Watawala wetu wameshindwa hata hili?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
5.jpg

Kila Jumamosi wananchi wa Sierra Leona wanatumia siku hiyo kufanya usafi wa nchi yao na kuirudishia sura nzuri hasa baada ya uchafu uliokithiri kufuati vita vya wenyewe kwa wenyewe. Siku hiyo hakuna magari madogo n.k na watu wanajitolea na wengine hulipwa katika jitihada za kuondoa uchafu, kuzibua mifereji, kuondoa taka katika mitaa ya miji ya nchi hiyo.

Wananchi wa Sierra Leone ambao ni weusi kama sisi (if you didn't notice) wanafanya hivyo kwa sababu viongozi wao na wao wenyewe wamehamasika katika kuhakikisha kuwa nchi yao inapendeza.

Sasa najiuliza hivi viongozi wetu sisi wameweza kuhamasisha nini katika kufanya miji yetu iwe safi na mazingira yetu kuwa bora? Kwanini kila kitu lazima kifanywe kwa malipo? Hivi ule moyo wa kujitolea ambao tuliiona hasa miaka ya sabini ambapo wananchi walikuwa wanajitolea hata kulima mashamba (nakumbuka kule kijijini tulikuwa na shamba lililoitwa la "kujitolea").

Nakumbuka tuliwahi kujaribu kuwa na jumamosi za kufanya usafi wakati wa Ally Hassan Mwinyi sijui tuliishia wapi? Hivi kweli kila kitu lazima kifanywe na serikali au NGO? Ni lini wananchi wataacha kulilia "manispaa" na kuanza kufanya "vitu vyao"? Na ni lini watawala wetu wataamua kuongoza katika jitihada za kufufua moyo wa kujitolea?

Au mambo ya kujitolea na kufanya vitu kwa sababu ya mapenzi ya vitu vile ni baraka ya wazungu na bahati ya watu wa magharibi? Binafsi sijui ni nini kwani hata fisadi meya wetu hapa the D mara moja wanashiriki katika jitihada za kusafisha jiji la Detroit.

Labda nafananisha Tanzania na Marekani sana.. but what about Sierra Leone, yaani hata Siera Leone wanatuzidi kwenye mambo haya?
 
Hapa kwetu kwa kuwa viongozi wamekosa uzalendo hakuna mwananchi ambaye atakuwa tayari kufanya kazi ya kujitolea ile hali haoni faida za hiyo serikali kuwepo kwani kila siku wanatuibia pesa na kuzipeka kusikojulikana .

Tanzania inawezekana kama tuu viongozi wataacha ufisadi na kuwatumikia wananchi wa taifa hili.
 
MKJJ,

1. Umenigusa sana haswa moyo wa watu kujitolea ktk kutunza mazingira Tz!

Hii inabidi ianze kwa ngazi za chini haswa ktk shule za Primary na Sekondari wanafunzi kujengwa moyo wa kujitolea ktk vikundi kama Scouts, mazingira n.k

In 1995 nakumbuka pale mifreji ya Ubongo maji Mzee Makamba akiwa RC alituonyesha mfano tulisafisha mazingira yale na yeye for over 3 hours kwa kujitolea!

2. Pia elimu ya mazingira kwa jamii ni muhimu sana- watu Dar hula machungwa na kutupa tu masalia ovyo2 tu hata in CBD kule posta! Je umeona watu wanakunywa maji na kutupa chupa kila mahali? Yet hakuna hata mzazi anayemkaripia mtoto kufanya hivi sii sahihi!

Kujitolea kwa nchi yako ni njia kuonyesha uzalendo wako!

Hii inawezekana- vingozi wanyeshe tu mfano kwanza!
 
Hapa kwetu kwa kuwa viongozi wamekosa uzalendo hakuna mwananchi ambaye atakuwa tayari kufanya kazi ya kujitolea ile hali haoni faida za hiyo serikali kuwepo kwani kila siku wanatuibia pesa na kuzipeka kusikojulikana .

Tanzania inawezekana kama tuu viongozi wataacha ufisadi na kuwatumikia wananchi wa taifa hili.

Na hilo ndilo ninalolihofia. Kwa wale wanaokumbuka "Political Economy" ilisemwa hivi kuhusu maisha chini ya mfumo wa Kibepari kuwa "everybody for himself but God for us all". Baada ya miaka kadhaa katika nchi za kibepari, nimegundua kuwa hawa jamaa wanaishi kijamaa kuliko wajamaa wenyewe!

a. Wanafanya kazi nyingi za kijamii kwa kujitolea
b. Na wanapokutwa na majanga hawaendi kuomba misaada nje bali wanajitolea wao wenyewe kila walichonacho. Mfano wa Katrina uko karibu.
c. Pamoja na ubepari wao wanapenda kushirikiana sana utadhani wanaishi katika "kijiji cha ujamaa".

Ubepari ambao upo sasa hivi una mlengo wa kati sana kuliko ulivyokuwa miaka ile ya sitini na kwa kadiri mambo yanaendelea ndivyo inavyoonekana maisha ya kiliberali kama ya nchi za Scandinavia ndio yanapata mwelekeo zaidi.

Watanzania, kutokana na kukubali ufisadi na uongozi mbovu tumekubali kuwa "mambo ndivyo yalivyo". Sitashangaa hivi karibuni mtasikia wazungu wanakuja kutuanzishia NGO ya kusafisha mitaa yetu kama haipo bado.

Ni utumwa wa mawazo au ubeberu wa kifikra?
 
5.jpg

Kila Jumamosi wananchi wa Sierra Leona wanatumia siku hiyo kufanya usafi wa nchi yao na kuirudishia sura nzuri hasa baada ya uchafu uliokithiri kufuati vita vya wenyewe kwa wenyewe. Siku hiyo hakuna magari madogo n.k na watu wanajitolea na wengine hulipwa katika jitihada za kuondoa uchafu, kuzibua mifereji, kuondoa taka katika mitaa ya miji ya nchi hiyo.
Kauli zingine kwa kweli zinatia kinyaa,"Watawala wetu wameshindwa hata hili?" Sioni mantiki yake katika kuboresha mazingira ya Jiji, Manispaa, Halmashauri za miji na vitongoji. Wananchi mpaka leo hii wapo tayali kushiriki katika kusafisha miji yao pale inapobidi. Kuna mifano chungu nzima katika usafishaji wa miji, vitongoji na mitaa.

Tanzania tokea mwaka 1992 mpaka mwaka 2002 imekuwepo katika mpango wa miji endelevu ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kuwapa nafasi kubwa wananchi kutambua kero zao na kuweza kuzitafutia uvumbuzi. Mafanikio ya mpango huo ni makubwa ambayo yanawezesha wananchi kujipangia ni nini kifanyike kwanza katika vitongoji vyao.

Wakati wa utekelezaji wa mpango huo wananchi wengi walishiriki katika kusafisha mazingira yao bure, na baada ya kufanikisha hilo, ili mpango uendelee (endelevu) ndipo kukazaliwa vikundi vya usafi katika jamii na maendeleo mengine chini ya CBO, kukazaliwa NGO za usafi na mambo mengine.

Huko Sierra Leone, kwa sasa lazima wafanye hivyo, kwani nchi ndio kwanza inatulia kutoka kwenye machafuko ya mara kwa mara,lazima miji yao ni michafu kupindukia kiasi kwamba pasipo kushirikisha wananchi kufanya usafi na kutambua umuhimu wa usafi miji hiyo itaoza. Hatua ambazo kwetu zimeshapitiwa miaka mingi iliyopita.

MKJJ,

Hii inawezekana- vingozi wanyeshe tu mfano kwanza!
Haya mambo ya viongozi waonyeshe mfano katika usafi kwa maneno mengine unahitaji kiongozi aje kukusafishia choo chako. Usafi huanzia nyumbani kwako. Iwapo Nyumba yako ni safi sio rahisi kushindwa kushiriki katika kuweka mtaa wako safi.
 
Hii nimeipenda sana, lakini kwa hali iliyopo siwezi kujitolea kwani kile kidogo tu ninachojitolea kwa njia ya kodi kinafisadiwa na kupelekwa nje.

sasa hivi mafisadi ndio hujitolea pesa zilezile yaliyoiba
 
Kauli zingine kwa kweli zinatia kinyaa,"Watawala wetu wameshindwa hata hili?" Sioni mantiki yake katika kuboresha mazingira ya Jiji, Manispaa, Halmashauri za miji na vitongoji. Wananchi mpaka leo hii wapo tayali kushiriki katika kusafisha miji yao pale inapobidi. Kuna mifano chungu nzima katika usafishaji wa miji, vitongoji na mitaa.

Tanzania tokea mwaka 1992 mpaka mwaka 2002 imekuwepo katika mpango wa miji endelevu ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kuwapa nafasi kubwa wananchi kutambua kero zao na kuweza kuzitafutia uvumbuzi. Mafanikio ya mpango huo ni makubwa ambayo yanawezesha wananchi kujipangia ni nini kifanyike kwanza katika vitongoji vyao.

Wakati wa utekelezaji wa mpango huo wananchi wengi walishiriki katika kusafisha mazingira yao bure, na baada ya kufanikisha hilo, ili mpango uendelee (endelevu) ndipo kukazaliwa vikundi vya usafi katika jamii na maendeleo mengine chini ya CBO, kukazaliwa NGO za usafi na mambo mengine.

Huko Sierra Leone, kwa sasa lazima wafanye hivyo, kwani nchi ndio kwanza inatulia kutoka kwenye machafuko ya mara kwa mara,lazima miji yao ni michafu kupindukia kiasi kwamba pasipo kushirikisha wananchi kufanya usafi na kutambua umuhimu wa usafi miji hiyo itaoza. Hatua ambazo kwetu zimeshapitiwa miaka mingi iliyopita.

Haya mambo ya viongozi waonyeshe mfano katika usafi kwa maneno mengine unahitaji kiongozi aje kukusafishia choo chako. Usafi huanzia nyumbani kwako. Iwapo Nyumba yako ni safi sio rahisi kushindwa kushiriki katika kuweka mtaa wako safi.

point well taken, lakini wananchi wanahamishwa kujitolea kwa kiasi gani? Ni mipango gani ambayo inafanywa isiyohusisha kulipana?
 
Hivi kweli kila kitu lazima kifanywe na serikali au NGO? Ni lini wananchi wataacha kulilia "manispaa" na kuanza kufanya "vitu vyao"? Na ni lini watawala wetu wataamua kuongoza katika jitihada za kufufua moyo wa kujitolea?
Unajua Mwanakijiji, kusema "Ni lini wananchi wataacha kulilia "manispaa" na kuanza kufanya "vitu vyao"? ni offence kwa wananchi! Si kweli hii kitu. Na hii ndio inarudisha-morale nyuma...

Mfano tu, Wiki jana tu, nimeshuhudia wazalendo waishio Kawe wilaya ya Kinondoni, walikuwa wakizibua mifereji(mtaro) iliyokuwa inachafua mazingira ya maeneo hayo. Kilichonifanya nijue ni kwasababu walifunga njia kwa upande mmoja na kuruhusu magari upande mwingine kuwawezesha kufanikisha zoezi hilo. Nitachoweza kusema tu ni kuwa, mahali pale palikuwa pakitoa harufu mbaya sana, lakini wananchi wengi sana wa maeneo yale walikuwa wakibeba ndoo na kupokezana kubeba uchafu huo kusafisha eneo hili. Wakinamama, wakina baba wote walikuwa wakishughulika. Mimi nadhani watu wanajitolea sana, ni kwavile hatusikii kwenye vyombo vya habari.
 
5.jpg

Kila Jumamosi wananchi wa Sierra Leona wanatumia siku hiyo kufanya usafi wa nchi yao na kuirudishia sura nzuri hasa baada ya uchafu uliokithiri kufuati vita vya wenyewe kwa wenyewe. Siku hiyo hakuna magari madogo n.k na watu wanajitolea na wengine hulipwa katika jitihada za kuondoa uchafu, kuzibua mifereji, kuondoa taka katika mitaa ya miji ya nchi hiyo.

Wananchi wa Sierra Leone ambao ni weusi kama sisi (if you didn't notice) wanafanya hivyo kwa sababu viongozi wao na wao wenyewe wamehamasika katika kuhakikisha kuwa nchi yao inapendeza.

Sasa najiuliza hivi viongozi wetu sisi wameweza kuhamasisha nini katika kufanya miji yetu iwe safi na mazingira yetu kuwa bora? Kwanini kila kitu lazima kifanywe kwa malipo? Hivi ule moyo wa kujitolea ambao tuliiona hasa miaka ya sabini ambapo wananchi walikuwa wanajitolea hata kulima mashamba (nakumbuka kule kijijini tulikuwa na shamba lililoitwa la "kujitolea").

Nakumbuka tuliwahi kujaribu kuwa na jumamosi za kufanya usafi wakati wa Ally Hassan Mwinyi sijui tuliishia wapi? Hivi kweli kila kitu lazima kifanywe na serikali au NGO? Ni lini wananchi wataacha kulilia "manispaa" na kuanza kufanya "vitu vyao"? Na ni lini watawala wetu wataamua kuongoza katika jitihada za kufufua moyo wa kujitolea?

Au mambo ya kujitolea na kufanya vitu kwa sababu ya mapenzi ya vitu vile ni baraka ya wazungu na bahati ya watu wa magharibi? Binafsi sijui ni nini kwani hata fisadi meya wetu hapa the D mara moja wanashiriki katika jitihada za kusafisha jiji la Detroit.

Labda nafananisha Tanzania na Marekani sana.. but what about Sierra Leone, yaani hata Siera Leone wanatuzidi kwenye mambo haya?

Mwanakijiji:

Kujitolea au watu kuwa na motisha sio kitu cha daima katika jamii. Huwezi kuwaambia watu wajitolee wakati juhudi zao nyingine hazieleweki zinakwenda wapi.

Kujitolea mara nyingi kuna kwenda na matumaini. Ukibadilika uongozi mara nyingi matumaini ya watu yako tayari kufanya kazi za kujitolea. Lakini siku zinapozidi kwenda ni lazima watu waone matunda ya juhudi zao na kama matunda hayaonekani watu watakuwa wavivu tu.

Siera Leone imetoka kwenye vita si miaka mingi na matumaini ya watu ni makubwa. Lakini tusitegemee miaka miwili inayokuja watu kuendelea kufanya kazi kujitolea wakati viongozi wanakula pesa bila mpango.

Eritrea ilipopata uhuru kutoka Ethiopia wananchi walifufua reli iliyokufa kwa zaidi ya miaka ishirini kwa mikono yao na bila msaada kutoka nje lakini leo sidhani kama watu wanaweza kufanya miradi ya aina hiyo bila malipo.

Kikwete alivyoingia madarakani alitushawishi watu kuwa tunaweza kurudi nyumbani kufanya kazi za kujenga taifa. Lakini yayoendelea sasa sidhani kuna mtu anaweza kuacha kubeba mabox na kurudi nyumbani kichwa kichwa.
 
point well taken, lakini wananchi wanahamishwa kujitolea kwa kiasi gani? Ni mipango gani ambayo inafanywa isiyohusisha kulipana?
Kwanza tukubaliane kuwa kujitolea sio jambo endelevu, ni sawa na operesheni fulani ambayo hufanyika katika muda fulani kwa lengo la muda huo. Baada ya hapo ni nini kinafanyika? Jibu ni hakuna kitu zaidi ya kusubiri kujitolea tena muda mwingine.

Kujitolea katika Tanzania ya leo ni kama motisha ya kufikia lengo fulani. Katika upande wa utunzaji wa mazingira ya miji, kujitolea kumeendelea kutoa changamoto kwa watendaji wa kila siku wa utunzaji wa mazingira. Hii imetokana na kuwepo na siku ya mazingira ambapo katika siku hiyo Mji safi kabisa hupata zawadi na kutangazwa nchi zima. Kupitia wiki ya mazingira wananchi wengi wamejikuta wakijitolea katika kusaidia shughuli za usafi ili kuweza kushinda na kuwa mji safi.

Miji ambayo ilikuwa ni maarufu kwa usafi katika Tz kama Arusha sasa imejikuta kuwa inapata ushindani mkubwa toka katika mji inayokuwa kwa sasa. Hii imetokana na wanachi wenyewe kujua umuhimu wa utunzaji wa mazingira, aidha mashindano ya usafi yamewezesha wananchi kwa muda fulani kujitolea kushiriki katika usafi.
y1pIjS-ngexYeUuAxERGmUhdUu1QjpK6C7x3yaQ_vPNiIQ8dCC8-2EkoBYt39L_3K28iPD5IomorWg

Wadau toka nchi mbalimbali wakijifunza mbinu za kuweka mji safi toka kwa CBO mojawapo Jijini Mwanza
 
yeah.. Kibungano.. you just confirmed my point..

Kuna mtu anaweza kuhisi huyo mtasha anasema nini:

Mtasha: "huu uchafu haufahi kuwa mjini namna hii jamani"

Mbongo mwenye Kilemba: "Hii ni kawaida yetu"

Jamaa mwenye shati jeupe: "Inalipa hii?"
 
Halafu akija mtu kama Augustine Mrema akaanzisha ulinzi wa kujitolea sungusungu somebody by the name of Mwanakijiji atakuja na swali " Kwanini tulinde sungusungu wakati kazi za ulinzi na usalama ni za serikali na tunazilipia kupitia kodi zetu"?

Nyie ma Arm-chair Generals hamuishi kushift goal posts Govt cant score!
 
by now you should know that I don't fit in your box.. hivyo usijaribu kufikiri nitasema nini, I'm the only one who knows!
 
Halafu akija mtu kama Augustine Mrema akaanzisha ulinzi wa kujitolea sungusungu somebody by the name of Mwanakijiji atakuja na swali " Kwanini tulinde sungusungu wakati kazi za ulinzi na usalama ni za serikali na tunazilipia kupitia kodi zetu"?

Nyie ma Arm-chair Generals hamuishi kushift goal posts Govt cant score!

Masatu:

Mtu akalinde sungusungu na kirungu wakati Jambazi ana SMG aka AK47. Ndio maana watu hawataki kusikia upuuzi mwingine wa kujitolea.
 
Mkjj, wako busy wanakusanya utajiri kupitia nyadhifa zao hivyo hata muda wa kuhamasisha wananchi hawana kabisa.
 
Tatizo kubwa kwetu sisi ni kwa sababu hatufuati sheria. Tungekuwa na serikali inayofuata sheria, basi swala la usafi wa mazingira lingekuwa ni la kisheria na kila mtu angelazimika kufuata masharti ya usafi wa mazingira.

Huko Singapore, usafi wa mazingira ni la kisheria. Ukitupa kishungi cha sigara barabarani, adhabu yake ni viboko 10 papo kwa papo. Ukitema chewing gum barabarani unapata bakora papo kwa papo. Ingawa adhabu hizi ni za kikatili, hiyo ndiyo ilivyo sheria yao na watu wote waniafuata.

Kwa hiyo usafi wa mazingira siyo swala la kujitolea ila ni wala la kisheria.
 
Back
Top Bottom