Watch Out; Tigo Pesa, M-Pesa ni Janga Kuu, wengi Wameumia!!

Naona kama wewe ndio Unaropoka, nimetoa advantages za hizi huduma kama vile kurahisisha utumaji, upokeaji pamoja na uhifadhi wa hela, pia ajira.
Pia nikatoa na tahadhari na namna mbalimbali watu wanavyolizwa.
Au mkuu wewe ni mojawapo ya hao Walizaji so nimegusa anga zako nin??

Hata mimi nimepata wazo la kuwa jamaa katokwa na povu kwa kuwa umeharibu dili lake! Big up mdau wa ukweli kwa kutuelimisha.
 
Wezi si viongozi wetu bali kutokana na ugumu wa maisha wakati Tanzania imejaliwa na fursa nyingi wakati wengine wako peponi kunalazimisha tabaka la chini kubuni survival strategies/coping mechanism, iwe nzuri or mbaya.
 
Mimi naona tigo wenyewe wanahusika na kama hawahusiki wanawajua wanaohusika
USHAURI

"TUHAMASISHE WATU KUTOKUTUMIA TIGO PESA NA NAOMBA KAMA INAWEZEKANA UJUMBE HUU WA JINSI MCHEZO ULIVYOFANYIKA UTOLEWE KATIKA VYOMBO VYA HABARI ILI KUTOA FUNZO KWA KAMPUNI ZINAZOWAHIFADHI MATAPELI" Ushahidi uliopo unatosha kabisa na hii itasaidia maana wengi wameumizwa kwa mtindo huu na wakienda tigo service wanaambiwa namba yako imeharibika na haiwezekani kurudishwa labda nunua laini nyingine kumbe wanajua nini kinaendelea juu ya laini ya mteja
Mimi naomba sana Ujumbe huu unatosha kabisa kwa kampuni isiyotaka kuchafuliwa jina/biashara yake kuhusishwa na utapeli na mimi naona ni muda muafaka wa kuchukua maamuzi na kama ikiwekwa katika FRONT PAGE gazeti litauzwa sana
Pia kama wanajamii forum wapo waandishi wa habari waende TIGO MAKAO MAKUU waulize kwanini namba nyingi zenye pesa katika akaunti zao zinaharibika? na Je kwanini wateja wanaibiwa na kama wao hawawezi kuzuia laini ya mteja kuingiliwa na matapeli wanampango gani wa kuwajulisha wateja wao wasitumie tigo pesa maana hawawezi kulinda akaunti zao? "MAJIBU YA MAELEZO/MAHOJIANO YACHAPISHWE ILI WATEJA WAWEZE KUPIMA KAMA KUNA UWEZEKANO WA KUENDELEA KUTUMIA HUDUMA YAO YA TIGO PESA AU LA?"Na pia namsihi mwandishi atakayekwenda kutafuta ukweli aangalie sana ASIHONGWE/ ASIPEWE RUSHWA NA KUFICHA UKWELI yeye na atumaini dua toka kwa watumiaji wote wa tigo pesa na fadhila ya malipo ya Allah kwani malipo ya mola wake hayaishii duniani tu bali yatamfaa hata kesho kaburini na siku ya hukumu mbele ya mola wake
 
Back
Top Bottom