Watanzania Wasota Jela Iran

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
Watanzania zaidi ya 50 wanaodaiwa kusamehewa na serikali ya Iran baada ya kufungwa jela kwa makosa ya kukutwa na madawa ya kulevya wanaendelea kusota jela nchini humo kufuatia kusubiri kibali cha Serikali ya Tanzania kuruhusu waachiwe.

Watanzania hao wanaodaiwa kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitano sasa, ndugu na jamaa zao wanasubiri kibali hicho ili jamaa zao waweze kuachiwa.

Kwa mujibu wa mmoja wa ndugu wa wafungwa hao, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, serikali ya Iran inasubiri kibali kutoka Tanzania ili iweze kuwaachia Watanzania hao.

“Fikiria, ndugu zetu wanaendelea kuteseka jela wakati serikali ya Iran imeshawasamehe, hivi serikali inashindwa nini kuandika hiyo barua waweze kuachiwa hawa ndugu zetu?” aliuliza.

Alisema ingawa ndugu zao walikutwa na makosa na kufungwa lakini wameshakaa jela miaka mingi na wameshajifunza ni bora serikali ingewaonea huruma kwa kutoa kibali cha kuruhusiwa.

Hata hivyo, NIPASHE Jumapili ilipowasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imesema haina taarifa ya kuachiliwa kwa baadhi ya Watanzania waliofungwa nchini Iran, na kuwataka ndugu na jamaa wa watu hao kwenda wizarani hapo kwa ajili ya kupewa msaada.

Afisa Uhusiano wa Wizara hiyo, Ally Kondo alisema mpaka juzi Wizara hiyo haijapata taarifa kutoka Serikali ya Iran ikiwaarifu jambo hilo hivyo itakuwa vyema kwa ndugu wa watu hao kufika hapo kuanza taratibu za kuwarudisha nyumbani.

Alisema kwa ujumla kuna Watanzani, wengi wamefungwa nchini humo kwa makosa mbalimbali na kama wangepata taarifa hizo Wizara hiyo isingesita kuchukua hatua ya kuiandikia barua Iran ikitaka kuwarudisha nchini.

"Sisi hapa hatuna tatizo la kuandika barua za namna hiyo, tatizo hatujapata taarifa kutoka Serikali ya Iran wala ndugu wa hao watu hawajafika hapa, sasa naomba kama ndugu wa watu hao wapo waje hapa tuanze utaratibu wa kuwarudisha,' alisema Kondo.

Alisema, utaratibu wa kuwarudisha nyumbani watu wa aina hiyo unafanywa kila mara pale panapopatikana taarifa kamili kutoka kwa ndugu au Serikali ya nchi husika.

CHANZO: NIPASHE JUMAPIL
 
Hivi Iran ni nchi mojawapo inayofuata sheria za kunyonga ukikutwa na madawa ya kulevya? Ilikuwaje hawa watz wakaachiwa huru?
 
Watanzania zaidi ya 50 wanaodaiwa kusamehewa na serikali ya Iran baada ya kufungwa jela kwa makosa ya kukutwa na madawa ya kulevya wanaendelea kusota jela nchini humo kufuatia kusubiri kibali cha Serikali ya Tanzania kuruhusu waachiwe.

Watanzania hao wanaodaiwa kufungwa jela kwa zaidi ya miaka mitano sasa, ndugu na jamaa zao wanasubiri kibali hicho ili jamaa zao waweze kuachiwa.

Kwa mujibu wa mmoja wa ndugu wa wafungwa hao, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, serikali ya Iran inasubiri kibali kutoka Tanzania ili iweze kuwaachia Watanzania hao.

"Fikiria, ndugu zetu wanaendelea kuteseka jela wakati serikali ya Iran imeshawasamehe, hivi serikali inashindwa nini kuandika hiyo barua waweze kuachiwa hawa ndugu zetu?" aliuliza.

Alisema ingawa ndugu zao walikutwa na makosa na kufungwa lakini wameshakaa jela miaka mingi na wameshajifunza ni bora serikali ingewaonea huruma kwa kutoa kibali cha kuruhusiwa.

Hata hivyo, NIPASHE Jumapili ilipowasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imesema haina taarifa ya kuachiliwa kwa baadhi ya Watanzania waliofungwa nchini Iran, na kuwataka ndugu na jamaa wa watu hao kwenda wizarani hapo kwa ajili ya kupewa msaada.

Afisa Uhusiano wa Wizara hiyo, Ally Kondo alisema mpaka juzi Wizara hiyo haijapata taarifa kutoka Serikali ya Iran ikiwaarifu jambo hilo hivyo itakuwa vyema kwa ndugu wa watu hao kufika hapo kuanza taratibu za kuwarudisha nyumbani.

Alisema kwa ujumla kuna Watanzani, wengi wamefungwa nchini humo kwa makosa mbalimbali na kama wangepata taarifa hizo Wizara hiyo isingesita kuchukua hatua ya kuiandikia barua Iran ikitaka kuwarudisha nchini.

"Sisi hapa hatuna tatizo la kuandika barua za namna hiyo, tatizo hatujapata taarifa kutoka Serikali ya Iran wala ndugu wa hao watu hawajafika hapa, sasa naomba kama ndugu wa watu hao wapo waje hapa tuanze utaratibu wa kuwarudisha,' alisema Kondo.

Alisema, utaratibu wa kuwarudisha nyumbani watu wa aina hiyo unafanywa kila mara pale panapopatikana taarifa kamili kutoka kwa ndugu au Serikali ya nchi husika.

CHANZO: NIPASHE JUMAPIL

Bila shaka ni wale jamaa zetu! Sharia ichukue mkondo wake
 
Hapo wameshapiga hesabu ya gharama za kuwarudisha na wakati kichaa anaongeza Dreamliner sahau.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom