Watanzania Wenzangu Naomba Tuwe Wazalendo...

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Aug 6, 2009
5,101
1,946
Wana JF,

Nimesikiliza kipindi cha Idhaa ya Kiswahili ya BBC "Dunia Yetu Leo Jioni" muda mfupi uliopita. Kuna mfanyabiashara wa Burundi analalamika mizigo inavyoibiwa bandarini Dar es Salaam kiasi kwamba wanaona bora waanze kutumia bandari ya Mombasa japo ni aghali kwa sababu ya umbali.

Swali la kujiuliza, ni kweli wizi bandarini hauwezi kuzuilika? Viongozi wa TRA (nawalaumu kwa kuchelewesha "clearance" ya mizigo ambayo ni sababu ya wizi kufanyika) na wa TPA wanajisikiaje wanaposikia mambo kama haya? Uzoefu wangu binafsi umenionyesha maamuzi ya ajabu ambayo hutayakuta nchi nyingine - na siongelei nchi za Ulaya au Marekani ni hapa hapa Afrika.

Mtanzania unajisikiaje moyoni unapofanya maamuzi yatakayoumiza kizazi chako mwenyewe? Wahindi wanapewa vibali vya kufanya kazi za ukarani, kuna wachina wana vibali vya kuuza nguo za mitumba, kuna wageni (hadi Wanaijeria) wanapewa passport za Tanzania). Hata kama ni njaa hii yetu imezidi.

Viongozi hawa WABOVU tunaowalalamikia ni "reflection" ya jamii yetu wenyewe ndio maana tunawaweka madarakani (hata kama ni kwa kuwasaidia kuiba kura na kuhongwa) NA KUTETEA MADUDU wanayofanya kila siku. Kwenye jamii ya waongo hakuwezi kutokea kiongozi mkweli. JAMA TUBADILIKE!
 
Back
Top Bottom