo hasa vinavyotufanya tuhoji hizi coincidence, za watoto wa vigogo kujazana mahali pamoja, ama ajira na tenda za sekta nyeti za sirikali kutotangazwa hadharani. Hatupo hapa kujadili haiba za watoto wa vigogo kamwe, hayo ni mambo binafsi! Wenye ajira za vimemo wanafahamika! Wenye ajira za "chupi" wanafahamika, na wenye ajira za "vichwa" wanafahamika pia.
Tunachong'ang'ania hapa sisi akina Idimi ambao hatuna majina makubwa wala wajomba wenye pesa na madaraka sirikalini ni haki katika zabuni na ajira.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom