TONGONI
JF-Expert Member
- Feb 18, 2011
- 1,041
- 373
hahaha, yaani ugiriki unakula raha? raha gani hapo rafiki yangu nchi inafilisika dunia nzima tunaona? hivi ungekaa America na canada ambako nimekaa miaka mingi si ndo ungejiona upo mbinguni?...kwa kifupi wewe ni limbukeni mtupu....si kwamba sisi wengine hatujaishi huko, tumeishi na tumeshafanya sana hizo kazi za mabox na kulelewa na wanawake wakizungu matajiri....tulishatengeneza hela lakini yote kwa yote, hakuna sehemu mwafrika anapata heshima na raha kama africa..ulaya ni dharau mtindo mmoja na hakuna maisha ya raha kwa mwafrica. ona sasa mnavyotia huruma hata kwenye picha tu, mmechokaaaa.....rudi hapa home na icho kidogo ulichokipata ujenge walau sehemu ya kufikia, ukifa utawekwa kwenye kibanda cha nani? njo uweke miradi hapa, kuna pesa nyingi kuliko huko kwa wazungu..sisi wengine tulishastaafu muda mrefu kubeba mabox....kalagabaho.
Kwenye red umeongea pumba,blue umeongea point...Unaongea kitu usichokijua huko unakosifia US na Canada mtu akifa mna changishana nchi nzima ndio msafirishe maiti kuzikwa nyumbani na mara nyingi hazitimii,lakini misiba yote ya Ugiriki kwa hali na mali watu wanasimama kidedea mpaka maiti inasafirishwa...Nimeshuhudia watu wakitoka US,Canada na hata UK akifika ugiriki anashangaa watu wanavyoisha...Huwezi kuwa mwanaume uliyekamilika unasimama mbele za watu bila aibu unajisifu kuwa umewekwa ndani na tipwa tipwa la kizungu 'what a shame!'
Kweli sasa hivi Ugiriki imechoka tena sana,na Dunia nzima inalijua hili.