Watendaji wamuacha solemba Rais Kikwete

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Na Daniel Mjema, Moshi

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, watendaji watano wa serikali mkoani Kilimanjaro, jana hawakutokea kwenye ziara ya Rais Jakaya Kikwete na kusababisha maswali yanayohusu kero za wananchi kutopata majibu ambayo mkuu huyo wa nchi aliyatarajia.

Hali hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa Kilimanjaro, Monica Mbega aliyekuwa pamoja na rais kwenye meza kuu kuonekana kukosa amani kila wakati mtendaji ambaye rais alimtaka asimame ili atoe majibu kwa wananchi, kukosekana kwenye ziara hiyo.

Sakata hilo lilitokea jana eneo la Marangu Mtoni wilayani Moshi Vijijini baada ya Rais Kikwete kumaliza hotuba yake ya ufunguzi wa tawi jipya la benki ya CRDB Marangu na kuamua kuingia kwenye siasa kutafuta kero za wananchi.

Akiwa kwenye mkutano huo, Kikwete alianza kwa kumwita kwa kumshitukiza mwenyekiti wa Kijiji cha Samanga, Thomas Makiponya ili aeleze shida zote zinazolikabili eneo hilo ili yeye kama mkuu wa nchi aweze kusikia na kuzitafutia majibu.

Ndipo mwenyekiti huyo alipoainisha kero mbalimbali ikiwamo tatizo la mifereji ya asili na zahanati ya kijiji ambayo ni ya zamani sana na kwamba alishaiandikia halmashauri ili iikarabati, lakini hakuna kilichofanyika.

Kero nyingine ambayo mwenyekiti huyo alimweleza rais ni kuhusu barabara za vijijini zilizo pembezoni mwa barabara kuu ambazo alidai zinawapa shida sana; kukosekana kwa kituo cha polisi na pia taabu wanayopata watumishi wastaafu.

Baada ya maelezo hayo, Rais KIKWETE alisema suala la ukarabati wa mifereji ya asili limezungumziwa pia na Mbunge wa Jimbo hilo, Aloyce Kimaro hivyo akataka mkurugenzi wa umwagiliaji asimame kutoa majibu, lakini mtendaji huyo hakuwepo mkutanoni.

Kukosekana kwake kulimlazimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi, Anna Mwahalende kujitutumua kujibu maswali mengi, likiwamo la mifereji ya asili akisema japo wanajitahidi kuikarabati, lakini bajeti haitoshelezi.

Wakati akieleza, Rais Kikwete aliingilia kati na kuuliza: "mkurugenzi wa umwagiliaji yuko wapi? maana yeye ndio mhusika ingawa halmashauri nayo ina nafasi yake…au hakualikwa?"

Na wananchi wakamjibu kuwa "kaingia mitini".

Baadaye, Rais Kikwete alimtaka mganga mkuu wa wilaya hiyo au daktari wa wilaya atoe maelezo kuhusu hoja ya zanahati, lakini kwa mshangao wa wengi hakuna aliyekuwepo hali iliyomfanya mkuu huyo wa nchi kuhamaki na kuhoji sababu za kutokuwepo kwa watendaji hao wote.

Japokuwa mganga mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Mtumwa Mwako naye alijitutumua kujibu, maelezo yake hayakumridhisha Rais Kikwete ambaye alisema kila swali linaloulizwa lina mwenyewe na watendaji hao wangekuwepo majibu mazuri zaidi yangepatikana.

Rais Kikwete hakuishia hapo, akamtaka mhandisi wa barabara wa wilaya atoe maelezo kuhusu kero ya barabara za vijijini, lakini kwa mara nyingine mtaalamu huyo hakuwepo katika mkutano huo, hali ambayo iliwafanya wananchi kuguna huku Mbega akionekana kukosa amani zaidi.

Hata Rais Kikwete alipomuulizia ofisa kilimo wa wilaya na ofisa anayeshughulikia mfuko wa Tasaf ili watoe maelezo kuhusu masuala yanayohusu ofisi zao, nao hawakupatikana, hali iliyoonyesha dhahiri kuwa ilimkera Rais Kikwete.

Baadaye Rais Kikwete alisema tatizo la halmashauri nyingi nchini ni wizi, akifafanua kuwa huwa zinapata fedha nyingi ambazo zingeweza kutekelezwa kwa shughuli nyingi za maendeleo vijijini, lakini zinaishia mifukoni kwa baadhi ya watendaji.

Alisema matatizo mengi yaliyoibuliwa na wananchi ameyasikia naye ameyachukua na atayafanyia kazi.


Chanzo: Mwananchi
 
kama amegundua tatizo ni wizi kachukua hatua gani? kwani leo ndo Vasco da Gama kajua halmashauri kuna wizi si pesa hizo ndo wanazozitumia kwenye kampeni za ccm!
 
Nini maana ya kukimbiwa na watendaji, hawakuwa na taarifa ya ujio wake? nafikiri hapana, tatizo hapa ni uwajibikaji na dharau iliyojengeka miongoni mwa viongozi ikiongozwa na mtendaji wao mkuu ambaye ni rais, pia wanaona kuwepo au kutokuwepo katika mkutano ni kitu cha kawaida maana hata wakieleza matatizo yao huwa hayatiliwi maanani.
 
Hii ni dharau kwa mkuu wa nchi......sijui siku hizi watu wanauchukulia urais kama kitu kidogo sana.....juzi rweyemamu anatoa cheap answers....eeh magari yaliharibika lakini ni jambo la kawaida....mmmh yaani wee acha tu....Rais??!!! mmh sielewi haya yoote yanaashiria nini
 
Mimi naungana kabisa na watendaji ambao hawakuweko. Hivi kulikwa na ulazima wa wao kwenda kushuhudia ufunguzi wa kale ka benki ka CRDB pale marangu mtoni? Kama raisi wa nchi ametumia gharama kubwa sana kuja pale Marangu kufungua tawi dogo kabisa la benki. Sura ya ufunguzi huu ilikuwa ya kichama zaidi kuliko ambavyo ingetakiwa iwe. Kama alikuwa kichama hakukuwa na sababu za yeye kuulizia wakurugenzi au watendaji wa shughuli za kiserikali.

Kwa kufanya kwao kazi kwa pupa bila kujua na kujenga watu hofu ndiko kulikopelekea wao kudhani kuwa penye raisi lazima watendaji wawepo. Hii si kweli! Kuna sehemu amabazo zinahitaji watu fulani wawepo ili kazi ziende! Kwa mfano labda mganga mkuu wa mkoa ndiye bingwa wa upasuaji na kuna ajali angemwacha mgonjwa afe kisa JK anafungua CRDB? Huu ni mtizamo potofu. Na kwa nini mpaka aje ndo ahoji hiki na kile? Ni kuuza sura tu wala hakuna lolote.

Bila aibu Mkuu wa mkoa anafungua shughuli ya kijamii anaanza KIDUMU CHAMA CA MAPINDUZIIIIIIIIIIIIII! Lol yaani wasokuwa wanaCCM hawaruhusiwi kujiunga CRDB? Kwani CRDB ni taasisi ya CCM?

Angetambua uwepo wa wadau wengine na sio CCM. Kwa kujikweza wengi walijipigia jezi zao! Nasikia hata kile kituo cha polisi kule Kibosho alichoenda kufungua walikuwa na pamba za kijani! kituo kilichojengwa na wadau wa kibosho ambacho hakina senti hata moja ya Serikali yake anakivalia njuga. Maabusu wa pale watakuwa ni wanaCCM tu ama na wengine pia?

Poleni CCM
 
Watendaji hao wanajua vizuri wajibu wao na ngazi za uongozi na wanajibu kwa nani ndio maana hawakuhitaji kuonana na JK. Kwani wanawajibika kwa JK? Yeye anatakiwa kuwawajibisha anaowasimamia kama mawaziri, n.k. ambao anawagwaya!
 
Hivi kila ujio wa Rais mahali lazima kila mtu aache kazi yake na kwenda kumlaki? Kwenye ufunguzi wa tawi la CRDB Mganga Mkuu wa Wilaya aende kutafuta nini? Akiacha hospitali na likatokea janga la vifo tata vya wagonjwa mtaanza kumlaumu kwamba aliacha kazi yake akaenda kwenye ufunguzi wa CRDB ambayo haina uhusiano wowote na kazi yake!

Ingeeleweka kama angelikuwa amekwenda kufungua zahanati Wilayani humo au angelikwenda kwenye eneo la mradi wa umwagiliaji maji ndipo angeliweza kuhitajika kuwepo huyo Mkurugenzi anayehusika. Mbona hakuwauliza Polisi wajibu kuhusu kero ya kukosekana kituo cha Polisi, au kawaogopa?

Leo mwaka wa 5 madarakani ndio anazungumzia habari kuhusu wizi katika halmashauri nyingi! He must be joking! Au ndio 'utani' mwingine huo?
 
Kila mtendaji wa serikali katika mkoa akishaalikwa si lazima walipwe ma per diem mengi tu. hizi si ndio zile safari ambazo pinda alikuwa anasema atazipunguza what is wrong with these people; and where was he all this time hakuja kusikiliza kero za wananchi. kwanini watu wawe vigeugeu kiasi hiki.

Na nani alisema kwamba kiongozi bora ni yule anayejidai kukasirika in public; nina uhakika 200% nothig will follow baada ya yeye kuondoka porojo nyingi na watendaji wameshajua huku ni kubweka tu hakuna kungata.
 
Je kwa hao viongozi kuingia mitini wataadhibiwa, au ndio usanii uliofanywa makusudi waingine mitini then ijulikane wao ndio wamekimbia kumbe ni usanii wa serikali yetu.

well na yeye mbona alituingia mitini hapa UK badala yake akaenda kuangalia mpira ???
 
Hivi kila ujio wa Rais mahali lazima kila mtu aache kazi yake na kwenda kumlaki? Kwenye ufunguzi wa tawi la CRDB Mganga Mkuu wa Wilaya aende kutafuta nini? Akiacha hospitali na likatokea janga la vifo tata vya wagonjwa mtaanza kumlaumu kwamba aliacha kazi yake akaenda kwenye ufunguzi wa CRDB ambayo haina uhusiano wowote na kazi yake! Ingeeleweka kama angelikuwa amekwenda kufungua zahanati Wilayani humo au angelikwenda kwenye eneo la mradi wa umwagiliaji maji ndipo angeliweza kuhitajika kuwepo huyo Mkurugenzi anayehusika. Mbona hakuwauliza Polisi wajibu kuhusu kero ya kukosekana kituo cha Polisi, au kawaogopa?

Leo mwaka wa 5 madarakani ndio anazungumzia habari kuhusu wizi katika halmashauri nyingi! He must be joking! Au ndio 'utani' mwingine huo?

Hivi uthibitisho wa wizi huo ameutoa kwenye taarifa za mkaguzi mkuu wa serikali au ameota tu na kutaka kuufurahisha umati uliopo mbele yake?
 
Watendaji waligoma kwenda kwasababu walijua Muungwana anaenda kuwapa kitochi.Mtendaji gani atakubali kunywa kitochi !!!!!!!!!.lol.
 
JK asitake mambo mengine ya utendaji yakwame, anataka azungukwe kama alivyofanyiwa pale diamond ili afurahi kuwa anaogepwa na viongozi. Alitakiwa kujua kuwa kuna shughhuli zinazoendelea ya kuhudumia wananchi badala ya kuwakusanya viongozi pamoja kisa ufunguzi wa CRDB.

kingine kinachoudhi ni huu UCCM kila mahali, wwanafikiri mida yote ni propaganda ya CCM. kufikiri hivyo ni sawaa na kujilisha upepo. wanaona nje ya CCM hamna maisha. Ni uniform tu kila mahali.
 
Hivi uthibitisho wa wizi huo ameutoa kwenye taarifa za mkaguzi mkuu wa serikali au ameota tu na kutaka kuufurahisha umati uliopo mbele yake?

Alitaka kufurahisha umati uliopo mbele yake! Mwaka 2007 alitishia kuzifunga halmashauri zilizokithiri kwa wizi -- lakini hakuna iliyofungwa!
 
wamemuona longolongo, hana mpango, anawatwisha mizigo ya Lawama kwa faida zake kisiasa. wamemshiti, .
wamemuonyesha kwa vitendo kuwa watumishi wauma wapo kwenye mgomo siku nyingi.
 
Good kama watendaji wote wangefuata mfano wa hao tungefika mbali, huu si uongozi ni majungu yaani swala la kupalilia barabara za vijinini ni la Rais, na mwenyekiti wakijiji atafanya nini? Ndio maana Lowasa na Rostam wanamuona kishoia hata mwenye duka la dawa baridi pale kijijijni kwao msoga hafanya kazi hivyo. watendaji wanamjua kwamba sio kiongozi na wananchi sasa tunamjua hivyo hivyo ndio maana kwa sasa tunajifanyia mambo yetu kimya kimya
 
Hii ni dharau kwa mkuu wa nchi......sijui siku hizi watu wanauchukulia urais kama kitu kidogo sana.....juzi rweyemamu anatoa cheap answers....eeh magari yaliharibika lakini ni jambo la kawaida....mmmh yaani wee acha tu....Rais??!!! mmh sielewi haya yoote yanaashiria nini

Nduku yangu wewe mbado unaishi katika ensi walisokuwa wanatumia mawe kama sana sa kuwindia? Ulitaka mtu kama huyo bwana mganga aache kutibia watu aende kusikilisa rais?
 
Nduku yangu wewe mbado unaishi katika ensi walisokuwa wanatumia mawe kama sana sa kuwindia? Ulitaka mtu kama huyo bwana mganga aache kutibia watu aende kusikilisa rais?

Tuko pamo! Pamoja babaangu. Hifi arawa niche mbeke inapasua mabiba niende nikasikilise kitu kani sasa. Kila mwooka ndifyo ifyo tu hakuna la saidi. Eti sidumu fikra sa mwalimuuuuuuuuuuuuuu. Tanu oyeeeeeeeeeeeeeee. Mbesa sa fooo wai.
 
well done watendaji...walijua hna la maana la kuongea ndo maana wakaendelea na mambo yao mengine...
 
Mtu mpumbavu akimdanganya mwelevu akafanya kama vile anavyotaka mwisho wa siku mambo yanakuwaje? Mara nyingine kwa mtu anayejua maana na ukuu wa kusimama mbele ya watu na kutoa ahadi, hawezi kujipeleka mbele akadanganye. Ni afadhali asulubiwe kama mtoro kuliko kusema uongo. Hizi zinazoendelea sasa ni sanaa tu!!!
 
Back
Top Bottom