chash
JF-Expert Member
- Jun 5, 2012
- 548
- 230
hahaha, yaani ugiriki unakula raha? raha gani hapo rafiki yangu nchi inafilisika dunia nzima tunaona? hivi ungekaa America na canada ambako nimekaa miaka mingi si ndo ungejiona upo mbinguni?...kwa kifupi wewe ni limbukeni mtupu....si kwamba sisi wengine hatujaishi huko, tumeishi na tumeshafanya sana hizo kazi za mabox na kulelewa na wanawake wakizungu matajiri....tulishatengeneza hela lakini yote kwa yote, hakuna sehemu mwafrika anapata heshima na raha kama africa..ulaya ni dharau mtindo mmoja na hakuna maisha ya raha kwa mwafrica. ona sasa mnavyotia huruma hata kwenye picha tu, mmechokaaaa.....rudi hapa home na icho kidogo ulichokipata ujenge walau sehemu ya kufikia, ukifa utawekwa kwenye kibanda cha nani? njo uweke miradi hapa, kuna pesa nyingi kuliko huko kwa wazungu..sisi wengine tulishastaafu muda mrefu kubeba mabox....kalagabaho.
Mkuu, the end justifies the means. Wewe kama umeshatimiza ndoto zako na ukarudi nyumbani, hongera, lakini usiwakatishe wengine tamaa. Unajua ukweli vizuri na hao wanaujua pia, huwezi kulinganisha maisha ya hapa na majuu hata siku moja, kwa njia yeyote. Labda uwaambie wawekeze hapa investments kama nyumba, kilimo na biashara na hii inashindikana kwa kuwa wanakosa watu waaminifu kuwasimamia miradi yao. Nadhani ndio kilicho kurudisha. Kama unachokisema kina ukweli wasingekusubiria mtu kuwaambia njoeni, wangesharudi siku nyingi. Majuu, hata kama unafanya kazi ya kudharaulika namna gani una uwezo wa kutoka na kuwa tajiri kwa standard za hapa. Lakini hapa watu waliokuwa wengi wamendikiwa umasikini maisha yao yote, kusota na kuishi hand to mouth, watu wapo majuu wamefungwa jela lakini wanaishi vizuri zaidi ya walio wengi hapa. Tusidanganyane mkuu.