Watawala wetu wachafu wanavyopenda utukufu!

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3]Chanzo: Freethinking Unabii (mpayukaji blog)[/h]

6bd0207326c79270c461d709a5346659.article.jpg

Ethel Mutharika Mausoleum Thylo Malawi

Jiulize ni mamilioni mangapi ya kwacha hata dola yameteketezwa kwenye kujenga jumba hili ambamo amezikwa rais wa zamani wa Malawi Bingu wa Mutharika? Zidi kujiuliza: ni pesa kiasi gani imeshaunguzwa nchini Kenya kuhifadhi mwili wa rais wa kwanza wa nchi hiyo Mzee Jomo Kenyatta tangu afariki mwaka 1978? Jiulize ni pesa kiasi gani ilteketea kwenye kujenga mji wa Gbadolite kijijini kwa mwizi wa zamani wa DRC Joseph Desire Mobutu au kanisa kubwa (kuliko la Mt. Petro la Roma) huko Yamoussoukro kijini mwa rais wa kwanza wa nchi ya Ivory Coast , Felix-Houphet Boigny na upuuzi mwingine mwingi uliotapakaa barani Afrika? Hakika watawala wetu wachafu wanapenda utukufu kwa utukutu wao na ujambazi wao.
2715b4b9.jpg

Baadhi ya majengo katika kijiji cha Gbadolite huko DRC yaliyojengwa na Mobutu na yasikaliwe na watu.

315287530_LVbWK-L-1.jpg
KKanisa kubwa la Yamoussoukro huko Ivory Coast.
 
Back
Top Bottom