Watanzania Wengi ni Wavivu? The Moment of Truth!

Tanzania haina vipimo vya kazi.Wala sizungumzii upuuzi kama Opras no. Hebu anagalia kiongozi anaweza kufanya jambo lisilo na tija , likailetea nchi hasara lakini hakuna wa kumwuliza matokeo ya alichofanya. Hivyo hivyo huko maofisini kwao hamna uwajibikaji na hakuna wa kumwuuliza mwienzake maana wote wako hivyo hivyo.

Mimi napiga kazi mahali fulani , najituma sana kibinafsi maana nimeona wenzetu huko nje wanavyofanya, ila sehemu hii ya kazi inaboa sana . Wakuu ni wabinafsi, wana upendeleo wa wazi wazi na mishahara sio even . Mimi na kimaster changu naona upuuzi, nimeamua kufanya biashara ambayo natumia muda wao mwingi kuimonitor. Sababu ni kuwa haka kabishara kananijali zaidi kuliko mwajiri wangu wa sasas. This is how life is in Bongo.

Una point ndugu.

Bila kukuhukumu wala nini, je unaonaje kama ungeacha kazi hapo ili ama uwe na muda zaidi na biashara yako au utafute mwajiri mwingine anayekujali.Nadhani kuendelea kuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje hujitendei haki wewe mwenyewe wala huyo mwajiri asiyekujali.Huenda kuondoka kwako pia kungempa mtu mwingine nafasi.
Samahani lakini.
 
Tanzania haina vipimo vya kazi.Wala sizungumzii upuuzi kama Opras no. Hebu anagalia kiongozi anaweza kufanya jambo lisilo na tija , likailetea nchi hasara lakini hakuna wa kumwuliza matokeo ya alichofanya. Hivyo hivyo huko maofisini kwao hamna uwajibikaji na hakuna wa kumwuuliza mwienzake maana wote wako hivyo hivyo.

Mimi napiga kazi mahali fulani , najituma sana kibinafsi maana nimeona wenzetu huko nje wanavyofanya, ila sehemu hii ya kazi inaboa sana . Wakuu ni wabinafsi, wana upendeleo wa wazi wazi na mishahara sio even . Mimi na kimaster changu naona upuuzi, nimeamua kufanya biashara ambayo natumia muda wao mwingi kuimonitor. Sababu ni kuwa haka kabishara kananijali zaidi kuliko mwajiri wangu wa sasas. This is how life is in Bongo.

Mfamaji, unachokifanya ndicho Watz wengi ambao ni 'successful' wanakifanya pia. Yaani, mazingira ya kazi zetu yanatufanya tuwe na kazi mbadala. La sivyo, 'you'll die poor'. Si kitu kizuri lakini ndivyo mfumo wenyewe wa kazi hapa Tz ulivyo.
 
Mwenye kazi haelewi umuhimu wa kazi mpaka anapofukuzwa kazini
Thanks Elusive,
Na kwa kuongezea tu ni kwamba, tuna kawaida ya kulalamikia kazi/ajira na waajiri wetu kuwa hawatujali lakini bado tunang'ang'ania ajira/waajiri ambao hawatujali.Inakuwaje hii? If one thinks s/he is good enuf why not walk out and sell your labour elsewhere for a premium price? Wengi wenye sifa hizo huondoka na kupata ajira bora zaidi na maslahi mazuri kwenginewe.Wanaobaki mimi naona wanawaibia waajiri wao ( hulipwa ujira bila kufanya kazi).Tupende au tusipende kila ajira ina makubaliano.Ufanye kazi fulani kwa ujira fulani na ni hiari.Ukiona haifai una hiari kuanza mbele.
 
WaTanzania sisi Ni wavivu sana, kwa kukuhakikishia hebu hapo ulipo kama unaweza kutizama nje, ama waeza kutoka nje na kuangalia wapitao njiani utaona jinsi wanavyotembea kivivu. mtu hana haraka wala malengo ya aendako.
Umegaragaza ile mbayaa.
 
Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk

Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?

Zingatia yafuatayo ambayo kwa wengi wanajua ukweli wake:

  • Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.
  • Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.
  • Lunch time inachukua si chini ya saa moja.
  • Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda
  • Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.
  • Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.
  • Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu
  • Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.
  • Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.
  • Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.
n.k, nk.

Kuna kiongozi mmoja wa kazi katika shirika aliwahi kusema, wanaofanya kazi kwa kuwajibika wakati wote ni kama asilimia tano tu. Katika asilimia 100% ya muda wa kazi, heunda ni asilimia 50% tu inatumika kwa kazi.

Je, shida yetu ni nini hasa? Tuwe wa kweli. Watanzania Wengi ni Wavivu? Nini kifanyike?

Inasikitisha sana
Inasononesha sana
Inafadhaisha sana

Watanzania sio wavivu. Matatizo ni kuwa mnawapangia expectations zenu ambazo mnaita maendeleo bila kuelewa wao wana expectations zao vilevile katika maisha.

Kiongozi anapokwenda kijiji na kuwaambia wananchi wajitolee kujenga shule, je hizo ni expectations za wananchi au za kiongozi?

Nilipokuwa shule nilikuwa mvivu wa kutupwa kwa sababu expectations zangu zilikuwa kupata maarifa na sio kufanya kazi za elimu ya kujitegemea ambazo nilishajifunza nyumbani tayari.
 
Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk

Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?

Zingatia yafuatayo ambayo kwa wengi wanajua ukweli wake:

  • Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.
  • Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.
  • Lunch time inachukua si chini ya saa moja.
  • Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda
  • Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.
  • Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.
  • Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu
  • Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.
  • Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.
  • Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.
n.k, nk.

Kuna kiongozi mmoja wa kazi katika shirika aliwahi kusema, wanaofanya kazi kwa kuwajibika wakati wote ni kama asilimia tano tu. Katika asilimia 100% ya muda wa kazi, heunda ni asilimia 50% tu inatumika kwa kazi.

Je, shida yetu ni nini hasa? Tuwe wa kweli. Watanzania Wengi ni Wavivu? Nini kifanyike?

Inasikitisha sana
Inasononesha sana
Inafadhaisha sana

hapa nakuunga mkono kwa hoja yako ya watanzania kuwa wavivu.
asilimia 90 ya watanzania ni wavivu.
maana utakuta kama mtu una dilizako za kutafuta ela na unakuwa na mishemishe nyingi za hapa a pale watu hapa bongo watakucheka , kukukejeli na kukushangaa.
ndio maana utakuta wachaga wengi wanafanya kazi kwa bidii na kufanikiwa kimaisha mwisho wake wanaambiwa wachaga wezi.kumbe wakati wachaga wanatafuta maisha bora kwa kufanya kazi kwa bidii wengine walikuwa wamelala usigizi!!
 
Hebu ngojeni kwanza. Tusiwe haraka wa kunyooshea vidole mambo ambao siyo kigezo sahihi cha kutufanya tuonekane wavivu.

Allien,

Hayo yote uliyo orodhesha mbona yanaendelea ughaibuni pia! Tena ughaibuni wafanyakazi wanatumia advantage ya flexible hours na laidback policies kufanya mambo yao muda wa kazi. Ukifanya kazi kwenye makampuni makubwa (over 10,000 employees) utakutana na flexible hours na laidback policies kibao.

Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.

Unazungumzia kuchelewa bongo, ughaibuni wafanyakazi wana abuse flexible hours policies kwa sana tu. Wengi wanafika kazini nusu mpaka robo tatu saa baada ya muda waliopanga. Halafu hutumia robo mpaka nusu saa cafeteria kutafuta kifungua kinywa.

Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.

Pengine ughaibuni huwa hawaendi kwa chai ya pili, lakini wana robo saa kibao za mapumziko ya uvutaji sigara. Pamoja na hayo mpumziko, bado kuna vimatembezi vifupi huko nje vya kunyoosha miguu

Lunch time inachukua si chini ya saa moja.

Asilimia kubwa ya wafanyakazi ughaibuni urudi kwenye cubicles robo saa baada ya lunch break kwisha.

Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda

Haaa Allien, hawa wenzetu huwa wanaanza kupiga soga za ‘supposedly’ jinsi watoto wao walivyo smart saa moja kabla muda wa kuondoka.

Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.

Well, hapa ni kweli. Huko kwetu kwa visemina visivyo na mpango tu hatujambo. Lakini hata hawa wenzetu huwa wana vi-training kibao ambavyo matumizi yake ni ya mbali sana.

Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.

Hivyo vihadithi hata ughaibuni vinapigwa sana tu. Movies, sports, celebrity lifestyles, cars, na family funs ni gumzo zinazoendelea muda wote makazini

Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu

Si afadhali bongo simu tu; ughaibuni simu, internet, desktop et la ni company resources ambazo zinakuwa abused sana tu.

Wengi wetu humu JF tunatumia computer na internet za makazini mchana kutwa kushinda hapa kijiweni...shhhhh chonde usiseme kwa nguvu, tusije tukamwaga unga bure...

Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.

Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.

Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.

Pengine hii ndio pointi kubwa inayotofautisha Bongo (na nchi nyingine zinazoendelea) na nchi zilizoendelea.

Unajua, pamoja na kwamba mambo mengi yanayoendelea makazini bongo na ughaibuni yanafanana, wenzetu wanajua jinsi ya ku-make up their lost time. Watachelewa kuja kazini, watachukua vibreak visivyo na mpango, na kupiga story; lakini siku zote wanajua ni jinsi gani watafidia huo muda ili kuweza kuwasilisha report katika muda uliopangwa. Hutasikia ooh sijui naomba masaa 24 mengine nimalizie wala nini. Muda ukifika report hiko mezani…tena imekamilika kama inavyopaswa. Hapa ndipo tofauti kubwa ilipo kati workforce ya nchi zinazoendelea na zilizoendelea.
 
Mimi nadhani ni utamaduni uliopelekewa na ukosefu wa kazi na misingi ya kufufua ajira kwa wananchi...Ukosefu wa shughuli za uzalishaji na kilimo bora ambako kumesababishwa na uongozi wa bora liende...Nakubaliana na Zakumi hapo juu...Pia ni lazima tukubali kuwa kazi hakuna...Tena nadhani afadhali sasa hivi...Kazi hakuna jamani na uwezekano wa kupata kazi kama huna connection haupo...Najiuliza sana kama ni watu wa aina gani tuko hapa JF...Inawezekana ni watu wenye priveledges ama hawakutokea kwenye mshike mshike za maisha ambayo hujui future yako ikoje....Sasa kama huji future yako utajuwa vipi unapokwenda wakati wa kutembea?
Si ndio maana hata wazungu wanapenda usemi wetu kuwa NO HURRY IN AFRIKA?

Ni utamaduni ambao ni lazima tupate viongozi bora wenye kulielewa tatizo na ndio tunaweza kulimaliza tatizo hilo.
Imekuwa kama utamaduni kiasi kwamba watanzania hawaoni umuhimu wa kuwa na kazi kwasababu hawaamini kuwa ziko na hata kama ziko hakuna uzoefu unaoonyesha kuwa watu huajiriwa kutokana na uwezo ama profession zao kwenye field husika....Na pia self esteem iko to the lowest na ndiyo maana unakuta wakenya wanakuja kuchukuwa kazi.

Tatizo hili tutaweza kulimaliza ikiwa ahadi kama zinazotolewa hivi sasa kuwa wakulima watawezeshwa nk...Na kweli ikaonekana kuwa kuna nia ya kufanya hivyo...Basi jamii yetu eventually itabadilika.

Siasa za ujamaa zilitulemaza kiasi pia kwani mali ya umma ni mali ya umma na haina mwenyewe...Na ninarudia kuhusu utamaduni kwani ndio maana unaona kuna utaratibu wa pesa za umma kutumika kwa minajili isiyounufaisha umma kama ilivyokuwa kwa pesa za ruzuku pamoja na ufujaji especially kwenye mashangingi nk.
 
Inashangaza mtu analaumu usimamizi mbovu ama serikali haina system ya kusimamia ufanisi, hivi hata kwenye shughuli zetu wenyewe tusimamiwe ama tuwekewe mfumo ndio tujali muda?????,
hapo juu nimezungumzia watu kutembea kivivu bila kujali muda hiyo ni sehemu ndogo ya kuonesha kwamba uvivu umo ndani yetu waTanzania. ingia ndani ya daladala yaani utastaajabu mtu anashindwa kusimama wima anaegemea hovyo utafikiri labda ni mgonjwa, kumbe sio na si mmoja ni karibu wote wako hivyo. nimetembea kidogo sehemu za nchi majirani, huwezi thubutu kumuegemea mtu kabisa yaani utatizamwa kama uliyejinyea.
 
Inawezekana kusema kuwa Watanzania wengi ni wavivu na usiishie hapo tu ni vema ukafafanua zaidi uvivu huo unapatikana katika maeneo yepi ya Tanzania. Kwa mfano watendaji wengi wa idara serikalini ni wavivu ama kwa makusudi ama kutokana na desturi zao.

Kwa mfano ukiwa mfanyakazi wa SMZ lazima utakuwa mvivu tu, na inatokana na desturi zao katika maisha yao. Kwa mfano kwenda sokoni ni jukumu la mwanaume. Soko linafunguliwa saa moja asubuhi na kufungwa saa tisa mchana. Kuingia kazini ni saa moja na robo na kutoka ni saa tisa mchana. Hakuna lunch break rasmi, lakini wafanyakazi wana lunch break, wana coffee break na zaidi wana kwenda marikiti kutafuta kitoweo na kukipeleka nyumbani kabla ya kurudi tena kazini.

Moja ya sifa za Maalim Seif (CUF) alipokuwa waziri katika SMZ ni kuondoa tatizo hili la uvivu wa wafanyakazi, na kwa asilimia kubwa alifanikiwa, kwani pamoja na kuwa ni waziri alikuwa anafanya kazi ya uangalizi wa ofisi kwa kuhakikisha kuwa anawahi kufika kazini na honi(Zenj kuingia kazini na kutoka lazima usubiri honi kulia) inapolia kuwa sasa muda wa kazi umeanza yeye alikuwa anapiga mstali kwenye buku la kuandika muda wa kuingia kazini. Na wale wote ambao watakuwa wamechelewa walipatiwa barua za onyo. Alifanya hivyo karibu katika idara na ofisi zote za SMZ, na wafanyakazi kwa kipindi hicho walishika adabu zao.
 
Maeneo ya nchi yaliyo ndani ya bahari na pwani yote ya Tanzania kuanzania Tanga hadi Mtwara kwa umbali wa kilomita 150 kutoka usawa wa bahari ndiyo maeneo yaliyokithiri kwa uvivu. Wananchi wa Mtwara wanashindwa kulima nyanya na mboga hali inayowafanya wafanyabishara wananunue nyanya kutoka Iringa, Mbeya, Kilimanjaro na Arusha na kwenda kuunza Mtwara.

Ninalo shamba Bagamoyo, nemeshindwa kupata mfanyakazi wa shambani kutoka eneo hilo. Jamaa ni waongo, ukikubaliana nao kufanya kazi ya shamba wanakubali na mara zote wanaomba uwaachie pesa ya kununulia unga, lakini ukienda kesho yake hutamwona tena. Au hata akifanya kiwango chake ni cha hali ya chini mno. Nimelazimika kutafuta wafanyakazi nje ya eneo la kilomita 150 nimewapata na wanafanya kazi nzuri sana. Tumekuwa tukijiuliza maswali mengi kuhusu hii tabia, rafiki yangu akaniambia eneo hilo la kilomita 150 kutoka usawa wa bahari lina joto kali na na lina unyevu nyevu wenye chumvi chumvi kutoka baharini, ambayo imewafanya watu wa maeneo hayo kuwa na hitilafu fulani kiakili, kimatendo na kwao kila kitu ni sawa.
 
...labda serikali ibadili system, tuwe nasi tunalipwa kwa masaa tunayoyafanyia kazi.
mfano; kima cha chini,

tshs 1'000/- kwa saa moja * masaa 7.5 (saba na nusu) ya kazi
=tshs 7'500/- kwa siku

mtu huyo kwa wiki ataingiza

tshs 7'500/- kwa siku * siku 5 za wiki = 37'500/- malipo yake ya jumla kwa wiki

ambayo ni sawa na

tshs 37'500/- kwa wiki * majuma manne katika mwezi = 150'000/-

kinyume na hapo, haya mambo ya uhakika wa malipo mwisho wa mwezi, hata kama kila wiki mfanyakazi anavisingizio vya 'nimefiwa na shemeji yake mke wa jirani', nk hayatakwisha!

Mchongoma umemaliza kazi, kwani uliyoyaeleza hasa ndiyo mawazo yangu. Mfumo wa ajira kwa kutegemea masaa mtu aliyoyafanyia kazi ndiyo njia pekee itakayosaidia kunusuru uchumi wa nchi hii. Kuna maeneo ambayo yanaweza kulipwa kwa mwezi kama vile polisi, jeshi,walimu na mfano wa hao. Lakini kuanzia madaktari, manesi, wafanyakazi wa mabenki, Posta, nk walipwe kwa masaa watayayoyafanyia kazi. Kama mtu hajafika kazini basi asitegemee kuwa kuna pesa ya bure ambayo ataipata, kama mtu ametoka katika sehemu yake ya kazi na kwenda kunywa chai basi ajue kuwa muda ule ni wake binafsi na hatapata pesa ya bure. Kama mtu atachelewa kufika kazini ajijue kuwa uchelewaji wake hautamgharimu serikali mwajiri wake.

Hii njia ndiyo muafaka kwani itanyoosha kona-kona zote na kuondoa visingizio visivyokuwa na ulazima.
Ninahakika kama mfumo wa malipo kwa saa utaanzishwa Tanzania, basi nidhamu ya kazi itarudi na neno uvivu litapotea.
 
Thanks Elusive,
Na kwa kuongezea tu ni kwamba, tuna kawaida ya kulalamikia kazi/ajira na waajiri wetu kuwa hawatujali lakini bado tunang'ang'ania ajira/waajiri ambao hawatujali.Inakuwaje hii? If one thinks s/he is good enuf why not walk out and sell your labour elsewhere for a premium price? Wengi wenye sifa hizo huondoka na kupata ajira bora zaidi na maslahi mazuri kwenginewe.Wanaobaki mimi naona wanawaibia waajiri wao ( hulipwa ujira bila kufanya kazi).Tupende au tusipende kila ajira ina makubaliano.Ufanye kazi fulani kwa ujira fulani na ni hiari.Ukiona haifai una hiari kuanza mbele.

Where will you sell your labour, while nearly every place is like that? Siyo kweli unachokisema. Kuna watu wanafanyakazi kama punda lakini malipo ni kidogo sana. Chukulia, mfano, kuna kiwanda fulani niliambiwa wanafanya kazi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 1 jioni bila muda wa kupoteza, lakini nasikia malipo ni kidogo sana.

Na kuna sehemu nyingi tu hapa Tz: walinzi, polisi, nk. Kwani watu wakiondoka pale si wengine wataajiriwa na bado mazingira yatakuwa yaleyale? Na watu nadhani wanavumilia wakidhani siku moja hali itabadilika na hiki ndicho kinachofanya watu waendelee kukaa pale.

Pia kuna mabosi fulani unawakuta kila mara kupiga simu na kuandika kwenye laptops zao na huenda mara nyingi siyo kazi za ofisi. Lakini mshahara mkubwa sana pamoja na malupulupu mengine - nyumba, usafiri, simu, matibabu nk. na wakitaka kazi za ofisi wanamtuma secretary wao ku'type'.

Mimi nadhani mfumo wa kazi pamoja na sheria za kazi hapa Tz inabidi zirekebishwe ili zikidhi mahitaji ya Watz na pengine itasaidia kuondoa hili tatizo tunalosema 'Watz wengi ni wavivu'.

Mimi nilienda mahali fulani kama mmojawapo wa staff na nilikuwa nasimamia malipo ya wafanyakazi. Mshahara niliokuta ulikuwa mdogo sana na kila mara wafanyakazi walikuwa wanakuja kukopa hela. Mwishowe nikashauri wapandishwe mishahara lakini wakubwa fulani walikuwa hawataki kabisa.

Hili bwana ni tatizo kubwa. Watu wanapata faida kubwa sana lakini wanawalipa wafanyakazi wao kidogo sana. Na haitoshi kusema asiyeridhika aondoke. Nadhani ni vizuri tukatafuta njia ya kubadilisha hiyo hali ili maendeleo yapatikane zaidi.
 
...tatizo la ku clock-in and -out, kuna watu wata abuse tu hiyo system. sijui tumelogwa sie?

bado panahitajika hatua nyingine madhubuti za kusimamia uwajibikaji, mfano; mtu apangiwe masaa ya kazi kulingana na uzito wa kazi yenyewe.

Haiwezekani kwakuwa mtu ni bosi, basi anakuwa na secretaries wawili plus mfagia ofisi-cum-mpika chai wa bosi. Matokeo yake kutwa nzima unakuta porojo za upatu, rusha roho, sare za harusi nk...

ughaibuni ukiingia kazini, hata kama ni kubandika lebo za mikate, basi saa moja mpaka saa tisa wewe na lebo lebo na wewe, hata ukienda kulala nyumbani kichwa kinaendelea ku 'click-click-click!'

Bongo nenda kwenye kajiofisi kadogo tu, utitiri wa wafanyakazi 'uchwara' kibao, pale Imalaseko, Shoprite, Games, maofisi ya wizara,na mashirika ya umma, kote huko kumejaa watendaji uchwara kuliko wateja/wahudumiwa...

...lazima pawepo na mfumo wa kuweka viwango vya ukamilifu wa kazi kwa kila mfanyakazi kwa kipindi maalum, i.e clearly outlined Job descriptions & Job specifications.
 
Kwa yote yaliyoongelewa, je ni sawa tukizungumza kwa ujumla wake (General), kwamba wengi wa Watanzania ni Wavivu wa Kufikiri na Kutenda na wamekosa ubunifu?

Je ni sawa pia tukisema Watanzania Wachache waliofanikiwa (excluding Mafisadi), wamekuwa Wabunifu na Wachapakazi?

Ni nini kifanyike katika kuliwezesha "Kwa Uhakika" (No politics), kundi kubwa ili liweze kujiletea maendeleo ya kweli na kwa haraka?
 
Leo, Julai 1, 2010, ni siku ya kihistoria. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imezindua soko la pamoja (common market). Maana yake ni kuwa hivi sasa mipaka ya nchi wanachama wa EAC - Tanzania, Burundi, Kenya, Uganda na Rwanda imefunguliwa. Hivi sasa Mtanzania anaweza kwenda nchi yoyote ndani ya EAC kufanya kazi au kusoma kama raia wa nchi hiyo bila kuwa treated kama foreigner. Tayari Rais Kibaki wa Kenya ameamuru kuwa raia wa nchi wanachama wa EAC wasitakiwe kuwa na vibali vya kazi (work permits) ili kuweza kufanya kazi nchini Kenya. Ina maana kuwa leo hii Mtanzania anaweza kwenda Nairobi na kutafuta kazi bila tatizo lolote.

Swali linakuja, je Kenya ambao wenyewe wanapeana kazi kwa ukabila watampa kweli kazi Mtanzania?
Na Wakenya wanajullikana kuwadharau Watanzania eti ni wavivu, wazembe, hawajasoma na hawajui English. Mtanzania ataweza kupata kazi kirahisi Kenya, Uganda au Rwanda?

Kwa miaka kadhaa sasa sote tumeshuhudia jinsi Wakenya walivyojaa Dar es Salaam na kuchukua kazi hata kabla ya hiyo common market kuanza. We know them, they are everywhere. Wengine wanajidai eti ni Watanzania kutoka mikoa ya mpakani, au walisomea sana Kenya au mama ndiyo Mkenya na baba Mtanzania. Baadhi ya waajiri kwenye mahoteli, banks, insurance companies, etc wamekuwa wakiajiri Wakenya tangu zamani eti wakisema wao ni wachapa kazi na wanajua English.

Hapa kilichobaki sasa kwa Watanzania ni kuwa aggressive na kupambana kwenye hili soko la pamoja. Watanzania twendeni Nairobi, Kigali, Kampala na Bujumbura na CV zetu na vyeti vya chuo tukatafute kazi. Tusiogope, sisi ni watoto wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wenye kampuni nao wachangamke kwenda nchi nyingine za EAC kufanya biashara huko na kufungua matawi Afrika Mashariki.

Wakati ni huu!
 
watafurumushwa watatembea kwa mguu hadi kenya. watz tuna umoja na utaifa mzuri, na hatutakubali kudharauliwa na wakabila kama hawa. hili wala lisikutie shaka. cha ajabu ni kwamba, tunaenda kuvunjavunja ukabila wa Rwanda,kenya, burundi na uganda kwa njia ya kuungana vizuri...lakini tunaenda kuanzisha ukabila mwingine mkubwa sana utakaokuwa na influence sana kwenye uchaguzi na maamuzi mbalimbali, nao unaitwa UTANZANIA UKENYA,UUGANDA, URWANDA NA UBURUNDI. na watu watapeana kazi na madili kwa ukabila huu mpya utakaoanzisha. hii kitu haitakuja kuondoshwa kwa muda, hadi tuje kujisikia kama kitu kimoja kama ilivyo US, ni miaka si chini ya mia mbili ijayo.
 
Back
Top Bottom