Elections 2010 Watishiwa Kunyimwa Mbolea ya Ruzuku kwa Kumuunga Mkono Mgombea wa Chadema

Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,290
756
MGOMBEA ubunge wa jimbo la Njombe Magharibi kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema) Thomas Nyimbo ameuonya uongozi wa serikali ya wilaya ya Njombe mkoani Iringa pamoja na aliyekuwa naibu spika wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda kuacha mchezo mchafu wa kuwatisha wananchi wa jimbo hilo kuwa iwapo watakwenda katika mikutano ya Chadema ama kuchagua chama hicho hawatapatia mbole ya ruzuku na wafanyabishara waliopo jimbo hilo watafukuzwa kufanya biashara katika wilaya hiyo.

“Nguvu inayotumika huku jimbo la Njombe Magharibi ni kubwa kwani serikali ya CCM imefikia hatua ya kuweka picha za mgombea ubunge wao Geyson Lwenge katika ofisi za kijiji cha Isinagosi baada ya wananchi wa jimbo hilo kukataa CCM kubandika picha za mgombea huyo katika nyumba zao kwa madai si chaguo lao na hawataki kuziona picha zake katika kijiji hicho ……ila hapa nauliza kuwa Chadema jimbo hili inashindana na CCM ama Serikali na nani anawapa nguvu maofisa watendaji wa vijiji na kata kuwatisha wananchi kuwa wakikutwa katika mikutano wawajibishwa”

Akiwahutubia mamia ya wakazi wa kijiji cha Itulahumba kata ya Mdandu jimbo la Njombe Magharibi katika mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni ,Nyimbo alisema kuwa akiwa kama mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chadema atahakikisha anapambana na mbinu chafu za CCM hadi bungeni Dodoma mara baada ya wananchi wa jimbo hilo kuihukumu NEC ya CCM octoba 31 kwa kumnyima kura mgombe wao Geyson Lwenge ambaye ni nabii asiyekubalika kwalo.

Nyimbo ambaye aliongoza kwa kura 6793 katika kura za maoni ndani ya CCM kwa kumshinda mbunge wa jimbo hilo Yono Keve3434 huku mteule wa NEC ya CCM akiambulia kura 2971 alisema kuwa uchaguzi katika jimbo hilo na mbunge tayari wananchi walimchagua yeye hivyo hata kama mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wote wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) wataweka kambi katika jimbo hilo wataambulia aibu na laana ya Mungu kwa dhambi waliyotenda ya kuwapokonya haki wana Njombe Magharibi Dodoma.

Alisema kuwa uamuzi wa wananchi wa jimbo hilo kumtema mbunge Kevella na kumchagua yeye ni uamuzi uliopaswa kuheshimiwa na NEC ya CCM ila kutokana na kujiamini kuwa wao hata kama watasimisha jiwe kugombea lazima washiinde kwa kuiba kura kwa jimbo hilo wamechemka na ili kuonyesha kuwa kura alizopata yeye ndani ya CCM sio kura za kubahatisha na wala sio za wizi kama walivyozoea wao basi CCM isubiri majibu octoba 31 na kuwa kura zake zitalindwa na wananchi wenyewe na mbinu zote za wizi wa CCM zinafahamika na wao wamejipanga kupambana na wizi huo kwa nguvu zote.

“Napenda kuwaomba wana Njombe Magharibi kutokubali vitisho vya CCM na serikali yake kwani kama uhuru nchi hii imepata uhuru toka mwaka 1961 hivyo hakuna mwananchi atakayenyanyasika kwa kuinyima kura CCM octoba 31 …nawaomba sana wananchi wangu wasiendelee kulia kwa kitendo cha wajumbe wa NEC ya CCM kuwavua nguo zao Dodoma kwa kupindua matokeo ila wajiandae kuivua nguo siku ya uchaguzi mkuu ambapo kura ni siri yao na hakuna wa kugeuza matokeo baada ya kupiga kura “

Katika hatua nyingine Nyimbo alihoji serikali ya CCM kupeleka watu wa usalama wa Taifa na askari polisi kwa wingi katika mikutano yake kwa lengo la kutisha watu badala ya usalama hao waTaifa kupelekwa Dodoma kuchunguza haki ya wananchi wa jimbo hilo ilivyonyang’anywa kwa nguvu na wajumbe wa NEC


Hata hivyo Nyimbo alisema kuwa katika maisha yake hakupanga kujiunga na Chadema ila uporaji wa haki za wananchi wa jimbo hilo uliofanywa na NEC Dodoma ndio uliompeleka kugombea ubunge kupitia Chadema na pia uteuzi wa Chadema kwa Dr Silaa kugombea urais umeweza kumvuta sana kushiriki katika mapambano ya kuiondoa serikali ya CCM madarakani mwaka huu.

Wakati huo huo CCM katik jimbo hilo kuna uwezekano wa kusambaratika baada ya madiwani wake walioangushwa katika kura za maoni na wale wanaogombea tena nafasi hiyo kutishia kurejesha kadi za CCM na kuacha kuhama chama hicho iwapo chama kitawalazimisha kuendelea kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo Lwenge ambaye wamedai kuwa hauziki haka katika kijiji chake cha Dulamu kata ya Ugwachanya ambako aliambulia kura sita huku Nyimbo akiongoza kwa kura zaidi ya 100 katika kijiji hicho .


Mmoja kati ya madiwani wa CCM ambao wanagombea jimbo hilo ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema kuwa hali ya kisiasa katika jimbo hilo ni mbaya sana na kuwa ni heri ya jimbo la Iringa mjini CCM inaweza kupenya ila sio Njombe Magharibi ambako Nyimbo ameonyesha kukivuruga kabisa chama cha mapimnduzi na kila mwananchi wa jimbo hilo akiombwa kura ya udiwani anataka kupata maelezo ya Nyimbo kuenguliwa na kueleza wazi kuwa hawatatoa kura zao kwa CCM .

“Ujue ndugu mwandishi madiwani wengi tuliogombea tulipita kwa nguvu ya Nyimbo japo wapo wa mbunge aliyemaliza muda wake Kevella ila wale wa Nyimbo ni wengi zaidi ….sasa ukisimama sehemu na kumsema vibaya Nyimbo ama kumwombea kura Lwenge (CCM) wananchi wanatamka wazi kuwa hata wewe hatukupi kura ……sasa tumekuwa tukifanya kampeni za ujanja sana kwa kusoma upepo na sehemu nyingine tumekuwa tukijinadi kwa kumtumia Nyimbo ili tuweze kukubaliwa vinginevyo hukumu dhidi ya Lwenge itatua kwetu"


Francis Godwin ni mzee wa matukio daima: NYIMBO APINGA WANANCHI KUNYIMWA MBOLEA YA RUZUKU KWA KWENDA KWENYE KAMPENI ZA CHADEMA...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom