"Watesaji walimhoji kama CHADEMA inahusika"

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,342
6,467
Hii inaweza kuwa ni clue nzuri ya kumfahamu mwenye mkono kwenye masahibu yaliyompata Dr. Ulimboka. Hivi ni nani anayekihofia Chadema hapa Tanzania? Chadema ni taasisi gani? Jibu la swali la pili ni chama cha siasa, chama cha upinzani rasmi bungeni, chama tishio kwa CCM.

Source: Mtanzania, 29 Juni 2012.
 
Kuwa makini na mawazoyako hayo,usijenge hoja ambazo hazina msingi,watakaosema hivyo ni akina nani wakati wewe ndo unasema.
Eleza sababu ambazo zimekufanya wewe ufikirie watasema hivyo hao ukiwemo na wewe.
 
Hili laweza kuwa kweli, wamejitahidi sana kuunganisha mgomo wa hawa madaktari na siasa,lakini imeshindikana. Ndio maana hata mimi napinga kabisa viongozi wa CDM kutaka kujihusisha na madaktari kwa faida za kisiasa, waacheni wagome kama professionals na sio kisiasa!
 
huyu mtu kanivuruga kabisa na hii hoja yake..yaani CHADEMA inahusikaje ?
 
haya maneno kama yamesemwa na Dr. Ulimboka ina maana wahusika wameshajulikana. hakuna sababu ya kuunda tume ambayo wahanga wenyewe hawana imani nayo. Ni vizuri huyu mhanga akaendelea kulindwa masaa 24 na watu wake wa karibu tu. Kuna madaktari wengine, tena kama wale wasiogoma kwa kuogopa LIWALO NA LIWE ndo wasiaminiwe kabisa.
 
Mleta thread jaribu kufikiri sana kabla ya kuja hapa jamvini!

Una maanisha kabla ya kuandika? Hiyo heading ni sub headline ukurasa wa mbele au juu kabisa kwenye gazeti la Mtanzania la leo tarehe 29 June 2012 sasa tatizo liko wapi? Labda mwambie mwandishi wa habari hiyo afikirie kwanza?!
 
Mimi kinachonishangaza ni hiki, kwanini CHADEMA wanashangilia sana huu mgomo wa madaktari? kuna nini hapa jamani.
 
Magamba mnakimbia kivuli chenu wenyewe na bado mtaanzana wenyewe kwa wenyewe !
 
Up to this moment am puzzled I can't judge completely who is involved. Mungu tuokoe tafadhali maana hatujui tuendapo
 
Mimi kinachonishangaza ni hiki, kwanini CHADEMA wanashangilia sana huu mgomo wa madaktari? kuna nini hapa jamani.

Mkuu sio CHADEMA tu, tuko wananchi wengi tunaowaunga mkono Drs mkono japo sio wanachama wa chama chochote! Tafakari na chukua hatua stahiki!
 
huyu mtu kanivuruga kabisa na hii hoja yake..yaani CHADEMA inahusikaje ?

tuliza hasira; Dr ULi katika kauli zake chache alizotoa alisema kuwa wakati hao vijana maalium wakim-limboka walikjuwa wakimtaka akiri kuwa CDM iko nyuma ya mgomo. Its no gossip men!!.
 
Ndio alivyokuwa anataka kuaminisha hivyo. Self incriminating.
 
Back
Top Bottom