Watoto....best interest.....

Zaweza kuwepo...japo labda hazitoki kwa mtoto.....
Hivi mzazi wa kike akikosa uwezo wa kukaa na mtoto wa miezi miwili (labda sababu za kimaisha ama ugonjwa)...kwa nini baba asipewe jukumu hilo kama anaweza?

Rai yangu ni muda wote kufanya maamuzi yanayozingatia masilahi ya mtoto kwanza....

Ndio maana nikasema ni vema likaangalia na kigezo cha uwezo hata hivyo nadhani pia kuna assumption kuwa mtoto wa chini ya miaka saba bado anatakiwa kuwa attached na mama yake (kuna ile bond kati ya mama na mwana ambayo ni muhimu sana kipsychologia kwa maendeleo ya mtoto) that is why hata sheria inambana Baba kama mama hana uwezo wa kulea basi baba atoe matumizi wakati mtoto anaendelea kuishi na mama. Ila wengi wetu tunaitumia hii chance vibaya, wengine huwakatalia hata wenzi wao kuja kuwaona watoto wao kwa kisingizio cha ugomvi! ni immature thinking tu na uselfish wa kipotofu.
Mtoto ana haki ya wazazi wote wawili (hata kama wameseparate, wametalikiana au wanaishi pamoja)
Mtoto ana haki ya mapenzi toka kwa pande zote mbili na anayo haki ya kuruhusiwa kupenda wazazi wote wawili
 
Aisee hili sredi halifai kuchakachulika aisee....... Ni mapwenti tu!

ODM anaunga mkono hoja na ushauri wa kijana wangu wa ubatizo....

Acheni kutumia watoto kama silaha ya kukomoana
Acheni kutumia watoto kama chambo cha kurudisha uhusiano ulioparanganyika ambao hata mkirudiana bado ni maumivu kwa mmoja wenu.

Na hili ndilo Neno la Mungu.
 
hommie baba anakaaje na mtoto aw miezi miwili? atamnyonyesha? nadhani hapo ingekuwa kuweka mazingira wezeshi, ya kumsaidia mama/mamdogo/shangazi/ili waweze kuziba pengo la mama

Kumbuka baba anatambulika kwa majukumu yake,,,nazungumzia maslahi ya mtoto zaidi hapo

Darling I am sorry to say hapa napingana na wewe....Kuna mifano mingi tumeona katika jamii... kama kakaa na mamake kwa miaka saba yoote, what is wrong with huyo mama aendelee kumtunza?? Pamoja na kusema baba anatambulika NDIO, But kumbuka kua mama mara nyingi humlea mtoto kwa karibu kuliko hata baba, baba akimchukua in most cases anapelekea kwa Step mom, why not leave the kid na mamake uendelee kutoa huduma??
 
Hommie...... Baba akabidhiwe mwanae kama mama hana uwezo wa kulea kutokana na sababu yoyote ile. Baba ndo aamue nani wa kumsaidia kumlea mwanaye......... haifai kuopt kwa ndugu wengine bila kumhusisha mwenye mtoto.
 
sweetie, hapo uko sawa na mimi kabisa, nilichosema ni kusupport mtoto kukaa na mtu anayeweza kubeba majukumu ya mama endapo mama anashindwa kwa sababu ya ugonjwa kwa mfano, ambao unamfanya asiweze kumlea mtoto, au kwen extreme labda amefariki....na kukwepa ila issue ya kumfanya mtoto akae na baba yake wakati baba hawezi kumlea kama ambavyo mama angemlea. baba anatakiwa aprovide mahitaji tu, ndo majuku hayo au sio love

Yanii uniachie kakid hako kakizaliwa:mimba: si itakuwa balaa love?
 
completely agreed hommie....hapo sisemi baba asihusishwe...khaaa
 
Ndio maana nikasema ni vema likaangalia na kigezo cha uwezo hata hivyo nadhani pia kuna assumption kuwa mtoto wa chini ya miaka saba bado anatakiwa kuwa attached na mama yake (kuna ile bond kati ya mama na mwana ambayo ni muhimu sana kipsychologia kwa maendeleo ya mtoto) that is why hata sheria inambana Baba kama mama hana uwezo wa kulea basi baba atoe matumizi wakati mtoto anaendelea kuishi na mama. Ila wengi wetu tunaitumia hii chance vibaya, wengine huwakatalia hata wenzi wao kuja kuwaona watoto wao kwa kisingizio cha ugomvi! ni immature thinking tu na uselfish wa kipotofu.
Mtoto ana haki ya wazazi wote wawili (hata kama wameseparate, wametalikiana au wanaishi pamoja)
Mtoto ana haki ya mapenzi toka kwa pande zote mbili na anayo haki ya kuruhusiwa kupenda wazazi wote wawili

Thanks MJ1....
Vipi hii hali ya mama kumpeleka mtoto mdogo kwa dada yake (au mama yake), anaposhindwa kukaa nae? Kwa nini baba asiwe second option?
 
hommie baba anakaaje na mtoto aw miezi miwili? atamnyonyesha? nadhani hapo ingekuwa kuweka mazingira wezeshi, ya kumsaidia mama/mamdogo/shangazi/ili waweze kuziba pengo la mama

Kumbuka baba anatambulika kwa majukumu yake,,,nazungumzia maslahi ya mtoto zaidi hapo

Afu Kaizer unadhani wababa wengine ....hasa wale wanaowanyang'anya wake zao watoto wakingali wadogo wengi wao huishia kumpeleka kwa Mama yake, dada yake ni wachache sana wanaoishi nao under one roof na kutekeleza mahitaji ya mtoto....kwa sababu tufike sehemu tukubaliane kuwa malezi ya mtoto ni tofauti na matunzo ya mtoto.....Malezi ni zaidi ya nguo, chakula na malazi.
 
