Watanzania Wengi ni Wavivu? The Moment of Truth!

Kwa ukweli usimamizi wa kazi ni mbovu sana Bongo.
Wenzetu wana time-sheets na performance reviews hata kwa wabeba box!! Ukichelewa hata dakika kumi inakua noma! Ukifanya ndo tabia lazima uitwe na HR manager!! Cant even imagine eti uchomoke lisaa lizima ukanywe Chai! ukirudi hauna kazi.
Vilevile watu wana lead by example, ukimwona supervisor wako amekamata ufagio anasafisha duka unajua watu wako serious.
 

Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk

Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?


Na tutaendela kusema tu, na wavivu watakuwa wavivu tu

uvivu ni nature ya binadamu yeyote yule, tunataka viongozi wanaoweza kubadilisha hali hii, kuweka system zitakazowalazimisha hawa watu waishi kivingine.

Mfano nimefanya kazi vodacom, they dont care unaingia saa ngapi, unafanya nini, wanachotaka ni results, hii ilitufanya kufanya kazi mpaka late night, wanataka wewe u-deliver tu, kun baadhi ya watu walifanyia kazi nyumbani na kudeliver good jobs.

Mchezo wa kuweka daftari la kusign, na watu kuishia kucheza karata kwenye kompyuta imepitwa na wakati.

Nasema viongozi wana wanawajibika , kumbuka Mrema at that time... watu walipelekeshwa mpaka basi, we need leaders like them...... though bado wanatakiwa waweke system za kumonitor huyu mtu,

kuna watu wanaingia kazini mapema, na wanatoka late, they ave done zero work..

Vipi kuhusu piece work?? wengi nao wanatumia hii system, they pay you as per piece work

Vipi kuhusu kulipa kwa masaa?? mtu akimaliza task zake na kwenda kufanya kazi sehemu nyingine

pengine hao wanaokunywa chai-late, wanajua kabisa kazi yao inachukua masaa 2 tu, na anamaliza anasifiwa.Same person kama ataambiwa analipwa kwa masaa na yuko free baada ya kumaliza, angeenda haraka kufanya kazi na kama ana akili anahamia sehemu nyingine part-time! unless anatakiwa awepo mda wote say mapokezi.

we have problem yes big one, we need good leaders to change the mind of these people, tatizo ni pale kuwa vingozi nao wanapitia system hiyohiyo!

waberoya
 
Ni kweli tuna kundi kubwa la watu wavivu (kama mimi). Lakini kama viongozi wangekuwa wanawajibika, wangekuwa na uwezo wa kukemea wasiowajibika. Kwa vile viongozi wengi ni watawala wasiowajibika, watawaliwa nao tumelemaa. Watanzania wanatakiwa kusahau kuwa maendeleo yao yatatokana na uongozi bora (ambao haupo). Kwa hali ya sasa maendeleo ya Mtanzania yatatokana na kila mmoja kuchukia hali aliyonayo na kuamua kubadilika. Ni vigumu kwa Tanzania kubadilika kama kundi.

Hii ni zawadi ya Christmass, UKWELI MTUPU, japo wengine utatuuma.

Viongozi nao si watanzania jamani? MULE MULE.
na hata yabia ya kusubiri kiongozi wako akukemee ndio uvivu wenyewe pia.
 
Upande mmoja tunaweza kusema kuna uvivu, na upande wa pili tunasema Taifa linazalisha wavivu. Mfano ukisafiri asubuhi na mapema, ukasimama vituo kama Chalinze, Namanga, Sirari nk. Utakuta watanzania kibao wameamka na wanatafuta riziki kwa kufanya biashara ya mazao yao ya kilimo ama bidhaa nyingine. Ingia ziwani ama baharini utakuta watu wanavua usiku wa manane. Niliwahi tembelea Tanga nikawakuta kina Mama na kina Baba wanalinda mpunga usiku usiliwe na ndege pale Pangani. Hawa wote sio wavivu, bali kama waliosema mwanzoni huwezi kufanya kazi kwa bidii halafu udhulumiwe. Wakulima wanalima, wakati wa mazao kununuliwa wanakopwa, kulipwa inakuwa mbinde. Wakilipwa wanaambiwa bei katika soko la dunia ilikuwa chini. Wavuvi pale ziwa Victoria, kaangalie zile mizani zinaopima Samaki kwenda viwandani, Samaki kilo mbili, atasomeka kilo 1.5, akifika kiwandani wanasema kaanza kuoza, labda achukue bei ya "reject fish". Inabidi auze hivyo hivyo manake hana pa kuwapeleka haraka.

Sasa kwa haya yote lazima TIJA ishuke kwa kila Mwananchi ambaye katika eneo lake la kazi anadhulumiwa. Angalia Mererani, wakati wachimbaji walipokuwa na maeneo yao huru, kabla ya kuingia wawekezaji, watanzania wenzetu walikuwa wanajituma. Na mambo yao yalikuwa yanaoneana pale Arusha mjini. Hivyo uvivu unachangiwa na mambo mengi, ikiwemo kutokuwajibika kwa waliopewa dhamana ya kutuongoza.
 
Tatizo ni Leadership Challenge: Miradi mikubwa (by country standard) yote iliyopo nchini wafanyakazi wake wengi ni wa-TZ, lakini angalia nani nyapara wao-ngozi nyeupe!!!! Hawa "wavivu" wakiwa chini ya kiongozi mzungu au hata mkenya-utaona wanavyochapa kazi kwa sababu bosi hana longolongo!. Kwahi yo tunalo tatizo la kutotaka kuonekana wanoko hasa wale ambao wako kwenye ngazi za usimamizi/uongozi. Kwenye sekta ya umma-balaa, maana hao watoa maamuzi wengi kama sio wote waliajiriwa bila-interview:Appointees, hapo balaa!
Ni muhimu kuangalia mfumo wetu wa uongozi (private, public and political) kwanza , jinsi gani yakuurekebisha !!
 
Naomba ndugu yangu katika hili niamue kutokubaliana na wewe.Umesema vizuri sana kwamba Tanzania kuna oungozi mbaya nk. nk.Sasa wewe huoni kwamba haya ndiyo yaliyowafikisha watanzania mahali walipo na hatimaye kukata tamaa na kupoteza matumaini kabisa?Hivi utafanya nini kama huna mtaji kabisa.?Naomba tuelewe kwamba watanzania sio wavivu.Hali yao ya kukata tamaa kufuatana na hali ilivyo nchini ndiyo iliyo wafikisha hapo walipo,wakiwezeshwa na kupewa matumaini wanaweza.Unastahili kuwaomba watanzania msamaha kama kweli wewe ni muungwana!


Tumesema mengi sana kuhusu Uongozi Mbaya tulionao . . . .
Tumesema sana kuhusu Ufisadi na Mafisadi . . . . .
Tumesema sana kuhusu Demokrasia mbovu . . . .
Tumesema sana kuhusu matumizi mabaya ya rasilimali zetu . . . . nk

Naomba sasa tuseme ukweli kama: Je. Watanzania Wengi ni Wavivu?

Zingatia yafuatayo ambayo kwa wengi wanajua ukweli wake:

  • Mfanyakazi anafika asubuhi kazini kachelewa, lakini bado anaenda Hotel au anatafuta kifungua kinywa na anakuwa hana haraka. Kazi anaweza kuanza saa tatu asubuhi.
  • Hapa katikati kama kuna chai ya saa nne, zoezi zima linachukua si chini ya nusu saa.
  • Lunch time inachukua si chini ya saa moja.
  • Kabla ya muda rasmi wa kumaliza kazi, wengi wanajiandaa kuondoka na si ajabu wakaondoka kamili au hata kabla ya muda
  • Safari na mikutano mingi ambayo haileti tija wala kuendana na ufanisi.
  • Bado kuna wengi wanapiga hadithi wakati wa kazi na kupunguza concentration ya kazi.
  • Matumizi ya simu kwa maongezi binafsi yanachukua muda mrefu
  • Wakati mwingine, maofisa husika hawapatikani ofisini wanakuwa wanafuatilia mambo yao binafsi.
  • Mambo mengi yanakwamishwa na maofisa husika kwa kuwa hana haraka na kazi au mpka ajue kuwa lile jambo lina maslahi yake.
  • Vijijini? Kilimo duni na uwajibikaji mdogo sana huku baadhi wakiwaachia wanawake majukumu mengi ya shambani na mengine mengi.
n.k, nk.

Kuna kiongozi mmoja wa kazi katika shirika aliwahi kusema, wanaofanya kazi kwa kuwajibika wakati wote ni kama asilimia tano tu. Katika asilimia 100% ya muda wa kazi, heunda ni asilimia 50% tu inatumika kwa kazi.

Je, shida yetu ni nini hasa? Tuwe wa kweli. Watanzania Wengi ni Wavivu? Nini kifanyike?

Inasikitisha sana
Inasononesha sana
Inafadhaisha sana
 
-Motisha mdogo
-Mapenzi madogo
-Mishahara midogo

Ufanisi Mdogo ndio unaozaa hayo.

Kwa hakika waTanzania tu wavivu sana, sio kwenye kazi tu, hata njiani ukitembea watu wanatembea taratibu tena bila malengo utafikiri hajui aendako. ndani ya vyombo vya usafiri watu wanakaa muda wote huoni anayesoma hata gazeti ah achilia mbali kusoma hata kumuana mtu akichezea game za kwenye simu hakuna mmoja. yaani mtu anakaa burebure hajishughulishi na chochote, hii inanishangaza na kuniumiza sana.
 
Watu wanazungumzia viongozi hawasimamii, kwani viongozi sio waTanzania???, tatizo ni la jumla ya waTanzania wote, awe kiongozi na asiwe kiongozi sote tuna tatizo hilo, chanzo chake sijui kimetokea wapi. Hata katika kazi zetu binafsi na biashara zetu, hatufanyi jitihada za ziada kupata ufanisi zaidi.
 
1. Mimi naona Watz wengi kwa sasa haswa ktk public sekta wanalalamika zaidi over rights za maslahi, mazingira bora ya kazi n.k kuliko nidhamu ya kazi (duties and responsibilities).
Nadhani perfomance appraisal ya kila mwezi..on WHAT ACTUALLY HAVE YOU PRODUCED?? ni muhimu! Na kama Productivity ni less that 50% then kuwe na consequences za penalty..kukatwa mishahara n.k.

2. Ikumbukwe tangu JK aingie madarakani mishahara ktk public secta imeongezeka kwa over 40% wakati inflation ni about 10%.

Ni wakati umefika kuteganisha siasa na nidhamu ya kazi..hakuna productivity..hakuna mshahara..period!

Nakumbuka wakati wa Sokoine na Mrema ukichelewa ofsini unakuta kiti kimechukuliwa..hii ndo spirit ya uoingozi thabiti! Kuwa na 'spot checks' saa 2 tu ni nani hajafika ofsini- na watu wasimamishwe kazi kwa uzembe..na utaona kama watu hawatawajibika!

Mimi siku zote nasema..tupate 'kiongozi kichaa' just to restore nidhamu ya kazi for 5 years...Watz wazoee kuwajibika!
 
Sikubaliani na hii dhana ya kuwa watanzania ni wavivu, ninachofahamu ni kuwa watanzania hawako serious na kazi za umma. Ukimkuta kaajiriwa katika kampuni ya binafsi, au kama anafanya shughuli zake binafsi utagundua kuwa mtanzania ni mchapaji kazi mzuri sana. Hebu fuatlia watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi uone jinsi wanavyobeba maboksi bila kujali.
........................!!!
Tatizo lililopo Tanzania ni mfumo mbovu wa uongozi na usimamizi tu. Kama viongozi wa kazi hawako serious ni dhahiri hata wafuasi pia hawatakuwa serious. Nadhani swali la kujiuliza ni kwa nini mfumo wetu wa usimamizi na uongozi uko vile katika taasisi zote za umma.
........................!!!
Katika experience yangu hiyo, ninachoona ni kuwa mfumo wa uongozi na usimamizi ndio uliobadilika na kusababisha utendaji wa kazi nao kuharibika.


naungana kwa pasenti mia na observation za Kichuguu juu ya hili.
Hakuna binadamu aliyezaliwa mvivu , ni yale mazingira yake yanamfanya mtu aonekane alivyo.Muundo wa usimamizi wa kazi , hasa za umma , hapa Tanzania ni mbovusana.
Twnde kwa mifano, chukua mfanyakazi wa Halmashauri yoyote ,kitengochochote hapa Dar.
-Kufika kazini saa 2.00, (anatafuta chai nusu saa)
-Kufanya kazi 2.30-4.00(4.00-6.00anondoka of mambo yake)
-Chakula cha mchana 6.00-8.00
-kufanya kazi 8.00-9.30(kupitia mafaili/wateja wachache)
-Porojo na vikao visivyo rasmi 9.30-10.00
-Kuondoka ofisini kwenda nyumbani

MASAA YA KAZI(EFFECTIVE)-MASAA 3
Kwa mwaka siku 300x3hrs -900hrs
(Mwaka una siku 365. siku 65 za likizo,offs etc)

Sasa kuna kampuni ya ninayoifahamu(siitaji jina)

-Kufika kazini 1.00
-Kazi 1.00-4.00
-Chai4.00-4.15
-Kazi4.15-6.00
-Chakula mchana 6.00-7.00
-Kazi 7.00-10.00
-Chai 10.00-10.15
-Kazi 10.15-12.00

MASAA YA KAZI (EFFECTIVE) MASAA 9.30

Kwa mwaka mzima 300x9.30- 2,850 hrs

Wadau tunaweza kuona kuwa WOTE tuna mtaji mmoja wa muda, lakini katika muda huo huo wendine wanafaya kazi ya masaa 900 wakati wengine ni masaa 2,850.
Huyu wa pili ni lazima aendelee kwa vyovyote vile na hili lipo Tanzania na tunaliona.
Kwa sekta ya umma, hta kumweka huyu mfanyakazi pale ofisini uzalishaji wake hautoshi kulipia gharama za mfanya kazi kuwepo pale(kiyoyozi,chai,usafiri etc).
Wadau bila kufanya analysis ya iana hii sioni jinsi ya kudhibiti upoteaji wa tija katika sekta ya umma.
 
Uvivu ni hali mtu anayojijengea mwenyewe au kujengwa na mfumo. Watanzania tulio wengi hatufanyi kazi kwa malengo, tunataka kusimamiwa, hatutaki kujiyuma. Utakuta mtu anafika ofisini akishasaini kitabu cha mahudhurio anaondoka kwenda kwenye shughuli zake. Siku ya mshahara wa kwanza kwenye foleni, akikosa mshahara wa kwanza kulalamika. Uvivu tumejijengea wenyewe. Mbona kwenye makampuni binafsi watu wanafanyakazi kama punda.

Angalia kwa mfano kampuni kama ya ujenzi wa bararabara. Mtu anapangiwa kuchimba mtaro kwa siku kadhaa na anamaliza kwa muda. Je uvivu upo kwenye sector za serikali tu. Tunatakiwa tufanye kazi kwa malengo tusitake kila wakati kusimamiwa?
 
Last edited:

...labda serikali ibadili system, tuwe nasi tunalipwa kwa masaa tunayoyafanyia kazi.
mfano; kima cha chini,

tshs 1'000/- kwa saa moja * masaa 7.5 (saba na nusu) ya kazi
=tshs 7'500/- kwa siku

mtu huyo kwa wiki ataingiza

tshs 7'500/- kwa siku * siku 5 za wiki = 37'500/- malipo yake ya jumla kwa wiki

ambayo ni sawa na

tshs 37'500/- kwa wiki * majuma manne katika mwezi = 150'000/-

kinyume na hapo, haya mambo ya uhakika wa malipo mwisho wa mwezi, hata kama kila wiki mfanyakazi anavisingizio vya 'nimefiwa na shemeji yake mke wa jirani', nk hayatakwisha!
 
Hivi ni visingizio tu maana hata wale wanaolipwa mamilioni hawana toafuti yeyote katika vigezo alivyovitoa Alien.

Tanzania haina vipimo vya kazi.Wala sizungumzii upuuzi kama Opras no. Hebu anagalia kiongozi anaweza kufanya jambo lisilo na tija , likailetea nchi hasara lakini hakuna wa kumwuliza matokeo ya alichofanya. Hivyo hivyo huko maofisini kwao hamna uwajibikaji na hakuna wa kumwuuliza mwienzake maana wote wako hivyo hivyo.

Mimi napiga kazi mahali fulani , najituma sana kibinafsi maana nimeona wenzetu huko nje wanavyofanya, ila sehemu hii ya kazi inaboa sana . Wakuu ni wabinafsi, wana upendeleo wa wazi wazi na mishahara sio even . Mimi na kimaster changu naona upuuzi, nimeamua kufanya biashara ambayo natumia muda wao mwingi kuimonitor. Sababu ni kuwa haka kabishara kananijali zaidi kuliko mwajiri wangu wa sasas. This is how life is in Bongo.
 
WaTanzania sisi Ni wavivu sana, kwa kukuhakikishia hebu hapo ulipo kama unaweza kutizama nje, ama waeza kutoka nje na kuangalia wapitao njiani utaona jinsi wanavyotembea kivivu. mtu hana haraka wala malengo ya aendako.
 
WaTanzania sisi Ni wavivu sana, kwa kukuhakikishia hebu hapo ulipo kama unaweza kutizama nje, ama waeza kutoka nje na kuangalia wapitao njiani utaona jinsi wanavyotembea kivivu. mtu hana haraka wala malengo ya aendako.

haha umenichekesha! maana nje kwangu kuna majaa wamekaa kwenye kaukuta cha bustani!! na kila siku wapo hapo. Pia niliwahi kusikia kuwa joto ndo linawafanya wabongo tuwe wavivu na tunatembea slowly..
 
Kwa ukweli usimamizi wa kazi ni mbovu sana Bongo.
Wenzetu wana time-sheets na performance reviews hata kwa wabeba box!! Ukichelewa hata dakika kumi inakua noma! Ukifanya ndo tabia lazima uitwe na HR manager!! Cant even imagine eti uchomoke lisaa lizima ukanywe Chai! ukirudi hauna kazi.
Vilevile watu wana lead by example, ukimwona supervisor wako amekamata ufagio anasafisha duka unajua watu wako serious.

Polepole watanzania wataanza kujifunza ku account for every minute wakiwa kazini.Kaika sekta binafsi hakuna utani -Usimamizi katika baadhi ya maeneo kama maduka makubwa -Game, Mr Price etc wanao utaratibu huu. Laiti usimamizi ungeimarishwa pia kwenye ajira ya umma.Kwenye mashirika ya kimataifa nako ni kibano mtindo mmoja..ukiwa mvivu utabwagwa chini hutachukua round.Performance assessment peke yake inakuonyesha mlango wa kuondokea.Sijui hiyo OPRAS serikalini kama inafanya kazi!
 

...labda serikali ibadili system, tuwe nasi tunalipwa kwa masaa tunayoyafanyia kazi.
mfano; kima cha chini,

tshs 1'000/- kwa saa moja * masaa 7.5 (saba na nusu) ya kazi
=tshs 7'500/- kwa siku

mtu huyo kwa wiki ataingiza

tshs 7'500/- kwa siku * siku 5 za wiki = 37'500/- malipo yake ya jumla kwa wiki

ambayo ni sawa na

tshs 37'500/- kwa wiki * majuma manne katika mwezi = 150'000/-

kinyume na hapo, haya mambo ya uhakika wa malipo mwisho wa mwezi, hata kama kila wiki mfanyakazi anavisingizio vya 'nimefiwa na shemeji yake mke wa jirani', nk hayatakwisha!

Huo ndio usimamizi wenyewe
 
Tanzania haina vipimo vya kazi.Wala sizungumzii upuuzi kama Opras no. Hebu anagalia kiongozi anaweza kufanya jambo lisilo na tija , likailetea nchi hasara lakini hakuna wa kumwuliza matokeo ya alichofanya. Hivyo hivyo huko maofisini kwao hamna uwajibikaji na hakuna wa kumwuuliza mwienzake maana wote wako hivyo hivyo.

Huo ndiyo ukweli viongozi wa serikali na mashirika wanachangia sana kuhusu hili suala la uvivu. Angalia ATCL Management na Board wamechangia kuliingiza shirika hili katika matatizo makubwa sana, lakini hadi hii leo bado wanapeta tu na kupokea mishahara yao minono na marupurupu wakati shirika haliingizi pesa yoyote katika hali kama hii tunategemea kweli mfanyakazi wa kawaida awe na motisha wa kufanya kazi wakati anaona shirika limehujumiwa na viongozi wa juu lakini hakuna wa kuwagusa?
 
Huo ndiyo ukweli viongozi wa serikali na mashirika wanachangia sana kuhusu hili suala la uvivu. Angalia ATCL Management na Board wamechangia kuliingiza shirika hili ktika matatizo makubwa sana, lakini hadi hii leo bado wanapeta tu na kupokea mishahara yao minono na marupurupu wakati shirika haliingizi pesa yoyote katika hali kama hii tunategemea kweli mfanyakazi wa kawaida awe na motisha wa kufanya kazi wakati anaona shirika limehujumiwa na viongozi wa juu lakini hakuna wa kuwagusa.

Tatizo liko kwenye performance assessment.Ingekuwa kila mtu anaweka malengo ya mwaka kufuatana na strategic plan ya taasis, halafu wakapimwa katikati na mwisho wa mwaka nadhani kila mmoja angekuwa macho kujipima mwenyewe kabla ya kusubiri msemakweli mwisho wa mwaka.No wonder hakuna anayejali maana wanajua mwisho wa siku ni business as usual.Hakuna adhabu yoyote.
 
Tanzania haina vipimo vya kazi.Wala sizungumzii upuuzi kama Opras no. Hebu anagalia kiongozi anaweza kufanya jambo lisilo na tija , likailetea nchi hasara lakini hakuna wa kumwuliza matokeo ya alichofanya. Hivyo hivyo huko maofisini kwao hamna uwajibikaji na hakuna wa kumwuuliza mwienzake maana wote wako hivyo hivyo.

Mimi napiga kazi mahali fulani , najituma sana kibinafsi maana nimeona wenzetu huko nje wanavyofanya, ila sehemu hii ya kazi inaboa sana . Wakuu ni wabinafsi, wana upendeleo wa wazi wazi na mishahara sio even . Mimi na kimaster changu naona upuuzi, nimeamua kufanya biashara ambayo natumia muda wao mwingi kuimonitor. Sababu ni kuwa haka kabishara kananijali zaidi kuliko mwajiri wangu wa sasas. This is how life is in Bongo.


Huo ndio usimamizi wenyewe tunaokosa.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom