Watoto hujisikiaje?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,877
2,758
Huwa inakuwa vipi pale mtoto anapopata ufaham wa kutosha na kugundua baba anaemlea si baba yake? Huwa anamfikiriaje mama yake?
 
inauma, but inategemea na sababu. hakuna aliye kamili huwezi kuanza kumuhukumu mama wakati mpaka wakati huo na wewe unaweza kuwa umemfanyia mama huyohuyo makosa makubwa but kwa mapenzi yake akakusamehe. So hata yeye anastahili msahama.

Kifupi nampenda mama yangu hata angefanya nini, mimi na yeye tumejifunza kuwa binadamu hayuko perfect so tunasameheana pale mmoja akianguka na kitu ambacho kimenifanya nifurahie maisha.
 
ila hapo unaposema ungemsamehe hata angefanya nini pananipa utata
 
utata gani? namaanisha hata mama yangu angefanya kosa gani ningemsamehe.

Je wewe ungemkacha mama yako simply coz umegundua baba unayeishi nae si baba yako? Sidhani kama ni kigezo. She must have her reasons, nimewahi kusikia cases ambapo baba hana uwezo wa kuzalisha ila kama ujuavyo wanaume wengu huogopa kwenda kufanya fertility test so anaoa bila kujua hana uwezo. Ndugu zake wanaanza kumsakama mke kuwa hazai (which is mostly the case in Africa watu humsakama mke) so mke anaamua kwenda nje kuprove kama hazai or sometimes anazaa nje ili tu kuonekane kuna mtoto kwenye ndoa.
 
jamani mtoto inategemea na huyo baba anamlea katika mazingira gani ..kama anam -treat vizuri kama mwanae hatakuwa na tatizo wala wazo baya juu yake ,,,
ila ataumia pale atakapogundua huyu baba ananitesa kumbe ni si baba yangu
 
Back
Top Bottom