Thanks MJ1....
Vipi hii hali ya mama kumpeleka mtoto mdogo kwa dada yake (au mama yake), anaposhindwa kukaa nae? Kwa nini baba asiwe second option?

RR hii mimi ninaipingwa kwa kusimamia vidole gumba......kwangu mie ni sawa na kumtusi dada yangu maana nikijaulizwa "kwani mumeo/baba watoto wako alizaa na wewe au dadako?' ntajibuje? Hii RR ni sehemu ya ubinafsi na kukomoana. Unless kuna dalili za kuwa Mama aliyekaimu anamnyanyasa mwanao ndio usite kumpeleka kwa babake LAKINI HATA katika situation hiyo ni vema mkazimeza Pride zenu na kudiscuss juu ya hili!

Na inategemea na mwanzo wa kuachana kwenu mlilihandle vipi swala hili kla mtoto kwa kuwa kama mama alishavimbisha kichwa kuwa mtoto ni wangu blablabla.baba anawezaakatake advantage ya kumchukua hata kama anajua hana pa kumpeleka!
 
  • Thanks
Reactions: RR
Afu Kaizer unadhani wababa wengine ....hasa wale wanaowanyang'anya wake zao watoto wakingali wadogo wengi wao huishia kumpeleka kwa Mama yake, dada yake ni wachache sana wanaoishi nao under one roof na kutekeleza mahitaji ya mtoto....kwa sababu tufike sehemu tukubaliane kuwa malezi ya mtoto ni tofauti na matunzo ya mtoto.....Malezi ni zaidi ya nguo, chakula na malazi.

Exactly my dear...hapo kweli kabisa..wapi Maty na issue ya wanaume suruali LOL
 
sweetie, hapo uko sawa na mimi kabisa, nilichosema ni kusupport mtoto kukaa na mtu anayeweza kubeba majukumu ya mama endapo mama anashindwa kwa sababu ya ugonjwa kwa mfano, ambao unamfanya asiweze kumlea mtoto, au kwen extreme labda amefariki....na kukwepa ila issue ya kumfanya mtoto akae na baba yake wakati baba hawezi kumlea kama ambavyo mama angemlea. baba anatakiwa aprovide mahitaji tu, ndo majuku hayo au sio love

Yanii uniachie kakid hako kakizaliwa:mimba: si itakuwa balaa love?

Hapo nimekupata lov... Najua kua mhusika anapopeleka mtoto mahala kulelewa anakua kabisa na best interests at heart ya kusema kua atamtunza ipasavyo... hio hubadilika saaana with time, kama alikua anaprovide kila week, itaanza kurushwa hadi kupotea kabisa mpaka pale itokee shida kama maybe ada au matibabu and the like - Pamoja na kusema kupeleka kwa mtu mwingine sababu baba hawezi kulea is the best option kwa wakati huo... Ila tu sema sababu haiepukiki, Matunzo ya huyo mtoto hasa emotionally and psychologically hua disturbed kabisa....

And of coz nitakuwinda kila siku kwenye ndoto ukimfanyia hivo kid wetu...
 
Mmmh hawa watakatifu wazamani, wanakuaga na point siku ya Ijumaa kweli? Dah ubarikiwe kwa somo zuri.

hahaha inabidi niulize kama jana umelalia ubavu upi manake sikujua kama Ijumaa imeshafika? LOL

halafu umemchafua Hommie mtakatifu wa zamani, inabidi umsafishe asiee...inauma sana
 
Wapo wengine na hii ni kwa wote wankwenda mbali zaidi kwa kuwatorosha na kuwaficha kabisa watoto hawa nao tuwaambieje?
 
Mmmh ex-Saint ni nini? Ndio maana haiwezekani point zitoke ijumaa bana kumbe ni pre-friday Kaizary! Abarikiwe ex-mtakatifu.
 
Utaniombea wapi radhi.......
 
Mh huyu anayefanya hivi ni mkatili kwa kweli. Mara nyingi mmama anayefanyiwa hivi huumia sana na kawaida huwa si rahisi kuvumilia kwa kuwa yeye ni mama atahangaika tu ampate. Na mbaba anayefanyiwa hili huumia pia ingawa huwa ana uhakika mkubwa kuwa mwanae atakua tu kwani mama ni mama. Kasheshe ni pale ambapo mama anapokuwa hana 'uwezo' wa kumlea vema huyo mtoto aliyemficha!!
 
Mmmh ex-Saint ni nini? Ndio maana haiwezekani point zitoke ijumaa bana kumbe ni pre-friday Kaizary! Abarikiwe ex-mtakatifu.

Utaniombea wapi radhi.......

Hivi si niliona Babu akiasa juu ya uchakachuzi wa hii thread ambayo ni useful yenye kutugusa wengi kwka namna moja au nyingine?? Waone vile
LD unafikiri kwa nini Mama anawezakuwa na chuki kiasi cha kumnyima mtoto wake haki ya kuwa na Baba yake?
 
  • Thanks
Reactions: RR
Back
Top Bottom