Watanzania wapuputika

Nionavyo mimi, hakuna dini inayoruhusu kufanya mambo ya hovyo ambayo ni dhambi. Mimi ni mkristu mkatoliki, na nimesoma vitabu vitatu vinne hivi ambavyo vinahusisha moja kwa moja Vatican na biashara haramu za mafia kwa mfano Vatican Connection, In God's name, Costra Nostra na hata Godfather ya Mario Puzo. Does it mean Catholism allows what mafias are doing? No way!! Ni collaboration ya mafia na corrupt church officials wachache ambao wwalikuwa kwenye position za kuongoza. Kwa mantiki hiyo ntaliangalia hili tatizo kama liko general kuliko ku base ktk influence ya dini.
Mazingira ya watu wa pwani ambayo wengi wao ni waislamu, ni ya ubaharia, kilimo na uvuvi. Umaskini upo sana na mazingira hayo yalichochea vijana wengi kurubuniwa kuwa utajiri wa haraka ni kudandia meli na kuenda mtoni.
Tukumbuke pia umwinyi miongoni wa watu wa maeneoa hayo huendana endana na katabia ka uvivu ambacho hakawezi kumkwamua mtu kutoka katika umaskini. Ndio maana hata shule watu wengi wa pwani hawakutulia umaanani..leo wengine wachache wanaendesha kampeni kuwa walidhulumiwa kitu ambacho nionavyo sio sahihi.
Lakini hata hivyo kama Taifa leo kuna mambo mengi yanayotishia mustakabari wetu na ni aibu kubwa machoni kwa watu wa mataifa mengine.Kwa mfano, kuua albino kwa ajiri ya utajiri, rushwa kubwa kubwa za viongozi waandamizi yote haya hayatoi picha nzuri huko nje.Nigeria iko hivyo hivyo ndo maana wanajulikana dunia nzima mana kuanzia viongozi walio wengi ni wezi na matapeli mpaka watu wa chini kabisa.
Hili linatugharimu sana sio tu kwa wauza dawa bali sisi kama taifa mana tunajiharibia.
Imefikika wakati sasa nionavyo mimi, tuhimize watu kuwa na skills ambazo zitatufanya tuuzike sehemu nyingi za dunia na kufanya kazi kutupatia utajiri kuliko hizi short cut tunazochukua.
Tupende kuheshimiana pamoja na tofauti za dini zetu badala ya kuanzisha malumbano ambayo hayatakuja kupata mshindi. Imani ni kitu kigumu sana kukibadili kwa malumbano mana kimejishika pale mtu roho yake ilipo.
Hizi mindset zetu zinahitaji mabadiliko, vinginevyo tutakazana kufanya mambo yasijo na tija ya wizi na kuuza dawa halafu wajanja wanatuibia kwa kujiita ma investor. Ni kunuia kupata elimu bora tu ndio utakuwa msaada wetu nionavyo mimi.
Mungu Ibariki Tanzania
 
Nakubaliana kabisa na Muheshimiwa Bowbow na maoni yake juu ya janga hili la madawa ya kulevya.Mitaani kuna vijana wanajulikana kama makontena, ukiwa na utumbo mkubwa tena ndo kontena haswa!!
Hata hivyo sikubaliani na kichwa cha mada-"WATANZANIA WAPUPUTIKA"
kUPUPUTIKA maana yake nini haswa.Je ni KUPUKUTIKA au KUPAPATIKA?
KUPUKUTIKA inaelezea kuisha/kufa mmoja baada ya mwingine,
PUPAPATIKA inelezea kubabaikia maisha na kutojua lile la kufanya
Bila kuiwater down mada ya Bowbow sijui kama ametumia neno sahihi.
 
Unachosema mkuu sio kigeni, wanaowatuma hao vijana kwenda huko wafahamika kabisa, na muungwana ana list yao na huko wanakokwenda huwa baadhi wanatajwa. Kubwa ni kuwa ukiongea sana issue hii mwisho unakuwa kama yule mtangazaji wa clouds FM. Serikali ina uwezo kabisa wa kupambana na tatizo hilo, ina uwezo wa kurudisha sifa na kulinda image ya watanzania ndani ya nusu mwaka tu. Kwanini haifanyi hivyo? that is a big question!
 
Ndugu zangu nafikiri tumeacha hoja ya msingi na tumedandia mambo ambayo nafikiri yameletwa au kuanzinshwa kwa bahati mbaya tu. Issue ni kuwa kwanini watanzania wengi tumekimbilia katika biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya na kuharibu sifa ya watanzania wengine ambao wana nia na biashara nzuri tu huko nje au wameenda kutafuta maisha kwa kufanya kazi halali. Nafikiri hiyo ndio hoja.

Kwa maoni yangu nafikiri watu tumekuwa na tamaa ya kupata hela za chapu chapu sana kiasi kuwa tumediriki kufanya mambo ambayo sio halali kuanzia biashara ya madawa ya kulevya, then viungo vya albino na ufisadi all these a elements of quick self enrichments. lakini nahao wenye hela ndio wanaoharibu vijana wetu, ndio hao wanawatuma wawasafirishie madawa au wakawaletee vioungo vya albino ili wapate hela zaidi then baada ya kupata hela wanataka protection so they run for political post.

we need to think aloud and re-evaluate ourself whether what we are doing is the right things .
 
Inawezekana kana walivyosema wengine watu wa Pwani ndio wanaopenda kushiriki kwenye hiyo biashara, sawa. Mbona tuna walaumu sana wasukuma kwa kuuwa vizee kwa tuhuma za kishirikina? Mbona tunawalaani sana wachaga tunasema wezi, mbona tunawalaaani sana wahaya tunasema wakabila na mengine mengi lakini linapokuja hili la madini ni watu wa Pwani na sio uislam.

Je hiyo tabia ya Wasukuma ya kuuwa wazee kiushirikina, Wachaga na wizi wao, Wahaya na ukabila bila kusahau ile biashra yao ya vibatari (Sina uhakika kama bado inaendelea) na watu wa mkoa wa Mbeya, mkoa unao ongoza kuwana makanisa na ushirikina wa kuuwana... Je hao nao na hayo wanayo yafanya nahisi ni kutokana na Ukristo wao...! lol! Kaaazi kweli kweli... Ama kweli Watanzania wapuputika (!!?) Poleni waislam kwa kutokuwa wasomi... Maana Taifa ili la wabongo lingewaingiza kwenye lawama kubwa la muanguko wa maadili, uchumi m'bovu... Elimu hisiyokuwa na mwelekeo... Bora hivyo hivyo nyerere alivyowapiga kibuti mkawa nje ya sirikuu a.k.a serikali kutokana na kutokuwa wasomi... lol.
 
Back
Top Bottom