BabyGal
Senior Member
- Jun 30, 2011
- 165
- 62
Wewe Babygal hivi bila kuenda mbali.... wewe ungelelewa kijijini completly ungekua na exposure ya kua na access ya JF hapa saizi??
Hizo circumstances za kijijini zilikuaje?? Majority inajulikana kabisa akisema kijiji... ni kijijini kweli... huyo mtoto alotolewa mfano hapo, huyo mamake unafikiri kweli anajali welfare ya mtoto kama inavo onesha dhahiri wewe ulikua unalelewa?? labda utuambie ni kitu gania kilifanya uamuzi wa kulelewa wewe huko ulikua ni upi/ au kwa nini??
Nililelewa kijijini mpaka nilipofikisha miaka kumi na tatu..kwa umri kama huo hata ningeenda kuishi na mzazi asiye na muda na mimi isingeniumza wala kuniathiri sana kwasababu tayari nilikua na uwezo wa kuelewa kwamba zipo sababu za yeye kua mbali na mimi.Tofauti na mtoto chini ya umri huo.
Na kwa point naweza kuendelea kumtetea huyo mama ambae ameona kuliko kumtelekeza mtoto wake na house girl asiyemjua wa undani ni bora ampeleke kwa ndugu/wazazi wake anaowajua vuzuri sana kwahiyo ana uhakika kipengele cha manyanyaso hakitakuwepo.Anaweza akawa na malengo ya kumchukua na kukaa nae pindi atakapokua kidogo ili hata ikitokea mfanyakazi akawa sio mzuri sana asiweze kumnyanyasa na kumfanyia mambo yasiyo faa kutokana na umri wake.Atakua na sauti/uwezo wa kukataa inapobidi pia kumweleza mama yake kwa uwazi zaidi kama kuna tatizo.
Again yote nnayoyaongelea sio tu nimeona na kusikia kwa watu wengine bali hata mimi mwenyewe nilipitia.Nilipokua mdogo kidogo nadhani miaka minne au mitano ulitokea msiba ikabidi mama atuache na mfanyakazi.Alitulaza njaa siku hiyo hiyo kwasababu umeme ulikua umekatika/hakununua mafuta ya taa mpaka klgiza linaingia na duka lilikua mbali hivyo kutumia jiko la mchini isingewezekana na mwisho kabisa hakutaka/aliona kazi kuwasha jiko la mkaa.First thing in the morning alikuja dada yetu mmoja kuangalia tunaendeleaje ndo akapata kujua hatukula jana yake (mind you we werent ratting the girl out but something happened so we had to tell) .Sasa hapo ndio muone tofauti ya ndugu (japo nao sio wote wenye mapenzi) na mtu baki awe mfanyakazi au mama wa kambo ambao wengi wao hua hawajali ilimradi wao wapate chao.